Isanga family kitu unachoshindwa kutofautisha ni kimoja, kwa upande wangu nimesifia mabasi ya wachina kwa sababu wanaelewa mahitaji ya soko. Ukiongelea uimara na ubora, Scania, Volvo, Benz, Leyland and the likes ndio magwiji, tatizo linakuja pale ambapo bei yao iko juu sana kulinganisha na mchina.
Sasa hata kama Scania inadumu, lakini itakua imechakaa, hauwezi kulinganisha na Mchina mpya hata kama hatadumu sana lakini abiria ndio wanachokihitaji, anasa. Mchina kwa anasa hajambo mkuu. Hizo picha za mabasi ulizoziweka umeshawahi kuziona hapa bongo? Unafikiri ni kwanini? Biashara inahitaji kusoma upepo wa mwenendo wa soko unavyoenda. Unaweza kuwa na bidhaa bora kuliko washindani wako wowote, lakini kama hakuna soko na watu wanakimbilia mbadala lazima ubadili formation ya mchezo kutokana na mchezo unavyoenda.