Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Yusuph Manji achukua fomu
04/06/2012
Taarifa rasmi na za uhakika alizozipata Shaffi Dauda kutoka makao makuu ya klabu ya Dar Young Africans almaaruf Yanga Sports Club, zinasema mwanachama maarufu na tajiri wa klabu hiyo, mfanyabiashara Yusuph Mehebob Manji amechukua fomu za kugombea nafasi ya Uenyekiti wa klabu hiyo.
Manji ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiisadia Yanga kiuchumi zaidi, alikwenda kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kuchukua fomu za Uenyekiti bila kuweka wazi kama ni kwa ajili yake au amemchukulia mtu kwa ajili kugombea nafasi hiyo.
Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na taarifa juu ya Manji kutaka kugombea nafasi hiyo japo mwenyewe bado hajathibitisha, ingawa kitendo chakecha leo kimezidi kuupa nguvu uvumi wa kwamba anataka kugombea nafasi ya kuwa bosi wa Yanga.
Wakati huo huo taarifa nyingine zinasema kuwa aliyekuwa mjumbe Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Binkleb naye muda wowote kutoka sasa atadondoka makao ya Yanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea umakamu mwenyekiti.
Mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo Issac Mazwile naye ameshachukua fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.
Naye Mkuu wa wilaya ya Handeni, bwana Muhingo Rweyemamu amechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Julai 15, 2012. Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis, Kaswahili amemwambia Dina Ismail kwamba jana kwamba wanachama hao wanafanya idadi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafsi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo kufikia 10 (baada ya taarifa hapo juu ya Manji kuchukua fomu, sasa idadi itakuwa 11).
Mbali na hao, wanachama wengine waliochukua fomu ni pamoja na John Jambele anayewania Uenyekiti, huku Ayoub Nyenzi akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, "Waliochukua fomu kuwania ujumbe wa kamati ya Utendaji mbali na Muhingo na Binkleb ni Isaac Chandi, Jumanne Mwamwenye na Salehe Hassan," alisema.
Source: wavuti - wavuti