Belo
JF-Expert Member
- Jun 11, 2007
- 12,897
- 10,213
Yanga haiwezi kuwa na mshabiki mbumbumbu kama weweMimi Yanga damu Boban ni mhenga kaja kula pension
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yanga haiwezi kuwa na mshabiki mbumbumbu kama weweMimi Yanga damu Boban ni mhenga kaja kula pension
Kawaida tu mbona chapati za kaduguda azijalipwa hadi Leo🍪🍪Yanga mnadaiwa mpaka na waganga.
Unanipangia timu? Yanga Chama langu Sema siku hizi hatuna timuYanga haiwezi kuwa na mshabiki mbumbumbu kama wewe
Hivi haya matumaini ya sisi wanayanga kuchukua ndoo yanatoka wapi? Ni hivi vimechi vichache tulivyoshinda,Siamini kitu gani?
Boban kuitumikia Yanga miezi sita. Ndoo inaenda Jangwani kama kawaida.
Wewe siyo Yanga NahisiHivi haya matumaini ya sisi wanayanga kuchukua ndoo yanatoka wapi? Ni hivi vimechi vichache tulivyoshinda,
Timu ya kuchukua ubingwa hatuna tushukuru mungu angalau tumekusanya points za kutosha hatuwezi shuka daraja.
Kwako mwalimu kashasha
Yanga bwana mnatapatapa kama mfa maji.
Bila kusahau zile hela za rambirambi za Marehemu Mafisango,nikikumbuka nalia sana hiii hiiii hiiii.Kawaida tu mbona chapati za kaduguda azijalipwa hadi Leo[emoji514][emoji514]
Great Bhinda.NIMJUAVYO HARUNA MOSHI 'BOBAN'
Kwanza kabisa ningependa nikujulishe ndugu msomaji, kuwa mie niandikae ujumbe huu naitwa Mohamed Bhinda, naweza kusema kuwa ni mtu pekee niliyewahi kuiongoza klabu ya Yanga kwa takriban miaka zaidi ya ishirini kwa nyakati tofauti na nyadhifa tofauti, sina lengo la kujisifu juu ya jina langu ndani ya klabu ya Yanga, bali nakudondolea kidogi tu ili kukuandaa msomaji juu ya nimjuavyo Haruna Moshi 'Boban'.
Haruna Moshi ni mmoja ya watoto wa Mzee Moshi, ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa Shirika la Reli nchini, mzee huyo mwenyeji wa Tabora alikuwa ni mkaguzi wa tiketi ndani ya treni za shirika hilo 'TT'.
Familia ya Mzee Moshi imejaaliwa kuwa na vipaji vya uchezaji wa soka, licha ya watoto wake wengine, hapa tunamchukua Iddi Moshi 'Mnyamwezi' ambaye alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya Yanga kwenye simulizi hii fupi.
Mwaka 1999 mie nikiwa Meneja mkuu wa Timu ya Yanga, tulitwaa kombe la ubingwa wa Afrika Mashariki na kati nchini Uganda, wakati huo kocha mkuu alikuwa mkongo Roul Piere Shungu,
Mara baada ya kupata ubingwa huo, ambapo Idd Moshi alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa Yanga, timu yetu ilipata mialiko mikoa kadhaa katika kusheherekea ubingwa huo,
moja ya mkoa tulioalikwa ulikuwa ni Morogoro kucheza na Mtibwa mchezo wa kirafiki,
Kwenye kikosi kilichokwenda mjini Morogoro, Haruna Moshi Boban naye alikuwemo, wakati huo bado mdogo sana kiumri,
Kwenye mechi hiyo dhidi ya Mtibwa, Kocha Roul Shungu alimuingiza Haruna zikiwa zimebakia dakika ishirini hivi, siku hiyo Haruna alicheza soka ya hali ya juu licha ya udogo wake, baada ya mechi kwisha kocha Shungu alishauri tumsajili, tulishauriana ni kwa namna gani tutamsajili Haruna wakati akiwa chini ya miaka 15?, wakati huo Haruna alidhamiria kuchezea Yanga, binafsi naweza kusema ndio ilikuwa ndoto yake, wakati sisi Yanga tukisuasua juu ya umri wake, ndipo walipotokea watu wa Simba na kumpeleka Coastal Union ya Tanga na baadae kumsajili Simba, naweza kukiri kuwa Yanga tulizembea.
