Za ndani....Simba kupewa points 3 mechi ya Namungo.

Tuanze ligi upya kwa mechi 7 zilizobaki kwa kuwapa Simba point 8 ili tulingane kabisa

Au sare tulizopata na kupoteza point mbili kwa kila sare, basi zile point wapewe simba kabisa
 
Hili halipo labda tu iwapo Namungo walijulishwa na TFF lakini wao wakamchezesha huyo mchezaji kwa makusudi. Toka sakata la mchezaji wa Kagera Sugar (nimemsahau jina) na Simba miaka michache iliyopita jukumu la kuzijulisha timu kabla ya mechi kuhusu wachezaji wao wenye kadi wasioruhisiwa kucheza mechi husika lilibaki kwa TFF na si kwa timu husika.
 
hakuna kanuni ya kipuuzi kama hiyo kwenye ligi yoyote duniani. Kama kweli Kichuya alikuwa na kadi 3 za njano lazima klabu iwajibishwe.
 
Kwa ninavyoelewa sheria za sasa hazibadilishi matokeo ya ndani ya uwanja zaidi adhabu zitahusu wahusika moja kwa moja kwa muktadha huu yaani timu au mchezaji husika au wote kwa pamoja.
 
Jangwani kuna waka moto na mechi ijayo na dodoma yanga wakifungwa au kutoa sare basi jangwani hali itakuwa sio shwari maana mayele na feisal wanasema walihujumu yanga last mechi sisi yetu macho tu msimbazi tunawaangalia tu mnavyohangaika.
 
Hakun ukuda huo wa pont za mezani siku hizi,Kolo pambaneni uwanjani kutafuta nafasi ya pili
 
nimejaribu kupitia nyuzi za humu ila nikagundua kua nyuzi kwa kiingereza ni thread, ila sa itakuwaje

au tumuulize msukule mkuu atupe majibu ya kuridhisha[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Dodoma Jiji Lazima Waifunge Yanga Ndiyo Hapo Watajielewa
 
Za ndani zinasema Simba kupewa points 3 kutoka mechi yao waliyocheza na Namungo na kutoa draw. Kuna mchezaji alikuwa hajamaliza adhabu ya card alichezeshwa na Namungo

Sasa hivi ni upepo unasomwa tu unavyoenda kutoa tamko rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…