Zahera yuko kibiashara, Yanga zindukeni

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Bado wanaYanga wana kumbukumbu yenye maumivu juu ya Biashara ya Heritier Makambo kwenda Horoya. Maumivu yakiwa bado hayajapoa kwa sasa Maabara yupo Molinga anasukwa.

Anapewa Promotion ya kila namna, anapewa dkk 90 za kucheza, anapambwa kwa kila namna na mwisho wa siku Zahera atamwita kwenye top 50 ya timu ya Congo ili KumBrand na kupaisha thamani yake.

Mwisho wa Msimu huyoooo Wydad Cansablanca bila Yanga kuambulia chochote.

Biashara ya Zahera itakuwa imetiki
Yanga tustuke mapema, Klabu iache kutumika kama Academy ya Zahera kubrand wachezaji na wa Kicongo na kuuza. Hata hivyo namsifu Zahera kwa ujanja na Elimu hii ya hali ya juu. Ni ushauri tuu Wanajangwani
 
Zahera kuna jambo ambalo analifanya afu YANGAwako kimya tu. Haiwezekani ktk game 2 za ligi plus zile za mwanza amchezeshe Molinga almost dk 360 zote wakati Yanga kuna washambuliaji wengine. Huyo molinga kwa maneno yake anasema anahitaji kupunguza mwili kwa maana nyingine hayupo sawa kwanini wengine hawachezi. Game na ruvu hata ya coastal nilitegemea atampa dk chache iliwengine wacheze pia kutafuta ushindi.
Bado yanga haionekani kutafuta ushindi hata goli limekuja tu.
 
SI JAMBO GENI KWA KOCHA KUMBRAND MCHEZAJI ILI APANDE THAMANI, TATIZO NI PALE LINAPOFANYIKA KWA MASILAHI BINAFSI, UTAKUTA HUYO MOLINGA ANA MKATABA WA MWAKA MMOJA TU
 
Molinga waweza kuta hana mkataba na Yanga dizaini ya Makambo ili Zahera apige zote wakati wa mauzo
 
Mikia bwana unajua wanachekesha.Iko hivi wewe mkia kaa chini nikupe darasa la mpira.
Ivi kama Molinga akifanya vizuri Yanga,akauzwa kwenda iwe ni ulaya,Asia,America au hapahapa Africa sifa inabaki kwa Yanga Africa.na Tz.samata anasifika kwa TP mazembe sio simba kwa sababu ndio iliyomtoa kimataifa.Kama Yanga ikifanya vizuri katika kuuza wachezaji hata kama haifaidiki ipasavyo lakin inaipa heshima timu na nchi.

Msuva amefanya vizuri Moroco ndo maana wananunua vijana wetu wengine kuwapeleka Moroco,bila samata Genk wangemwona Kelvin John?

Simba mbona ina wachezaji bora lakin haiuzi nje ya nchi Kama Yang@? Jibu ni kuwa wanatambua kuwa wachezaji wa simba sio vipaji asilia.Ndio maana baada ya msimu jana kufanya vizuri kimataifa wakazimia.Saiz ndo wanazinduka tena.

Mpira ni strategy.Yanga ni timu Ya mipango sio blablabla kama mbumbumbu
 
Tuweke Kumbukumbu vzuri..
Unasema Yanga ndio imeuza sana Wachezaji nje ya Nchi? Be serious brother
 
hivi Kagere mbona sijawahi kusikia kuna timu huko nje inamuhitaji? au kwa sababu mechi za kimataifa anapotea kabisa
 
hivi Kagere mbona sijawahi kusikia kuna timu huko nje inamuhitaji? au kwa sababu mechi za kimataifa anapotea kabisa

Atakua anatumia dawa za kuongeza nguvu yule! hivyo anahofia akitoka nje ya nchi, huenda akashtukiwa! Haiwezekani mchezaji ana miaka karibia 40, lakini anafunga tu magoli kama Tammy Abraham wa Chelsea!
 
Mo Dewji yupo kihisani au kiufadhili zaidi?
 
Kikubwa kwa sasa awape wanachohitaji kwa sasa. Ambacho ni matokeo.
Umaskini mbaya sana na yanga ni maskini.
 
Uko Kijiji gani mkuu kiasi kwamba hujui hisa anazomiliki MO ndani ya simba
Nipo Mkoani Dar.
Anamiliki 49% hewa . Hajatoa hata senti moja kununua hizo hisa. Ni mfadhili tu hadi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…