Zahera alitudanganya usajili wa Yanga

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika kocha Zahera anajua kujitetea.Baada ya majigambo ya kuifunga Pyramid ya Misri kushindikana,Kocha Zahera katika utetezi wake amesema usajili aliiufanya ulikuwa kwa ajili ya ligi kuu tu.

Najiuliza kama kocha alijua hivyo kwanini Yanga ilipopangwa na CAF kwenye mashindano hakuwafahamisha viongozi juu ya uwezo mdogo wa wachezaji waliosajili kutokuhimili mashindano ya kimataifa badala yake mbwembwe na majigambo ya kufanya vizuri vikitawala.

Ni aibu kwa kocha kutoa utetezi wa aina hivyo na Yanga ikifanya vibaya ligi kuu atatuambia wachezaji hawakusajiliwa kwa ligi kuu.
 
Baadhi ya mashabiki ni ma mbumbumbu kupitiliza sasa alicho ongopa Zahera ni kipi? Timu zilizokua inafahamika zitashiriki michuano ya Caf ni Simba na Azam, Yanga imekuja kushtukizwa ikiwa Hawajui kama watashiriki Champion League.
Walichofanya Yanga ni kutumia uzoefu kushiriki na wamejitahid kwakua uwezo ndipo ulipo ishia. Sasa mleta mada ulikua unataka kocha wa Yanga aseme mechi ijayo Yanga itafungwa!!!
Alicho Sema Zahera Kocha Yeyote duniani Angesema hivyo, Ata watakapo ondoka kesho kwenda Misri bado atasema wanatarajia kushinda kwakua kwenye mpira lolote laweza tokea. Kwani mbumbumbu walitegemea watatolewa apo Uwanja wa Taifa na UD Songo?
Usiwe na akili mbovu kama za Edo Kumwembe, jaribu kutathmini kitu kabla ujaandika au ongea ili uwe na akiba ya lakusema baadae.
 
Anamshangaa Zahera kusema ukweli. Mourihno aliwaambia bodi ya Manchester hana wachezaji wa kubeba taji. Zahera kaongea ukweli mchungu kuna wachezaji Yanga wanadai hadi wamegoma wengine wanacheza basi tu. Usajili ulifanyika bila viwango.

Michuano ya Africa unacheza na timu kubwa zilizojipanga. Sio Mbao. Mashabiki wa Yanga wanajiwekea malengo makubwa bila kuangalia hali halisi ya club.
 
Wewe ndio una akili sio mbovu BALI za kuku ,mbona ulijisifanya mna kikosi kipana? Kama mlishitukizwa kwanini msijitoe mkajifanya vidume yako wapi ndio maana Simba iliwaambia IGA UFE na kweli mkaingia kichwa kichwa
 
Lakini alipokuwa akileta wakongo wake alisema wana uzoefu wa kimataifa mbona hakusema wa ligi kuu, vitu vingine sio vya kutetea
 
Wewe ndio una akili sio mbovu BALI za kuku ,mbona ulijisifanya mna kikosi kipana? Kama mlishitukizwa kwanini msijitoe mkajifanya vidume yako wapi ndio maana Simba iliwaambia IGA UFE na kweli mkaingia kichwa kichwa
Sasa Simba aliyekuja na Kaulimbiu Iga ufe tena akiwa amejiandaa vya kutosha ametolewa round ya kwanza, Akiwa ametumia zaidi ya billion tatu anatolewa na wauza mitumba wa msumbiji UD Songo. Nijambo la aibu na fedheha kwa majigambo mliyokua nayo sasa Iga ufe mmekufa wenyewe saiz mna galagala mchangani.
 
Mwinyi Zahera ni bomu linalosubiria tu kulipuka pale Jangwani. Ana kipaji cha kubwabwaja kuliko kutenda.
 
Yanga wamepewa barua tarh 4june usajili umeisha 31july
 
Simba hawajabidili gia angani kama Zahera eti wachezaji ni wa ligi kuu ,ngoja tubiri Yanga ifungwe na Ndanda sijui Zahera atasema wachezaji waliosajiliwa ni wa Ligi ya daraja la 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…