Zahera aitwa TAKUKURU

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
7,359
Reaction score
5,837
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), imewataka wadau wote wa michezo akiwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuwasilisha malalamiko yao licha ya taasisi hiyo kuwatuma maofisa wake kufuatilia yanayoendelea kwenye Ligi Kuu Bara.

Takukuru wametoa kauli hiyo kufuatia hivi sasa wadau wengi wa soka kulalamika juu ya uwepo wa rushwa michezoni katika kuzihujumu timu kwenye mechi za mwisho za Ligi Kuu Bara. Zahera mara kwa mara amekuwa akilalamika juu ya baadhi ya timu kutumia vibaya fedha zao katika kuzihujumu timu nyingine.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema kuwa kwa upande wao tayari vijana wao wapo kazini kufuatilia kila kitu kinachotokea katika ligi kuu kupitia timu shiriki huku akiwataka wadau akiwemo Zahera kuwapelekea malalamiko yao ili waweze kuyafanyia kazi.

“Ni kweli hizo taarifa zimetufikia lakini kitu kinachotusikitisha sana kutoka kwa wananchi (wadau) ni kwamba mambo yanaongelewa na watu lakini wahusika wanaoguswa na hayo mambo hawaji kutupa taarifa kwa ufasaha yaani kutupa kamili, nini kimetokea, nani kafanya nini wakati gani na wapi.

“Sasa tuna taarifa lakini ni za kuungaunga mno, sisi tungependa hao watu wanaolalamika waje watueleze, nani kachukua rushwa, wakati gani na wapi, sisi tunaingia kazini yaani tupo tayari, tumepata habari nusunusu vijana wetu wemekwenda kufanya uchunguzi lakini inakuwa vyema kama tunapata taarifa ambazo zimejitosheleza kwa sababu inatusaidia kuanza na tatizo kuliko kusubiria,” alisema Mbungo.
 
Hata mie huwa nachukizwa sana na hawa wanaotoa shutuma hizi za rushwa lkn Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa! Yanga Simba na Azam ni timu kubwa zenye kucheza vizuri pia! lkn naamini bado kuna watu HAWATAKI kukubali hili! Wao wakishafungwa ili kijikosha kwa wapenzi wao ni kulaumu kwamba hawajafungwa KIHALALI! Mbona wakifungwa na timu nyingine HAWAPIGI kelele? Sasa kama kweli kuna rushwa imetolewa bc vyombo vinavyohusika VIANZE na hao ktk upelelezi ili KUKOMESHA suala la timu kutoa rushwa au kulalamika kuishe maana wanafanana na WACHOCHEZI!
 
Inaelekea umeanza kufuatilia mpira wa tz,unamjua kocha siang'a wa simba aliyehudumu chini ya ufadhili wa mo dewji alisema nini kuhusu kununua/kuuza mechi?!
 
Inaelekea umeanza kufuatilia mpira wa tz,unamjua kocha siang'a wa simba aliyehudumu chini ya ufadhili wa mo dewji alisema nini kuhusu kununua/kuuza mechi?!
Ckumbuki mkuu! Hebu nikumbushe ili na wengine humu wajue tuweze kujadili kwa upana zaidi kwa faida ya soka letu ambalo limejaa matokeo kabla ya tukio!
 
siang'a alisema ugomvi wa yeye na mo ni yeye kukataa kuwauzia mechi zamalek mwaka 2003,pia walikua wakinunua mechi za ligi kuu
Je huo ugomvi wao uliishaje? Maana kusema ni lazima UKUTHIBITISHE! Kumuita mtu mwizi hawezi kuwa mpaka athibitishwe!
 
Zahera kama kocha wa timu kubwa kama Yanga hatakiwi kuwa analipigia kelele hili swala.

Ajulishwe historia ya vilabu vyetu na aambiwe kwamba hata Yanga hili wamewahi kulalamikiwa, na ikisema uchunguzi ufanyike hata hao kina Karia hawatabaki madarakani.
 
