Zahera hana mpango wa kuondoka Yanga

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Nimesoma gazeti la mwananchi Online limemnukuu Zahera akisema," Kurushiwa makopo kawaida wala haimuumizi kichwa." Akaongeza yeye bado anamkataba na Yanga.

Huyu jamaa sjui kwanini anang'ang'ania Yanga wakati anasema halipwi chochote.

Mi ananichefua! basi tu.
 
Hatari
Your browser is not able to display this video.
 

Akiondoka Nani Atalipa Mishahara Hao Wachezaji?
 
Timu haipigi hata pasi tatu..aisee hata ally mayai hawezi kufundisha mpira mbovu vile akipewa timu[emoji16]
 
Zahera alilipa mpaka posho za wachezaji vyura watapata kocha mwekezaji wapi tena,kamleta makambo kamuuza kavuta mpunga ,tukumbuke anayofamilia avumiliwe huyo ,na sio lazima timu zote ziwe vizuri kuimba kupokezana Simba wanapaswa kuchukua VPL miaka 10 ndio tujadili ya vyura
 
Hiyo mbona iko wazi kabisa. Ikitokea ameondoka mwenyewe itabidi ailipe Yanga kwa kuvunja mkataba. Anachosubiri (na hata ingekuwa mimi) ni Yanga kumfukuza ili alipwe gharama za kuvunjiwa mkataba wake. Kwa hiyo akitupiwa makopo, mawe, n.k. bado atavumulia tu mpaka uongozi uvunje mkataba na si yeye kuuvunja mkataba. Tofauti na hivyo ni uongozi wa Yanga kukaa na Zahera meza moja na kukubaliana kwa pande zote kuvunja mkataba kistaarabu ukizingatia wamekaa muda kidogo pamoja ili Zahera asemehe baadhi ya madai yake na kwa kuwa uongozi hauna ugomvi nae hili linaweza kuwa suluhisho rahisi kuliko yote. Katika hali kama hii uongozi itabidi wamuombe Zahera apunguze/asamehee baadhi ya madai wamlipe ili ampishe kocha mwingine.
 
Hakuna mtu Yanga wanamwogopa kama Zahera, sijui yule jamaa ni mchawi, Yanga wanatamani aondoke hata Leo lakini ujasiri wa kumwondoa hawana bali ajiondoe mwenyewe.


Atavurundaaaa weeee lakini hakuna wa kusitisha mkataba wake mpaka atakapopenda mwenyewe.
 
Wewe inakuhusu nini?? Sisi wana Yanga kindakindaki tunafahamu na ndiye tunayemuhitaji kwa sasa.
 
Atang'ang'ania weee! ila mwisho wa siku atang'oka tu. Atake asitake. Hana jipya, hana mbinu mbadala, hana plan B! Na siku ya kuondoka, aondoke na Noel Mwandila! maana hatuna upungufu wa makocha wasaidizi na wazalendo wa timu nchini mwetu.

Yaani unawaacha wachezaji wazuri halafu unasajili magarasa! Halafu unakuja kujitetea kwa sababu nyepesi nyepesi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…