Trophic
Member
- Jun 8, 2020
- 11
- 8
Hello JamiiForums,
Hii itakua thread yangu ya pili humu Jukwaani toka nijiunge kama member June, 2020. Mimi ni Producer, Composer & Songwriter. Ndani ya miaka mitatu nimekua nikijaribu kuendeleza craft yangu kiujumla na ningependa muweze kuipitia na kunipea genuine feedback, your support and maybe be fans. Sijawahi sikia nyimbo iliyotembea kisa JF, sio mbaya hii ikiwa ya kwanza 🤞🏾
Anyways, nyimbo yenyewe ni Zaidi/Mama na ni tribute kwa kina mama wote, especially mama angu mzazi. Kikwetu kwetu, ni ngumu/nadra sana kwa watoto wakiume kuwaambia wazazi wao wanavyowapenda, sikuwahi kumtamkia mama angu neno hilo na mwaka jana, 2022 nlimpoteza ikawa one of my biggest regrets. Mziki ni namna yangu ya kudeal na stress, depression and the likes. Hivyo, in her honor, na kwa kina mama wote, nimeandika huu wimbo.
P.S. Kama mama ako uko nae bado, nadhani ni vyema kumwambia ni namna gani una mu appreciate, when you still have the time.