Zahanati yahifadhi vitanda stoo, wajawazito wakijifungulia sakafuni

Zahanati yahifadhi vitanda stoo, wajawazito wakijifungulia sakafuni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
286895914_417787150216909_2179256002463363063_n.jpg


Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Paul Chacha ameupa siku tatu uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupitia idara ya afya kuhakikisha inafunga vitanda vya akinamama wajawazito kwenye Zahanati ya Kijiji cha Usangi ambayo wajawazito wamekuwa wakilazwa sakafuni kabla na baada ya kujifungua.

Akiwa ameambatana na kamati ya usalama, mkuu huyo wa wilaya ameshuhudia mama wajawazito katika Zahanati hiyo wakiwa wameketi sakafuni wakisubiri kupatiwa huduma za matibabu, huku vitanda vikiwa bado vimehifadhiwa stoo kwa zaidi ya miezi mitatu pasipokuwa na sababu za msingi.

Mkuu huyo wa wilaya pia ameshuhudia dawa zikiwa zimehifadhiwa chini, jambo lililomsukuma kutoa fedha yake ili kushughulikia baadhi ya vifaa muhimu.

286728154_773745220658857_1661735075339499029_n.jpg


Source: Azam TV
 
Kaliua maduka ya madawa ni kitu nyeti kuliko ujuavyo kikubwa uwe mtunza Siri zawateja wako wanacholopoa mimba aibu magonjwa mbalimbali na inaonesha hao madaktari Kijiji hicho wanamaduka ya madawa akati MSD wanasheria inakataza waziwazi wahudumu wa afya maeneo husika kutokua au kuazisha biashara zamaduka ya dawa baridi...... Tabu tupu
 
Back
Top Bottom