Za ndani: Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya haziko tayari Ukraine kujiunga na NATO

Za ndani: Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya haziko tayari Ukraine kujiunga na NATO

SaintErick

Member
Joined
Aug 7, 2013
Posts
90
Reaction score
53
Naam, unaweza kudhani ni mzaha lakini ndivyo ilivyo.

Mwaka huu viongozi wengi wa ngazi za juu kutoka Ulaya na Wanadiplomasia mbalimbali wamekua wakipishana huko District of Columbia (Washington), Arlington-Virginia na New York wakipishana milango ya White House, Makao maku ya Republicans, Democratic, Wizara ya Ulinzi na mabilionea wakubwa.

Vita vya Ukraine imekua agenda kubwa ya kwanza, mpango wa Ukraine kujiunga na NATO pamoja na uchaguzi mkuu wa Marekani.

Viongozi wote wanatafuta kuafikiana juu ya maswala tata zaidi kama vile kujitoa kuisadia Ukraine silaha na kuisadia kua mwanachama wa NATO.

Ila katika vikao vya siri ambavyo The Politico walipata nafasi ya kuongea kwa siri na wanadiplomasia zaidi ya 50 mtazamo wao juu ya Ukraine kua mwanachama wa NATO bado ni ndoto tofauti na imani ya wengi. Hii inakunzana na msimamo wa watu mashuhuri akiwepo katibu mkuu wa NATO: Mark Rutte ambaye anaamini atahakikisha Ukraine inajiunga na NATO.


Hata katika mahojiano na Aljezeera alyewahi kua Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Owen anasema sio swala la Ukraine kujiunga au kutokujiunga na NATO bali swali ni lini?! Finland na Sweden ambao ni wanachama wapya wa NATO bado wanaamini Ukraine anaweza kufanya ambavyo wao wamefanya lakini je ni kweli?

The Political wanaarifu kua Marekani bado haiamini angalau kwa sasa kwamba Ukraine inapaswa kua sehemu ya NATO kwa hivi ilivyo (wanaamini labda mipaka isiwe hii) ili kutoileta NATO katika vita vya moja kwa moja na Urusi, angalau kwa sasa.

Licha ya kwamba wanajinasibu kuiunga mkono Ukraine hadharani lakini ndani ya majengo ya Washington, Virginia na New York wanateta tofauti. Wazo hili la Marekani linaungwa mkono na mataifa takribani saba ya Ulaya kama vile; German, Hungary, Belgium, Slovenia na Spain.

Hata hivyo, licha ya kwamba nchi nyingi kwa sasa hazipingi waziwazi ila NATO ikianza mchakato rasmi wa kuipa Uanachama Ukraine, basi tegemea sauti nyingi kutoka Ulaya zikipinga Ukraine kuingia NATO.
 
FB_IMG_17297557789810403.jpg
 
Back
Top Bottom