Yutong/zongtong/Higer and scania buses

mswiden ni noma, ukiangalia tanzania kampun nyingi zilizo anza na mabasi ya kichina kwa sasa zinahali mbaya(sitaki kuzitaja) ila kampuni zinazotumia scania zinafanya vizur. mfano hood abood, kilimajaro, dar ex. hapana chezea scania
 
Mkuu mi naona hujasafiri kwa muda mrefu kaangalie sasa hivi gari za kichina zinaenda mbeya_Arusha bila kuwa na tatizo lolote na dar_Mwanza ambazo ni zaidi ya 1000km na upande wa scania hujasema ni scania series gani maana hapa bongo scania zimetokana na malori yaani malori yamegeuzwa kuwa mabasi kwanzia scania93, 94D,113,114 na p230 ni gari chache sana zenye chassis na injini halisi ya basi yaani scania F series chassis na vile vile hujaongelea uwezo wa gari amabazo zimekuja badala ya Nissan diesel ambazo ni MAN HB3 na MAN HB4 ambazo zinatembea zaidi ya km 2000 kwenda congo na kampala via kagera
 
hizi ni body tu za marcopolo unaweza kufunga injini kati ya scania,benz,Man na Volvo sasa hapo hatujui mwenzetu umejuaje kama scania imefungwa hapo
 
Mkuu kwani wewe hukusoma methali "Bure aghali"?
Usiwe kama profesa anayelilia uenyekiti aliojiuzulu kwa hiyari yake!!!?
 
hizi ni body tu za marcopolo unaweza kufunga injini kati ya scania,benz,Man na Volvo sasa hapo hatujui mwenzetu umejuaje kama scania imefungwa hapo
Mimi mtoa uzi huu nina experience. Scania zipo safari ndefu. Moshi-Mwanza. Muulize Isamilo mwenge zongtong na Yutong. Anapata shda gan kwa Mghamba na Kibo. Route ya Dar - Mwanza waulize kina Dar lux wenye Yutong wanapata shda gan kwa Kisbo ambzo ni Scania. Scania zina nguvu ase. Kampuni nyingi zinadumu na Scania. Kwa mfano Mghamba. Alianza na Scania flan hivi ameiita "Missisipi" na nyngne ameiita "Suez canal" zipo till now na bdo zinatembea kwenye road.
 
mgamba na kibo zina chassis na injini za mabasi scania fseries au nayo ni malori yaliyojengewa body za mabasi??
 
Kwan engine c Scania?
tofautisha injini ya scania maalum kwa ajiri ya basi na injini maalum kwa ajili ya lori ikafungungwa kwenye basi unafikiri itakuwa imevuta mzigo hapo hood zenyewe zile za arusha mbeya saizi zimefungwa injini za malori
 
hizi ni body tu za marcopolo unaweza kufunga injini kati ya scania,benz,Man na Volvo sasa hapo hatujui mwenzetu umejuaje kama scania imefungwa hapo
Zipo kerk/Nugget Street Johannesburg huyo Mtanzania mwenye hizo kaweka Engine za Scania ni wachache wanaoweka mercedes...
 
tofautisha injini ya scania maalum kwa ajiri ya basi na injini maalum kwa ajili ya lori ikafungungwa kwenye basi unafikiri itakuwa imevuta mzigo hapo hood zenyewe zile za arusha mbeya saizi zimefungwa injini za malori
Kaka hilo sio tatizo kwani bado ni scania iwe fseries, streamliner, bado ni scania. Kwanini gari za kichina hawafungi injini za malori ya kichina na badala yake basi nyingi za mchina wabongo wameweka dif na gear box ya scania na wengine injini, gear box na dif zote scania.

Hata ukija kwenye malori ya kichina shida ni zile zile mwaka mmoja tu pump kwisha kazi injini inachanganya oil na maji kwasababu vikombe kwenye block vinabanduka kama viumeungwa na bablishi. Kuua piston ni jambo la kawaida ndio maana hakuna guarantee ukinunua. Unaambiwa nunua gari tano tunakupa na moja ya ziada. Sasa fikiria mtengenezaji wa scania au benz actros anakupa guarantee ya 10yrs. Hii inamaanisha ana uhakika na ubora wa kitu anachokupa.

Angalia basi ambazo zina engine za malori yale malori yameendeashwa zaidi ya miaka kumi hadi kumi na tano ulaya na bado ukileta hapa ukavisha bodi ya lori au basi bado unasumbua njiani kwa kipindi kingine cha miaka kumi au zaidi.
 
kaka acha kupotosha uma injini ya scania maalum kwa ajili ya basi na injini ya scania kwa ajili ya lori ni tofauti katika utendaji wa kazi ukifunga injini ya lori kwenye basi inakuwa haina mzigo wowote na inakuwa na nguvu zaidi
 
na hizo gari za kichina ambazo unasema zimewekewa vitu vya scania ni zile yutong toleo la kwanza f11 fatilia yutong toleo la pili f12 kama kuna hata moja iliyowekewa kitu chochote cha scania
 
nenda marcopolo south africa kajionee mwenyewe
ambacho hujaelewa nimesema Wamiliki wengi wa mabasi wanapendelea kuweka Engine za Scania hasa kwa wageni Wazambia,WaTz,Watswana na wengineo wao SA wanatumia Man na Mercedes Benz hata Volvo engine huko ndio tunakoshinda na kazi ndio hizo hizo za mitambo na engine kubwa kutoka Gauteng Province..
 
mkuu hapa tunazungumzia injini na sio bodi usifananishe scania na hayo magari ya kichina
ndio maana nimeuliza maana najua mghamba kafunga injini za
113 na kibo ni 94D hapo hakuna basi ni malori kaangalie zhongtong zinavyopelekana na scania f95-310 route ya dar_Tunduma au Mbeya _Arusha
 
habari ya mjini sio yutong..kwasasa ni zhongtong na higer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…