Yusufu Fundi Seremala

Yusufu Fundi Seremala

Nchaby

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
797
Reaction score
259
Wakuu, hapa pameniwea pagumu kuelewa. Lakini naamini katika jukwaa hili, wapo watu waliobobea na waelewa historia ya biblia kwa kiwango cha juu mno kisicho na shaka.

Biblia ninayoisoma inataja Yusufu mwana wa Yakobo aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri (Mwanzo 37:2-36)

Vilevile, inataja Yusufu mwana wa Yakobo; fundi seremala aliyemchukua Mariamu kuishi naye na hatimaye kuzaliwa kwa mtoto Yesu Jerusalem katika banda la ng'ombe (Mathayo 1:16)

Hapa nashindwa kuelewa!
Yusufu aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri, ndiye baadae alikuwa fundi seremala na kumlea mtoto Yesu alipozaliwa?
Au hawa Yusufu ni watu wawili tofauti?

Historia ya maisha wana wa Israel ni ndefu sana na wakati mwingine haiko wazi sana kiasi kwamba sisi wengine ambao siyo wabobezi wa maandiko tunapata shida sana kuelewa na kupambanua kwa kina maandiko.

Maisha ya wana wa Israel yamejawa na kuanguka na kusima mara kwa mara. Vile vile historia inasema mara zote wana wa Israel walipotii sheria za Mungu na kukubali kufanya kazi yake; maisha yao yalikuwa yenye furaha, amani na mafanikio makubwa kinyume chake ilikuwa ni kuanguka na kukumbwa na mateso.

Baada ya hawa wateule wa kufanya kazi ya Mungu, kutoka utumwani Misri, inasemekana, walianguka tena, wakawa watumwa kwa mara nyingine tena!

Wajuzi na wabobezi wa maandiko, nisaidieni; hili taifa teule la Mungu, nini kiliwakumba kwa mara yapili na hatimaye kwenda kuwa watumwa?

Ni taifa gani liliwatumikisha kwa mara nyingine Waisraeli na walishikiliwa utumwani kwa kipindi gani?
 
Hao ni watu wawili tofauti mfano jina lako kuna mtu mwingine analitumia. Huyo yusuph alikuwa mtoto wa yakobo ndugu zake walimuuza akapelekwa misri, huko alikaa kama mtumwa lakini baadae mambo ya limnyookea hata akawa waziri wa nchi ya misri.

Njaa iliingia dunia nzima iliyopelekea watu kuingia misri kununua vyakula maana wao walikuwa na akibaa kubwa!

Ndugu zake na yusuph baada yakusikia chakula kipo misri nawao walienda kununua huko wakakutana na yusuph ambaye wao ndiyo waliomuuza.

Yusuph alijitambulisha kwao na akawaambia wakamlete mzee wao ambaye ndiye yakobo au Israeli kwahiyo familia yote ya mzee yakobo ilihamia misri ikiwa na watu 72!

Huko walikaa na kuongezeka na baadae mzee yakobo alikufa na farao pia pamoja na yusuph hata nakile kizazi cha kwanza. Farao alieingia hakumjua yusuph na pia aliona waisrael wanazidi kuongezeka kwahiyo akaamuru wawe wanafanywishwa kazi ngumu na watoto wakiume watakao zaliwa wauuwe.

Huko misri walikaa miaka 400 baadae walitolewa na Musa.
 
Mkuu, nimekupata!!
Umepapasa tu! Lakini kiu yangu imebakia pale pale!
Kama hawa Yusufu ni watu wawili tofauti! Mbona Biblia inawataja wote kama wana wa Yakobo?
 
Yakobo alikuwa na wana 12 katika hao wana mmoja wapo aliitwa yuda kwa hiyo yusuph ametoka kwenye kizazi cha yuda ambaye baba yake ni yakobo.
 
