Taarifa zinaonesha kuwa zaidi ya ekari 15,000 za ardhi ya misitu ziko katika mchakato wa kuondolewa hadhi ya misitu (degazettement), hatua inayoweza kufungua njia ya ardhi hiyo kupewa hati miliki.
Maeneo yanayotajwa ni Mount Elgon Forest – ekari 11,483, Turbo Forest – 3,069, Kakamega Forest (Shiru) – 235, Kakamega Forest (Shaviringa) – 89, na South Nandi Forest (Chepkumia) – 2,444. Kwa jumla, takwimu hizi zinafika takribani ekari 17,320.
Kinachozua maswali zaidi ni madai kwamba baadhi ya wakazi wanaoishi karibu na maeneo haya hawana taarifa za kutosha kuhusu kinachoendelea.
Mchakato huo unadaiwa kuanzishwa kupitia ombi lililowasilishwa Bungeni na Waziri wa Mazingira Deborah Barasa, huku ripoti ya kamati ya Bunge ikionesha pendekezo hilo limepiga hatua kubwa kuelekea kukamilika.
Wakati huohuo, kuna madai ambayo hayajathibitishwa kwamba baadhi ya wanasiasa wanaweza kuwa na maslahi katika ardhi hiyo. Pia kumekuwa na taarifa kuhusu Mama wa Taifa Rachel Ruto kuhusishwa na mpango wa “adoption” wa Kakamega Forest—jambo ambalo halimaanishi umiliki wa msitu, lakini linaongeza umuhimu wa kuweka wazi mchakato huu kwa umma.
Wadau, tuambiane ukweli: Kwa nini maelfu ya ekari za misitu yanaondolewa hadhi? Ni nani atapewa hati za ardhi hii, na wananchi walipewa nafasi gani kutoa maoni? Mwisho wa siku, nani atanufaika?