Miaka ikapita ndoto za Haruna kuchezea Yanga zikawa kichwani mwake, ndipo siku aliyotaka kusaini Yanga kutoka Simba, palifanyika umafia wa kumtorosha kwenye uwanja wa Muhimbili ambapo mie nilipanga na Imani Madega kwenda kumsainisha mkataba, nakumbuka watu wa Simba walivamia pale shule ya msingi Muhimbili na kuzima taa za uwanjani na kumteka Haruna.
Tulimuandalia safari Haruna kwenda Arabuni kwa mkataba wa mwaka mmoja, na lengo akirudi asajili Yanga, aliporudi aliikuta Yanga ipo kwenye migogoro, hivyo ilishindikana kumsimamia usajili wake.
Miaka imepita na Haruna kalinda kipaji chake, leo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera katangaza mwenyewe kuwa amemtaka Haruna Moshi 'Boban'.
Ha ha haaaa, ndoto za Haruna kuchezea Yanga zimetimia japo kwenye utu uzima, waswahili wanasema "mwenye kujua anajua tu, kipaji akijifichi".
Karibu Haruna Moshi Boban kwenye timu uliyoidhamiria kuichezea tangu utotoni,
M.S.Bhinda
2018
Katika pitapita zake akamwona kwenye TV anatoa pasi nzuri,na ndo mara ya kwanza kumwona
Kamusoko majeruhi yanamuandama..hawezi kucheza mechi mfululizoMkuu acha kumfanisha Pirlo na vitu vya ajabu, kiungo inaitaji kiongozi yule Babu kamusoko ni kipa au beki? Yanga kwa Sasa inaenda kwa kundra tu
Huo ni mfano sijafananisha uchezaji wa Pirlo na Haruna..kinachofanana ni mazingira ya usajili..Rage njoo uchukue watu wako hukuHahaha, watu tunajua kujipa faraja, ati Andrea Pirlo!
Mkuu hebu acha utani bana.
Hivi ile billioni 20 imeanza kuleta faida au Gabacholi anaongeza deni mwenye ile bilioni sita anayowadai????Yanga mnadaiwa mpaka na waganga.
Mmmh boban humjui jamaa kashiriki vita ya KageraBoban na kagere nani mzee?kagere kaanzal kucheza mpira wakati police wanavaa vipensi kipindi cha soboso huko,itakua huyu boban alieanza juzi tu hapa
Yanga hata wakimsajili Hadija Kopa watashinda tu.Nasikia Yanga wanataka kumsajiri kwa mara nyingine Sunday Manara ili kumkata ngebe Haji Manara.
Mimi nitawasaidia wawasajiri pia Nteze John "Rungu",Fikiri Magoso na Chibe Chibindu ili kuboresha kikosi chao.
Yanga Veterani Oyeeeeee!![emoji16][emoji16][emoji23]
Toa hela ili wasajili unavyotaka.Mimi Yanga damu ila sitaki timu ya kuungaunga Kama timu ya umitashumta au umiseta
Tupo sahihi kabisa mwananchi mwezanguMhuu Hapa YOUNG AFRICANS FOOTBALL CLUB "The Citizen Team" bado sijaelewa elewa vizuri hivi. Vipi wananchi wenzangu yaweza kuwa sahihi hii!?
anawashwa uyo mkuu mvumilie tuuuWewe jamaa utakufa kwa presha kuifatilia fatilia yanga. Wewe si ndiye uliandika na uzi ya kwamba Yanga wanashinda kwa bahati na upepo na ipo siku upepo utakata. Inaonekana jinsi gani Yanga inakupa maumivu ya moyo.