Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 17,499
- 25,295
Wakuu kwema
Jana nilipata changamoto ya kiafya ikabidi niende pale zahanati ya halmashauri mwenge karibu ba uwanja wa KMC ni Mwenge, nilikutana na mambo ya kushangaza sana, na huu ni wizi wa mchana kweupe kabisaa.
Yaani hakuna namna wale watumishi pale ni wezi kabisa, nilifika pale nikaelekezwa kulipa registration fee shiling 1000 nikalipa no RISITI nikasema sawa baadae nikaambiwa nikamuone docta na maabala nikaambiwa nilipe 18000/= nikalipa cash no RISITI Yaani mnapeana pesa kama pesa binafsi
Baadae nikaenda FAMASI pia nikakuta NO RISITI
Baadae nikauliza kuhusu ripoti nikaambiwa hakuna nikashangaa SANA, Kwamba yaani inawezekanaje serikali ishindwe kabisa kutoa risiti jamani
Ujumbe wangu kwa manispaa
1. Risiti ni muhimu kama kielelezo cha kupatiwa huduma stahiki. watoa huduma siyo MALAIKA, ivi yule kijana niliyemkuta anachezea simu pale MAPOKEZI ni muaminifu kiasi gani kwamba anaweza kukusanya 1000 kwa kila mgonjwa kwa masaa 8 na azifikishe zote salama kwa mwajiri wake? DED jiulize wewe ungeweza?
Swali hili pia waulizwe watu wa phamacy na maabala HAPO HOPSITAL kwanini hawatoi risiti? kumbe serikali haimanishi inaposema UKINUNUA DAI RISITI?
CONTROL NUMBER: Kwanini hazitumiki shida ipo wapi? utajuaje kwamba nani kalipa na nani hajalipa? ivi unampaje mtu huduma bila hata risit ya mkono jamani?
Serikali hasa ya manispaa ya kinondoni ijitathmini huu ni wizi na rushwa kubwa kabisa. Unahubiri watu walipe kodi bila risiti?