Zee la madawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,895
- 4,478
Kitengo cha Biashara cha Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam, kimetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na kampuni ya ZH Poppe Limited pamoja na wasimamizi wa mali za Marehemu Mfanyabiashara Zacharia Hans Poppe waliokuwa wakitaka kuizuia Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kuuza kwa mnada mali zilizowekwa dhamana kwa Mkopo unaozidi Shilingi Bilioni 7.4.
Uamuzi huo ulitolewa Jumatatu, Juni 15, 2026, na Jaji Arnold Kirekiano, ambaye aliruhusu TCB kuendelea na hatua za kurejesha deni baada ya kubaini kuwa waombaji hawakufikia vigezo vinavyohitajika kisheria ili kupewa zuio la muda.
Mgogoro huo unatokana na mkopo uliotolewa na TCB kwa ZH Poppe Limited, ambapo benki ilidai kuwa mkopo huo haukulipwa kwa mujibu wa makubaliano, jambo lililoisukuma kuanza mchakato wa kuuza dhamana mbalimbali ikiwemo malori, magari ya kusafirisha Mafuta na Trela.
Waombaji walidai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika uhamishaji wa hisa za Kampuni na waliomba kusitishwa kwa hatua za utekelezaji wa dhamana hadi shauri la msingi litakaposikilizwa.
Hata hivyo, Mahakama iliamua kuwa madai hayo hayakuthibitishwa na kwamba kwa kiasi kikubwa yalihusu masuala ya ndani ya Kampuni ambayo hayakuwa na msingi wa kuzuia benki kutekeleza haki zake za kisheria za kurejesha deni.