Zaidi ya Sh Bilioni 510 kujenga laini ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze Substation hadi Dodoma

Zaidi ya Sh Bilioni 510 kujenga laini ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze Substation hadi Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeikabidhi Kampuni ya TBEA ya nchini China kandarasi ya kuanza ujenzi wa laini ya kusafirisha umeme kutokea Kituo cha kupozea umeme 'Chalinze Substation' mkoani Pwani hadi Dodoma ikigharimu Sh Bilioni 510.

Akizungumzia kandarasi hiyo Aprili 17, 2024 akiwa Chalinze - Substation, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, amesema utekelezaji wa kandarasi hiyo ambayo inamtaka mkandarasi kukamilisha ndani ya miezi 22 kipande hicho chenye urefu wa kilometa 345 utaongeza tija ya kupatikana kwa umeme zaidi nchini.
WhatsApp Image 2024-04-18 at 10.02.50_4b4bc5d1.jpg
"Tunaanza utekelezaji rasmi wa mradi wa laini kubwa ya umeme ya msongo wa Kilovati 400 ambayo itabeba umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma," amesema Mkurugenzi huyo.

Ameongeza "Ule umeme unaotoka Julius Nyerere (JNHPP) unafika Chalinze unaenda maeneo mengine ya Nchi yetu kwa kutumia laini ambazo ni ndogo," amesema Mkurugenzi huyo.

Pia ameeleza umeme huo utasafirishwa kupitia line hiyo kwenye kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichopo jijini Dodoma na kuwa baada ya umeme kufikishwa hapo itakuwa rahisi kufika maeneo mengine ya Tanzania kwa kuwa utasambazwa.

Ameongeza kuwa umeme ambao utasafirishwa kutoka Chalinze hadi Dodoma unatokea kwenye mradi mkubwa wa JNHPP, ambapo amesema kwa siku za mbeleni Kituo cha Chalinze kinatarajia kupokea umeme zaidi kutokana na mitambo mingine ambayo bado haijawashwa.
WhatsApp Image 2024-04-18 at 10.02.50_a37559eb.jpg

WhatsApp Image 2024-04-18 at 10.02.49_4a0388ac.jpg

WhatsApp Image 2024-04-18 at 10.02.50_ae258e96.jpg

"Sasa hivi kule JNHPP tunapata Megawati 235 kuja hapa Chalinze, lakini mitambo yote tisa kule ikianza kufanya kazi maana yake umeme utakaokuwa unatoka kule ni megawati 2,115," ameeleza Mkurugenzi huyo.

Akifafanua sababu na umuhimu wa laini hiyo amesema kuwa waliamua kutekeleza suala hilo hili kutanua wigo wa miundombinu itakayowezesha kusafirisha umeme mwingi zaidi hasa baada ya mradi wa JNHPP kuanza kutoa megawati zinazotarajiwa, ambapo amedai kuwa laini iliyopo sasa ina uwezo wa kusafirisha megawati 850, hivyo amesema kuwa haiwezi kuhimili umeme wote baada ya mitambo yote kuwashwa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho amesisitiza miradi huo kukamilika kwa wakati huku akiitaka menejimenti ya Tanesco kusimamia suala hilo kwa ukaribu zaidi.

"Kazi hii inachukua miezi 22, kila kitu kama kipo, fedha hipo tuhakikishe mkandarasi anaweza kutimiza suala hili kwa ndani ya miezi 22, kwahiyo menejimenti mtusaidie kusimamia kila kitu kiende sawa ubora uzingatiwe," amesema Dkt. Rhimo Simeon.

Ameongeza kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na laini za kusafirisha umeme zenye ubora ili kuwezesha umeme unaozailishwa kwenye vyanzo mbalimbali unakuwa na tija, amedai kuwa kunaweza kuzalishwa umeme wa kutosha lakini bila kuwa na laini rafiki inaweza kuleta changamoto.

Hivyo, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utasaidia kufikisha umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini kilingana na uwekezaji unaoendelea.

"Watanzania wanataka umeme uwepo hata tukizungumza sana, tukiandika sana, tukifanya kila aina ya kitu lakini kama mgao wa umeme upo bado hatujafanya kazi," amesema Dkt. Rhimo Simeon.
 
Back
Top Bottom