Halafu yuda huyo huyo alimlala mke wa babake hadi babake akamfukuza,sasa
Siyo yuda ni Ruben na ndio maana wanasema uzao wake haukupata urithi

Ila naye Yuda alimtafuna mkwe wake kiajali ajali [emoji1][emoji1]..hatari sana
 
Mkuu, nimekupata!!
Umepapasa tu! Lakini kiu yangu imebakia pale pale!
Kama hawa Yusufu ni watu wawili tofauti! Mbona Biblia inawataja wote kama wana wa Yakobo?
Yakobo ndio shina la Israel, au kwa kifupi ndio Israel kwa jina lingine, (alikuwa akiitwa Yakobo lakini baadaye Mungu alimpa jina la Israel) kwa hiyo kuanzia watoto wake hadi wajukuu na waisrael wote wanaitwa wana wa Yakobo,

Ukitaka kuielewa Biblia vizuri huna jinsi zaidi ya kuisoma kuanzia historia ya Abrahamu (Ibrahim) ambayo inaanzia kwenye kitabu cha Mwanzo hadi angalau kwenye vitabu vya Mambo ya nyakati..

Ni ngumu na inachosha lakini hamna namna.
 
Mkuu, nimekupata!!
Umepapasa tu! Lakini kiu yangu imebakia pale pale!
Kama hawa Yusufu ni watu wawili tofauti! Mbona Biblia inawataja wote kama wana wa Yakobo?
Kwani kuna john joseph wangapi hapa bongo?
 
Hao ni watu wawili tofauti. Eliudi akamzaa Eliazer, Eliazer akamzaa Matani, na Matani akamzaa Yakobo na Yakobo akamzaa Yusufu ambaye ndie aliye mposa Mariam.

Ukija kwa Yusufu aliye kuwa waziri mkuu Misiri. Ibrahimu akamzaa Isaka, na Isaka akamzaa, Esau na Yakobo, na Yakobo na akamzaa, Rubeni, simion, Yuda, Gadi, Yusufu n.k jumla walikuwa wanaume 12,
 
Achana na hizo hadith za kufikirika hata huko misr hao watu hawafatilii hizo hadith achana nazo usiumize kichwa hata wakiwa 10 hawakusaidii kitu
 
Wakuu, hapa pameniwea pagumu kuelewa. Lakini naamini katika jukwaa hili, wapo watu waliobobea na waelewa historia ya biblia kwa kiwango cha juu mno kisicho na shaka.

Biblia ninayoisoma inataja Yusufu mwana wa Yakobo aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri (Mwanzo 37:2-36)

Vilevile, inataja Yusufu mwana wa Yakobo; fundi seremala aliyemchukua Mariamu kuishi naye na hatimaye kuzaliwa kwa mtoto Yesu Jerusalem katika banda la ng'ombe (Mathayo 1:16)

Hapa nashindwa kuelewa!
Yusufu aliyeuzwa na ndugu zake utumwani Misri, ndiye baadae alikuwa fundi seremala na kumlea mtoto Yesu alipozaliwa?
Au hawa Yusufu ni watu wawili tofauti?

Historia ya maisha wana wa Israel ni ndefu sana na wakati mwingine haiko wazi sana kiasi kwamba sisi wengine ambao siyo wabobezi wa maandiko tunapata shida sana kuelewa na kupambanua kwa kina maandiko.

Maisha ya wana wa Israel yamejawa na kuanguka na kusima mara kwa mara. Vile vile historia inasema mara zote wana wa Israel walipotii sheria za Mungu na kukubali kufanya kazi yake; maisha yao yalikuwa yenye furaha, amani na mafanikio makubwa kinyume chake ilikuwa ni kuanguka na kukumbwa na mateso.

Baada ya hawa wateule wa kufanya kazi ya Mungu, kutoka utumwani Misri, inasemekana, walianguka tena, wakawa watumwa kwa mara nyingine tena!

Wajuzi na wabobezi wa maandiko, nisaidieni; hili taifa teule la Mungu, nini kiliwakumba kwa mara yapili na hatimaye kwenda kuwa watumwa?

Ni taifa gani liliwatumikisha kwa mara nyingine Waisraeli na walishikiliwa utumwani kwa kipindi gani?
umelitumia sana neno historia,lakini ukweli ni kwamba biblia sio kitabu cha historia
hakuna kitabu cha historia kinachoelezea hao wanaoitwa waisraeli kuwa utumwani misri
 
Unaelewa nini kuhusu neno " historia" ?
 
Unaelewa nini kuhusu neno " historia" ?
roughly,historia unaweza kusema ni study ya matukio yaliyopita ambayo yamekuwa documented au narrated
matukio hayo yawe yameandikwa na mwandishi mmoja au zaidi ambae/ambao uwepo wao(their existence) hautiliwi shaka
mfano historia ya misri kama ilivyoandikwa na aristotle,plato nk
 
Back
Top Bottom