Z-Anto adai yupo tayari kurudi Tip Top lakini siyo WCB

Z-Anto ni miongoni wa wasanii waliozishika chat za radio na TV mbalimbali za Tanzania miaka kadhaa iliyopita, na waliozunguka karibia kila mkoa kama sio kila wilaya kupiga show kutokana na kuhit sana kwa wakati huo.

Tetesi za Z-Anto kuwa atasaini Wcb zilienea na hatimaye amefunguka kuwa kulikuwa na mazungumzo kati yake na Wcb lakini binafsi yake asingependa kufanya kazi na lebo hiyo kwasababu anaamini mafahali wawili hawakai zizi moja. Amesema pengine ingefaa akirudi Tip top connection alipoondoka zamani lakini siyo kufanya kazi Wcb. Z-Anto akiongea kwenye Planet bongo ya EA Radio kuwa tayari kuna Lebo 5 kubwa Tanzania zinamtaka na moja wapo itamsaini hivi karibuni.

Amesema atarudi soon kwenye game na amewataja Ali kiba na Dully sykes kama wasanii anaoona watampa changamoto kutokana na uwezo wao mkubwa wa sauti, melody na utunzi.

MAONI YANGU
Inawezekana Z.Anto Ni Mmoja kati ya wale Watanzania Wanne...
Hahahahah hebu nicheke mimi kwanzs kabla ya kuchangia kitu
 
Huyu dogo ana ufahari gani kwa sasa kafeli kabla hajarudi kwenye game ajue kuwa gemu limebadilika sauti anazowasifia hao znamchango mdogo sana kwenye mziki wa sasa kama kajifua sauti tu kapotea xana
 
Z-Anto ni miongoni wa wasanii waliozishika chat za radio na TV mbalimbali za Tanzania miaka kadhaa iliyopita, na waliozunguka karibia kila mkoa kama sio kila wilaya kupiga show kutokana na kuhit sana kwa wakati huo.

Tetesi za Z-Anto kuwa atasaini Wcb zilienea na hatimaye amefunguka kuwa kulikuwa na mazungumzo kati yake na Wcb lakini binafsi yake asingependa kufanya kazi na lebo hiyo kwasababu anaamini mafahali wawili hawakai zizi moja. Amesema pengine ingefaa akirudi Tip top connection alipoondoka zamani lakini siyo kufanya kazi Wcb. Z-Anto akiongea kwenye Planet bongo ya EA Radio kuwa tayari kuna Lebo 5 kubwa Tanzania zinamtaka na moja wapo itamsaini hivi karibuni.

Amesema atarudi soon kwenye game na amewataja Ali kiba na Dully sykes kama wasanii anaoona watampa changamoto kutokana na uwezo wao mkubwa wa sauti, melody na utunzi.

MAONI YANGU
Inawezekana Z.Anto Ni Mmoja kati ya wale Watanzania Wanne...

Kweli dunia ina mambo.
 
sijaelewa hapo kwenye mafahari wawili anamaanisha nini?
Usikute kamaanisha yeye na Chibu.

Ila yule bwana alivyo mstaarabu itakuwa tu kachanganya kati ya Ng'ombe na Mbuzi...ilitakiwa tu anayemsikiliza amsahihishe kuwa kwa Mbuzi haitumiki Fahari ni Beberu....kwa hiyo kwa kufupisha stori ni kwamba alimaanisha kuwa Beberu haingii Zizi la Fahari.
 
Ameanza lini comedy....maana hii hata Kingwendu akisoma lazima achanike mbavu.
 
Back
Top Bottom