Z-Anto adai yupo tayari kurudi Tip Top lakini siyo WCB

Z-Anto adai yupo tayari kurudi Tip Top lakini siyo WCB

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,076
Reaction score
17,247
Z-Anto ni miongoni wa wasanii waliozishika chat za radio na TV mbalimbali za Tanzania miaka kadhaa iliyopita, na waliozunguka karibia kila mkoa kama sio kila wilaya kupiga show kutokana na kuhit sana kwa wakati huo.

Tetesi za Z-Anto kuwa atasaini Wcb zilienea na hatimaye amefunguka kuwa kulikuwa na mazungumzo kati yake na Wcb lakini binafsi yake asingependa kufanya kazi na lebo hiyo kwasababu anaamini mafahali wawili hawakai zizi moja. Amesema pengine ingefaa akirudi Tip top connection alipoondoka zamani lakini siyo kufanya kazi Wcb. Z-Anto akiongea kwenye Planet bongo ya EA Radio kuwa tayari kuna Lebo 5 kubwa Tanzania zinamtaka na moja wapo itamsaini hivi karibuni.

Amesema atarudi soon kwenye game na amewataja Ali kiba na Dully sykes kama wasanii anaoona watampa changamoto kutokana na uwezo wao mkubwa wa sauti, melody na utunzi.

MAONI YANGU
Inawezekana Z.Anto Ni Mmoja kati ya wale Watanzania Wanne...
 
Mafahari wawili hawakai zizi moja kivipi?...kwani huko Tip Top connection hakuna mafahari?...cha msingi atumie muda huu kufanya maamuzi sahihi.
 
Mafahari wawili hawakai zizi moja kivipi?...kwani huko Tip Top connection hakuna mafahari?...cha msingi atumie muda huu kufanya maamuzi sahihi.
Hana lolote, Anajikweza tu,
 
sijaelewa hapo kwenye mafahari wawili anamaanisha nini?
 
Z anto huyu huyu au mwingine? Ufahari huo kautolea wapi labda mpaka aseme hawakai zizi moja labda sijamwelewa.
 
Hahaha unadhani bila kusema hayo atapata wapi kick za kurudi kwenye game?
 
Z-anto ni msanii mzuri sana na kazi zake ni nzuri kama mpenzi jini, binti kiziwi na kisiwa cha malavidavi..aongeze juhudi, nidhamu na ubunifu ili aweze kufika mbali zaidi katika mziki na mafanikio kimataifa
 
Hehehe!
Et mafahari wawili! Na sauti ile labda apambane na ally k

Bangi sio za mchezo mchezo walah!

Sema STUNTER apo ulipobold z-anto akiiona i post atakushtaki [emoji28][emoji28]
Hahaha kwanza uliona wapi swala akalisogelea kundi la simba hhahaa...
 
dah yaan huyu anataka apate kiki,yeye mwenyewe anajua hawezi kuwa WCB
microphone.png
musical_keyboard.png
guitar.png
 
Back
Top Bottom