Za kuambiwa, tuchanganye na zetu

Za kuambiwa, tuchanganye na zetu

Aramun

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
461
Reaction score
2,213
Ahabu - mke 1

Herode - mke 1

Anania - mke 1

Pontio Pilato - mke 1

Yeroboamu - mke 1

Nebukadreza. - mke 1

Hamani - mke 1​

Na wote walipotea njia na kumsaliti Mungu.

1. Ibrahimu - wake 2

2. Yakobo - wake 4

3. Daudi - wake 4

4. Sulemani - wake 700

5. Rehoboamu - wake 18

6. Abiya - wake 14

7. Elikana - wake 2

8. Lameki - wake 2​

Na wote wakapata kibali machoni pa Bwana.

Lakini wachungaji wanatuambia kuwa kuoa wake wawili ni dhambi kwa Mungu.

Something somewhere is not right.
 
Ahabu - mke 1

Herode - mke 1

Anania - mke 1

Pontio Pilato - mke 1

Yeroboamu - mke 1

Nebukadreza. - mke 1

Hamani - mke 1​

Na wote walipotea njia na kumsaliti Mungu.

1. Ibrahimu - wake 2

2. Yakobo - wake 4

3. Daudi - wake 4

4. Sulemani - wake 700

5. Rehoboamu - wake 18

6. Abiya - wake 14

7. Elikana - wake 2

8. Lameki - wake 2​

Na wote wakapata kibali machoni pa Bwana.

Lakini wachungaji wanatuambia kuwa kuoa wake wawili ni dhambi kwa Mungu.

Something somewhere is not right.
Kuoa wake wengi sio dhambi ndiyo maana maandiko yasema tuijie kweli nayo kweli itatuweka huru....tatizo viongozi wa dini wanatukaririsha walivyodanganywa wao bila kuyachunguza maandiko ... ndiyo maana ukristo unakuwa ni kama kitanzi kwa wenye wake wengi ....ni kama kuna mkono wa shetani ili tusiijaze dunia kama agizo la Mungu
 
Paulo alitoa amri kuwa "Askofu awe mme wa mke mmoja"
1Timotheo 3:2-12
Sasa viongozi wanatumia sababu hii kupinga ndoa za wake wengi utafikiri sisi wote ni Maaskofu.
 
Ibrahimu - wake 2

2. Yakobo - wake 4

3. Daudi - wake 4

4. Sulemani - wake 700

5. Rehoboamu - wake 18

6. Abiya - wake 14

7. Elikana - wake 2

8. Lameki - wake 2​
Na wote wakapata kibali machoni pa Bwana.
Hawa wote walibarikiwa/walipata kibali machoni pa Mungu kabla ata hawajaoa na Kuna walioangusha na hizo ndoa zao wakapoteza hicho kibali na kurudi kwa Mungu tena kutubu Ili wapate kibali tena

Somo hapo ni kwamba tafta kibali/rehema za Mungu kwanza wanaweke/ndao inaweza kukupoteze machoni pa Mungu ukiwaendekeza.
 
Weka hapa aya inayosema ndoa lazima iwe ya mke mmoja.
1 Wakorintho 7:2
[2]Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Nevertheless, to avoid fornication, let every man have his own wife, and let every woman have her own husband.
 
Uadilifu kwanza kwa hao wake , kama sio muadilifu kukidhi haja zao basi fanya kuoa mmoja .
 
Viongozi wa dini hawataki uwatese wanawake, maana wanajua kipato chako cha papatu papatu...
Ukiwa na wake wawil...wote uwatendee sawa utaweza?
 
1 Wakorintho 7:2
[2]Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.

Nevertheless, to avoid fornication, let every man have his own wife, and let every woman have her own husband.
Hii sio amri ya Mungu bali ni ushauri wa mtume Paulo.Mtu anahukumiwa kwa kuvunja amri za Mungu na sio kwa kutofuata ushauri wa mitume na manabii.
Kwenye 1Wakorintho 7:1 mtume Paulo anashauri ni bora watu wasioe au kuolewa, lakini leo wakristo wanaoa na kuolewa kwasababu wanajua kilichoandikwa kwenye hiyo aya sio amri ya Mungu bali ni ushauri wa Paulo.
Hakuna sehemu yoyote kwenye Bible ampapo Mungu amekataza ndoa ya wake wengi.
 
Back
Top Bottom