DOKEZO Yusuph Kitumbo mkurugenzi KITAYOSCE Anayetoa rushwa michezoni kwa kurubuni wachezaji. TFF Chukua hatua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Yusuf Kitumbo ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Cheyo Manispaa ya Tabora kwa mara nyingine yupo katikati ya tuhuma za rushwa na kupanga matokeo kwa ligi daraja la kwanza.

Alifungiwa mwaka 2016 na utawala wa Jamal Malinzi kwa kupanga matokeo ya ligi daraja la kwanza akiwa Mwenyekiti wa Tabora, yeye na Katibu wake Fateh Rhemtulla wakafungiwa maisha na Utawala wa Malinzi ambapo Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia alikuwa Makamu wa Rais.

Miaka kadhaa baada ya Utawala wa Karia kuingia madarakani ukamfungulia Kitumbo ambaye alikata rufaa, akagombea tena nafasi ya Mwenyekiti wa Tabora akishindana na Dick Mlimuka aliyeondolewa baadae kwa madai ya kurununi wapiga kura wa Wilaya ya Urambo kwenye uchaguzi wa Wilaya.

Mlimuka alifungiwa miaka 10 hali iliyomfanya Kitumbo kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya Uenyekiti. Muda mfupi tu baada ya kushinda Uenyekiti, akiwa Diwani na Mkurugenzi Mtendaji wa KITAYOSCE anatuhumiwa kupanga matokeo tena kwa kuwarubuni wachezaji wa Fontain Gate na kurekodiwa akiahidi pesa alizokuja kutuma baadae (Tshs 2,470,000/=) ili wachezaji waachie mechi.

Inawezekana Karia na wenzie hawakuwa na nia mbaya walikuwa na nia njema kwakuwa mpira unahitaji watu wenye uwezo wa kuusaidia kipesa na Kitumbo ni mfanyabiashara anaweza kuwa msaada, lakini ameingiza mpira kwenye matope tena.

Hali inayoonekana kama vile mtu aliyemhurumia mwanawe katika malezi kwa kumfanyia mambo mazuri anayopenda tu lakini anakuja kuharibika kwakuwa kijana asiye na nidhamu wala maadili katika jamii.

Mpira wetu unahitaji sana wafanyabiashara, lakini hauhitaji wafanyabiashara wa kutumia pesa zao kupanga matokeo kwa kurubuni wachezaji au waamuzi kwa manufaa ya vilabu wanavyoviongoza.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa kuhusishwa na kupanga matokeo sio kitu kidogo, tena na sauti pamoja na miamala ya kutuma pesa ikionekana, linapaswa kufatiliwa kikamilifu na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu, mpira wetu una rushwa kila mahala, lakini viongozi wakuu wakijiingiza huko basi tumekwisha.

BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)

Huyo bwana nimemkumbuka, alikuwa mmiliki wa mabasi ya KITUMBO, iliyofilisika. Si mfanyabiashara, ni mission town mzaliwa wa Morogoro na pia ana makazi Dodoma. Pesa yake anapata munispaa ya Tabora kwa miradi hewa kata ya Cheyo. Pesa ya Miradi kwenye kata hiyo huishia kugawana kati ya maafisa wa manispaa na diwani mh Kitumbo. Nikifika Cheyo usiku, nilichoka. Barabara ya lami ni kipande cha mita 250, zingine zote ni mashimo na mitaro.
 
Back
Top Bottom