Scania ni noma; Mbeya-Dar kuna Happy Nation (Sauti Ya Manka), Arusha-Dar kuna Chakito(Ndama Jeuri au Masogange) Ngorika(Nazareth au Macedonia), Mwanza-Day Kuna Ally's Sport Bus. Hayo mabasi niliyataja hapo hakuna Yutong ishawahi kuyaona hata yalipopita...
Nachangia kwa utaalam as mechanical engineer, Youtong technlojia na design iliyotumika kulitoa basi hilo kwa matumizi inaruhusu gari hilo kulala kwa nyuzi 52 (fitytwo degrees) wakati mabasi mengine including scania ni 32 degrees that means ikitokea kuyumba na tairi zikanyanyuka upande mmoja kwa mlalo nilioutaja, Youtong iko vizuri kurejea barabarani bila madhara tofauti na scania
Kwenye sifaza chuma kigumu na majina hiyo ni kwa miaka tuliyopita ni kweli tulihitaji mabasi yanayodumu kwa muda wa miaka mingi lakini sasa tunahitaji teknolojia ya kukuwezesha kufika kwa muda mfupi, comfortably na luxurier mambo ya unaisikia scania inavyolalamika mlimani htutaki!!!
Bado hakuna kampuni ya kuishinda Scania. Na labda huko ambapo Yutong zinasumbua wana Scania model za zamani. Sasa hivi kuna Scania F330 ambako kwa Mwanza wanazo kampuni ya Ally's, kwa Mbeya kuna Nganga, Budget, Moshi na Arusha kuna Dar-Express na mengineyo. Bado hakuna Yutong ya kukimbizana na hizo gari. Ina Scania Euro6 engine 9.0L Turbo Intercooler plus Turbo Compound inayogenerate 330HP na 1600 Nm of Torque and a top speed of 130kph (Scania Euro 6 buses and coaches) ulinganishe na Yutong yenye engine ya Cummins 300HP Turbo and the max speed of 110kph(ZK6116D-YUTONG). Nissan Diesel haziwezi kupambana na hao wawili kwa kuwa hazinaga Turbo ila zina sifa ambayo hayo yote hapo juu hayana nayo ni uwezo wa kwenda safari ndefu mno. Ukitaka kuhakiki angalia kampuni zenye mabasi yanayokwena nje ya nchi..
Mabasi yenye injini nyuma, yakiwemo ya Scania, hayafai kwa barabara na mazingira yetu ya Afrika, hasa kwa nchi kama Tanzania. Itakumbukwa kuwa Scania waliwahi kuleta mabasi ya modeli K93 na K113 yenye injini nyuma katikati ya miaka ya 1990 lakini hayakuwa na mafanikio katika soko kutokana na kuchakaa haraka na kusumbua katika matengenezo. Miongoni mwa makampuni ya usafirishaji yaliyokuwa na aina hii ya mabasi ni Kiswele, Scandinavia, Abood, Matema Beach, Air Msae na Royal Sumayi.
Nikukumbushe
1,VOLVO
2.SCANIA
3.NISSAN UD
4.DAF
5.YUTONG
6.IVECO.
Wadau wanaosema yutong,waambie waende Moshi Arusha,Mnyama Ngorika,Dar exp
Mwanza miaka nenda rudi Alikuwa Scania Super Najmunisa,Yutong good but shortly,kama Big G vile hizi yutong,scania utatumia hata miaka 10 na zaidi,
wadau wa yutong Mchina wameshasikia SCANIA MODELS HIZI?
SCANIA 91
SCANIA 92
SCANIA 93
SCANIA 94
SCANIA 111
SCANIA 112
SCANIA 113
SCANIA 114
SCANIA 124
SCANIA 524 Hii bado haijafika Bongo bado,kila design hapo ina maana yake ktk mbio,ubebaji wa mizigo,wepesi,uimara nk
Utaipenda kwenye milima,kama ina shuka vile,ikiwa na gia 16.
naunga mkono hoja scania ni imara kwa kila kitu watu mnaangalia kukimbia mna maana gani na barabara zetu za makufuli speed inayotakiwa ni ya kawaida kwa barabara zetu speed inayotakiwa isizidi 120 kutokana na barabara zetu ila utakuta basi lipo 140 to 160 hii ni hatari kwa abiria halafu mnasifia kuwa inakimbia kumbe mnajitafutia vifo, asilimia kubwa ya ajali za barabarani hasa mabasi utasikia speed wakati inakimbia abiria wanafurahia saaana na wakiwapita wenzao ndio vifua vinawajaa kwa furaha huku mkijisemea mchina noma, hayo magari ya kichina baada ya miaka mitano mtaniambia yatakavyochakaa angalia hizo scania zina muda gani na zikoje. yale yale tuliokuwa tunasema vya bei rahisi vinagharama yake sana ila watu hawajui hilo.
Scania zinakuwa nzito sana hasa kwenye kupandisha milima/milimani....lakini kwenye flat road...dah usipime!! Yutong ni laini mno na zinapepea kama karatasi, it is good by then!!
wadau kuna kaubishi kapo hapa kijiweni kwetu kuhusu efficiency ya haya magari especially mabasi. Ubishi ume-base sana kwenye
1) speed ya mabasi, wengi wanaSema yutong ni funiko kuliko scania na ud.
2) ubovu- wamerate kuwa ubovu mchina anaongoza na relate kipindi yalipoingia Yalilaza watu njian nikiwemo na mimi. Ud wanatolea mfano sumry anavoPotea kwenye ushindan.
3)oil consumption. Mchina consumption yake iko chini kuliko wote. je ni kweli
NaOmba wadau na wajuzi wanisaisidie kwasabab nahitaJi kujua ubora wa haya Magar na hata wadau
wengine ambao wanaweza kutaKa kuinvest kwenye c
biashaRa ya magari itawasaidia
Mkuu ni kweli ulichosema ila naomba nikurekebishe kidogo twende sawa... mosi katika scania namba ya mwisho huwa ni toleo ie series , namba zinazofatia ni ujazo wa engine in litres (cc) kwa maana hiyo 94 ni engine ya cc9000 (9litres ) toleo la nne, katika series one kulikuwa na option ya engine tau tu 81 ,111na 141 (v8) seies two kulikuwa na option nne 82 ,92 112, na142(v8) , series three zlikuwa option tatu 93 ,113 na 143(v8) series four kulikuwa na engine option tano 94 ,114, 124 ,144(v8),164(v8). Baada ya series four waliamua kubadilisha naming format kulingana na cabin types na uwezo wa engine (hp) that is P ,R, G,& T series kwa maana hiyo hakuna R524 bali ipo R500, R580 n.k hope nimesaidia..
kulinganisha Scania na Yutmg ni kuchekesha walionuna.
Matajiri wengi walionunua Yutonga wanajuta ni gari ambayo haiwezi kaa barabarani zaidi ya 2yrs , wanachofanya wanunua Yutong na wanaweka engine za Scania.
Na uimara wa body ya U tong haifikii hata nusu yd uimara wa body ya marcopolo ambazo zinatumika kwenye magari ya Scania.
Matajiri walimbilia kwenye U tong sababu ya bei .
hiyo kuna uzi wake kue hoja na habari mchanganyikoHapo vip?View attachment 166846