Zahera asante kwa kuhamasisha michango ya fedha ila Uwanjani umefeli vibaya.

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Toka afike Yanga huyu ni kocha wa visingizio kila kukicha.Tukiacha visingizio vya msimu uliopita,toka msimu huu uanze amekuwa ni kocha wa visingizio viiingi visivyokua na kichwa wala miguu. Alipofungwa na polisi TZ,mechi ya kirafiki alisingizia uwanja, akaenda Arusha akatoka sare na FC Leopard akaulalamikia uongozi kuwa ziara ya Arusha ilikua ni kupoteza mda. Baada ya kufungwa na Ruvu Shooting akailalamikia bodi ya ligi kuwa inaipendelea Simba kwamba kwanini wao walicheza mapema wakati walikua nje ya nchi? Hakuishia hapo akaomba mechi zake na Mbeya city,n Prison ziahirishwe ili kujiandaa na Zesco ili wachezaji wasichoke. Tff ikakubali cha ajabu leo timu imechapwa. Tusubiri kesho sjui ataongea nini.
Zahera anamapungufu mengi sn hasa jinsi anavyoipanga timu. Anakosea sn. Hv kweli unampanga Ali Ali unamwacha nje Juma Abdul kwann? Kushoto Ali Sonzo hawezi kupanda mbele. Timu nzuri inapimwa kwa kufunga magoli sio kulinda. Mbaya zaidi timu inacheza ovyoo ovyo kabsa.
 
kumbe Simba timu mbovu sana maana wababe wao walioshindwa kuwafunga UD SONGO wamefungwa mechi zote nyumbani na ugenini na platinum ya zimbabwe
 

Ukipewa timu utaifikisha wapi wewe?
 
Yanga haina kocha tangu alipoondoka Lwandamina Yanga inacheza mpira usioeleweka ovyoovyo tu msimu uliopita tulikuwa na bahati ya kushinda ila mpira ulikuwa haueleweki tunaocheza mimi nadhani viongozi wafanye mabadiliko ya kocha kabla hatujapata aibu zaidi mbeleni maana kwa mwendo huu sio kabisa
 
Mtoa mada uko sahihi. Hata mimi nilishamgundua Mwinyi Zahera kama siyo kocha mwenye tija kitambo tu tangu alipomkataa Benno Kakolanya kwa kisingizio dhaifu ili tu Mkongomani mwenzake Kindoki apate nafasi ya kuanza kama golikipa namba moja! Lakini mwisho wa siku tuliyaona madudu aliyoyafanya.

Ukija kwa wachezaji, Mwinyi Zahera amekua hana staha na pia hana saikolojia ya kuwajenga wachezaji kama mzazi kama alivyofanya mtangulizi wake George Lwandamina! Amekua ni mtu wa kutoa shutuma hadharani badala ya kukaa nao faragha, amekua ni mbaguzi! Mtu wa majivuno, kubinua tu midomo (Boo) na kujishaua.

Na mfano mzuri ni kwa mchezaji Mwinyi Haji Mngwali aliyelalamikia kubaguliwa kwake na mwalimu na kutomchezeaha bila sababu za msinhi.

Amewaondoa wachezaji wengi ambao kimsingi walikua bado ni wazuri na mwisho ameishia kusajili wachezaji wa kawaida sana! Hata mimi nimeshangazwa na kitendo cha kumuanzisha mchezaji ambaye namuona ni wa kiwango cha chini sana Ali Ali na kumuacha Juma Abdul nje.

Anamuanzisha Deus Kaseke ambaye hakupata muda mwingi wa kucheza, na kumuacha Ngasa nje! Ameanza kufanya mabadiliko dk ya 82 na wakati timu ilikata pumzi tangu dk za 60! Maproo wake wengi aidha wanasugua benchi, ni majeruhi au wanaruka ruka tu uwanjani.

Hakika jamaa ametuingiza tu hasara. Na nitashangaa kama atadumu mpaka mwisho wa msimu. Mwinyi Zahera anastahili kabisa kutimiliwa Yanga. Tutamshukuru sana kwa kuanzisha utaratibu wa kuchangia timu enzi zile shida na za wale wapigaji viongozi wa muda. Kwa sasa atuachie tu timu yetu. Maana hatatufikisha kokote.
 
kumbe Simba timu mbovu sana maana wababe wao walioshindwa kuwafunga UD SONGO wamefungwa mechi zote nyumbani na ugenini na platinum ya zimbabwe
platinum ya Zimbabwe wewe yanga ungeiweza au unaleta tu ushombe shombe wako hapa
 
Ni kocha pekee aliyopo Yanga na vyeo vyote kwa mkopo, tatizo wakimfukuza hawana hela ya kumpata kocha mwingine mzuri
 
Ila aliikuta Yanga vibaya kihela na kwenye hayo magumu na baadhi ya wachezaji kugoma goma ligi kuu akamaliza nafasi ya pili,hiyo hatua aliyofika CAF simba hatujafika mwaka huu,siyo mbaya sana ila nahisi hashauriki anataka yeye awe kila kitu
 
Huyo kocha mchovu acheni kumtetea, uwezo wake yafaa afundishe timu modest kama Mtibwa, Mbeya City au Mwadui. Hafai kabisa na ni mtu wa visingizio tuu. Very hopeless.

............ukipewa timu utaifikisha hatua gani?
 
Hao mbona tulishawatoa na ndio kisa cha Ngoma,,Kamusoko na Chirwa kuja Yanga
Hatuzungumzii history, tunazungumzia yanga ya sasa ya Zahera, inàweza kuitoa Platinum ya sasa?
 
kumbe Simba timu mbovu sana maana wababe wao walioshindwa kuwafunga UD SONGO wamefungwa mechi zote nyumbani na ugenini na platinum ya zimbabwe
Simba hajatolewa kwa kufungwa
Na mpaka simba inatolewa haijwai kufungwa klabu bingwa mwaka huu
Simba imetolewa kwa kanuni

Wkt yanga imetolewa kwa kufungwa 2-1
 
kumbe Simba timu mbovu sana maana wababe wao walioshindwa kuwafunga UD SONGO wamefungwa mechi zote nyumbani na ugenini na platinum ya zimbabwe
Zilongwa mbali zitendwa mbali.. Simba kaingiaje hapa? Mada mwinyi zahera na mustakabali mzima na kazi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…