Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

Kwa huu ujinga huu ugonjwa utakaa muda mrefu sana hapa kwetu
 
Hapa ndipo umuhimu wa wapinzani unapoonekana kwani ni wazi hili jambo wangeliaongelea Bungeni bila kuogopa/kumuogoa Bwana Yule.
 
Kimsingi kuna taharuki miongoni mwa raia! Cha kushangaza Serikali imeamua kukaza shingo.

Siyo dhambi kutangaziwa rasmi uwepo wa tatizo, na pia hatua mahsusi kuchukuliwa! Zikiwemo za kuongeza hivyo vifaa vya upumuaji kwenye mahospitali yetu! Kutenga maeneo rasmi ya kuhudumia wagonjwa wa aina hiyo kwa ukaribi na kwa haraka kama ilivyokuwa mwaka jana kabla ya serikali kuweka mpira kwapani, nk.

Sijasema kuwepo na lockdown!! Maana wale wenzangu wenye miguu ya kuku wanaweza kunivamia na kunishambulia kama mwewe vile.
 
Naona wabunge wameanza kupata akili sasa.
... tatizo wanazipata wakiwa wamechelewa sana! Tungezingatia taratibu sahihi kwa wakati za kupambana na hili janga tungeokoa roho ngapi? Hadi majenerali, maprofesa na viongozi wa dini waanze kuteketea ndio wanashtuka? Sisi makapuku hakuna mwenye habari na sisi! Ajabu sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…