Zahera ni mmoja wa makocha wazuri sana, Yanga musije kumpoteza

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Nimeangalia makocha wengi Tanzania na afrika.sijaona kocha kama Zahera. Yanga wanapaswa kuwa wavumilivu wampe nafasi. Ana vitu vikubwa sana wasije wakamwacha haraka Simba au Azam wakamchukua.

Toka amekuja mwaka jana Yanga imebadilika sana.inacheza mpira wa nguvu na mambo mambo mengine. Usajili alioufanya ni moja ya Sajili nzuri sana sema tu wachezaji bado hawajapata chemistry nzuri.ila naona yanga ambayo itatisha sana msimu huu.

Mmeona jinsi ambavyo ameifikisha yanga hapo ilipo kimataifa.yanga imekuwa na uwezo wa kupindua matokeo ugenini bila hofu kabisa.

Nawashauri chonde chonde msimwache Zahera ni kocha mzuri sana kwa sasa hapa Afrika na pengine Ulaya, ukichukulia amewahi kufundisha vilabu vikubwa Ufaransa.
 
Mwinyi Zahera agombaniwe na Azam na Simba! Ngoja waje wahusika walijibie hili. Mimi ninavyofahamu, Yanga ilikuwa ikicheza mpira mzuri enzi za babu Hans na pia George Lwandamina!

Walivyo ondoka hao walimu wawili, ndipo Yanga ikaanza tena kucheza mpira usiovutia na kueleweka, ingawa ilikuwa ikijipatia matokeo wakati fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…