Ohoo!
 
sianga alitimuliwa simba akaenda mtibwa
Kwa hiyo alitimuliwa kwa tatizo hilo? Maana Hakuna kocha atakayesema katimuliwa kwa 7bu walizotoa viongozi! Kwani hata simba naamini walitoa 7bu tofauti na alizosema Siang'a! Lkn yote kwa yote kama ilikuwa kweli alipaswa aende kwenye mamlaka husika akatoe taarifa! Eidha polisi, chama cha soka, caf au fifa! Hapo ndio ingekuwa dawa kama ingethibitishwa
Siang'alitimuliwa simba
 
Hizo timu za kkoo huwa ziawauzia waarabu mechi,ndiyo sehemu ya wafadhili kurudisha fedha na kupata faida,yanga ya kondic walipoenda misri,usiku akatoka kocha,kipa na mabeki,kesho wakafungwa goli tatu za vichwa na yule muangola,mwaka flan wakapangwa na timu ya libya,gari la balozi wa libya likaonekana jangwani,nadhani walibya walibishia dau,wakapigiwa mpira mwingi kwao,walivorudiana dar,khami yusuf wa yanga akakosa penat na walibya wakashinda 2-1...khamis yuduf mara nyingi alikua akipata kadi nyekundu arabuni..kutipoti ni kupoteza muda tu
 
siang'a alisema ugomvi wa yeye na mo ni yeye kukataa kuwauzia mechi zamalek mwaka 2003,pia walikua wakinunua mechi za ligi kuu
Yaani mwenzio anataka uthibitisho wewe unaleta maneno yako tena, Lete angalau video ya maneno ya Siang'a.
Shida ya hizi timu mbili simba na Yanga zinapokua hazifanyi vizuri zinatafuta sababu za kutokea na kuanza kusingiziana.
Na kwa sababu hata mashabiki wa timu hizi sio wadadisi ili kujua ukweli wanapokea tu.
Ka Takukuru walivyosema ukiwa na ushahidi peleka takukuru si kua mbeya mbeya kuongea tu maneno unayoyasikia hata kama huna uhakika nayo.
Hapa juzi Zahera kwa sababu ya kupokea tu maneno akadanganywa kua Nadir alikua na Mo ndio mana Yanga imefungwa na Simba. Kwa sababu nae anapokea tu maneno ya umbeya akaenda kumtimua Nadir bila kupata ukweli wa mambo.
Hata marefa hua ni binadamu kuna makosa ambayo wanafanya ka wao sio kwa sababu ya kua wamepewa rushwa au wanamapenzi na timu. Lakini sisi ikitokea refa kafanya makosa ambayo yatawafaidisha timu kubwa hasa simba na Yanga utasikia hi timu imenunua mechi. Lakini sisi wenyeye hata mpira wa wenzetu ambao tunasema tunataka kujifunza tunaona Mara nyingi makosa hafa ya offside au penalty yanajitokeza Mara nyingi lakini hatusikii makocha wa timu kulalamika hata kushtumu kusema timu flani imenunua mechi.
Mfano tu mechi ya Jana Man city vs Burnley beki wa Burnley anacheza kwa mkono mpira uliokua unaenda langoni kwake refa hakuona tukio akaacha. Ingekua bongo sasa ungesikia huyu refa anataka man city isipate matokeo ili liver achukue ubingwa, hapo tungetengeneza na uongo mwingne kwanza huyu refa ni shabiki wa liver.
Tuache kua wapokeaji tu bila kujiuliza ka hizo taarifa zina ukweli au la.
Hapa ningeomba hata TFF lingekua ka FA hakuna kumzungumzia refa kabla na baada ya mchezo ka ambavyo makocha na viongozi wa timu wanafanya.
Nyie simba na Yanga acheni kuwalaghai mashabiki wenu kwa kujificha kwa marefa pindi timu zenu zinapofanya vibaya tafuteni wapi mmekosea kurekebisha.
Pia kulalamika sio kosa, lakini ka una ushahidi lalamika kwenye vyombo vinavyohusika ili hatua zichukuliwe sio kua wambeya.
 
Kama unataka kauli ya siang'a google,na kuhusu rushwa michezoni hilo si geni na si tz tu hata world cup,serie a na la liga,hapa kwetu rejea tukio la osman kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…