JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Paul Chacha ameupa siku tatu uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupitia idara ya afya kuhakikisha inafunga vitanda vya akinamama wajawazito kwenye Zahanati ya Kijiji cha Usangi ambayo wajawazito wamekuwa wakilazwa sakafuni kabla na baada ya kujifungua.
Akiwa ameambatana na kamati ya usalama, mkuu huyo wa wilaya ameshuhudia mama wajawazito katika Zahanati hiyo wakiwa wameketi sakafuni wakisubiri kupatiwa huduma za matibabu, huku vitanda vikiwa bado vimehifadhiwa stoo kwa zaidi ya miezi mitatu pasipokuwa na sababu za msingi.
Mkuu huyo wa wilaya pia ameshuhudia dawa zikiwa zimehifadhiwa chini, jambo lililomsukuma kutoa fedha yake ili kushughulikia baadhi ya vifaa muhimu.
Source: Azam TV