Zahanati yakosa Maji,Mbunge apokewa kwa Ndoo tupu

Zahanati yakosa Maji,Mbunge apokewa kwa Ndoo tupu

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Wananchi wa Kata ya Naalarami, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wanaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji, hali inayoathiri shughuli zao za kila siku pamoja na utoaji wa huduma muhimu za kijamii.

Wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Monduli, Isack Joseph, wananchi walimlaki wakiwa na ndoo tupu kuashiria ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa maji katika eneo hilo.


Soma zaidi:Wananchi walalamikia mradi wa Maji wa Shilingi bilioni 2.5 kutoleta manufaa Losikito,Arusha

Uhaba huo wa maji umeathiri pia sekta ya afya, ambapo zahanati inayohudumia wakazi wa eneo hilo imelazimika kusitisha baadhi ya huduma kutokana na ukosefu wa maji.


Akizungumza na wananchi, Mbunge Isack Joseph aliahidi kuwa Kata ya Naalarami itaunganishwa kwenye mradi wa maji wa vijiji 13 na kusisitiza kuwa atafuatilia utekelezaji wa mradi huo hadi utakapokamilika.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, mabomba ya mradi wa maji wenye thamani ya Shilingi bilioni 21 yanatarajiwa kuanza kupokelewa Julai 27 katika chanzo cha maji cha Ngaramtoni, Wilaya ya Arumeru.

Hatua hiyo inatarajiwa kuharakisha utekelezaji wa mradi huo na kusaidia kutatua tatizo la uhaba wa maji kwa wananchi wa Naalarami na maeneo jirani.
 
Back
Top Bottom