Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

Pole sana kwa wote walioathirika na ajali hii kubwa.

Muhimu kwasasa ni kuangalia namna ya kuzuia hayo machimbo kufukia
watu kila mara.

Kwa mtu maskini hana choice, kufa kwa kufukiwa au kufa kwa umaskini.

Serikali ina wajibu wa kusaidia kuondoa umaskini uliokithiri ili watu wasilazimike ku take rfisk kubwa kama hawa wachimbaji wadogo wadogo.
 
Pole sana kwa wote walioathirika na ajali hii kubwa.

Muhimu kwasasa ni kuangalia namna ya kuzuia hayo machimbo kufukia
watu kila mara.

Kwa mtu maskini hana choice, kufa kwa kufukiwa au kufa kwa umaskini.

Serikali ina wajibu wa kusaidia kuondoa umaskini uliokithiri ili watu wasilazimike ku take rfisk kubwa kama hawa wachimbaji wadogo wadogo.
hakuna cha kuathirika hapa hawa wamepata lana kwa kuwaua maalbino ,jana nilizungumza na mkereketwa mmoja wa machimbo ambae yeye ni mteja ,amesema sasa watapata dhahabu na vito vingi zaidi ,kwani jopo lililokwenda na mizimu ni kubwa ,hivyo mali itakuwa nje nje na wanatarajia kupata kwa wingi.
Sasa ndio nimeona kuna wengine wanasikitika wakati wengine ndio wamefurahi ,eti vipuri vya mazeruzeru huwenda vikashuka bei kwani kwa sas havihitajiki kwa karibu wala hakuhitaji waganga.
 
poleni sana ndugu zangu ...najua mlikuwa mkipambana na ugumu wa maisha ...ni mashujaa...tunajua mmekufa kwa sababu usalama wa washimbaji wadogo haudhaminiwi...tunajua mmekufa kwa ajili ya ugumu wa kupata madini siku hizi hasa baada ya muwekezaji kaburu ..kwa kutumia vifaa kuingia hadi maeneo yenu kwa chini na kukomba madini yote ambayo ni urithi wetu na zawadi yetu adimu...tunajua ipo siku watoto wenu wataiona tanzania iliyo bora kutokana na jasho lenu la maji na damu!!!

Mungu awape pumziko la amani na milele amina!!!
 
Taifa lisilo na kipaumbele! Lakini ngoja aje muwekezaji mkubwa muone jinsi gani masharti ya sheria ya madini yatakavyojaribu kufuatwa... Hawa maskini wa Mungu wanachangia nini kulinganisha makampuni makubwa au wanachimba ili wapate cha kula na cha kulalia?

Ni siku ya msiba tumepoteza watu, lakini zaidi pia tumepoteza ile hali ya kujali utu na thamani ya kila Mtanzania. Hii siyo ajali ya kwanza kutokea mererani, na haitakuwa ya mwisho; lakini ni mojawapo ya yale yale yanayojirudia kwa sababu tumeshindwa kubuni jinsi gani tunaweza kuwasaidia vijana hawa kufanya kazi katika hali ya usalama (vifaa, codes n.k)

Kwa vile machimbo mara zote hubeba risk bila kujali ambapo mgodi upo lakini haya ya maji kufurika tunaweza kabisa kuangalia jinsi gani ya kupunguza vifo.

Lakini siwezi kushangaa maana kama wameshindwa kuhakikisha maji yanatiririka msimbazi au kutengeneza drain system kwenye jiji la mabilioni la Dar, wataweza kufanya hivyo Mererani?
 
R.I.P
I hope serikali will impose more rules concern safety. Vile vile i hope waziri wa madini will impose check list before they start to operate again.

I believe the safety katika haya machimbo ni sawa na sifuri, i don't know kama serikali inafanya safety analysis every now and then. I know ajali kwenye madini ni part of kazi, lakini i guess its a time hawa investors waoperate the same way wanavyo operate kwenye machimbo ya nchi zilizo endelea.

Regular ispections is something missing katika machimbo ya africa. Na hii inasababishwa na serikali kuwa so easy kwa hawa wawekezaji katika sector ya madini. It a good time kwa new cabinet kushine in.

I hope Masha and waziri wa Nishati na Madini will ask bunge to impose new law concern safety and inspection katika madini. I don't know hata kama kuna kiongozi anaefahamu what is the maximum hours kwa mchimbaji wa kawaida anatakiwa kuwa under the ground.

Majanga kama haya yanapotokea ndio inatakiwa iwe time mahususi ya kurestudy the whole sector na kuangalia kama kunaumuhimu wa kuweka rules and regulations mpya. Otherwise, tutapoteza watanzania wenzetu wengi kama haya mambo hayataangaliwa.

Poleni wafiwa, Poleni Watanzania. Mwenyezimungu Inshallah aawafanyie wepesi wafiwa wote
 
we cant act like all thats happening in TZ is whats in headlines..Kuna matatizo mengi,ajali, vifo n.k in all parts of the country, hii sio baby-day-care State tunalia the President anakula kuku watu wanakufa;yaani, kama vile kuna proportionality ya ulaji wake wa Chicken na vifo...Nyerere,Mwinyi,BMW wote wamekula, Rais wa Comoro hata yeye na umati wake wa wananchi wanaoweza sell-out Stadium ya kisasa ya mpira,pia hula Kuku..JK ale nini sasa?

we WHINE too much...I say Ngereja should go there Now....lets all call HMM..

+ 255-787-603-535

We'll know kama halishughulikii kabisa, Ngereja may need the Headline..Yaani, hata El Ninho ikimwaga mvua machimbo is JK Fault??

Your missing the point. President is entitle especial when more than 100 people died. Bush late to showed up in Louisiana during Katrina, that killed his reputation.

More than 100 poor Tanzania wamezikwa hai more than 100 feet below ground. Hakuna swala la kuwa Butiama wala Majengo. You expect rahisi awe kwenye 7:00Am breakng news declare state of emergency, na sio kuwepo kwakwe kwenye tea party with banch of corrupted loosers NEC members.

When you decide to run for president, you need to know your taking a #1 position in the world. When Hasheem Thabeet out performed you will get bravo for that, also when disaster happen and you late to respond you will get blame for that. So, there is no cherry pick on presidential position. Kwamba hili lina nihusi na hili haliniusu linawausu mawaziri.

Good Job kwa Pinda. I hope more action will be taken in a near future for better of Tanzania. Mungu ibariki Tanzania
 
mererani.jpg
ANGUISH AND DESPAIR: Small-scale tanzanite miners listen to Philip Marmo, Minister of State in the Prime Minister`s Office, at a meeting between them and three ministers at the Mererani yesterday in the wake of floods feared to have killed over 70 miners.


Uopoaji maiti Mererani wasuasua



*Ukosefu wa vifaa ni tatizo sugu
*JK atuma salamu za rambirambi

Na Said Njuki, Mererani

KAZI ya uopoaji maiti ndani ya migodi ya tanzanite, Mererani wilayani hapa, imezidi kuwa ngumu na hata kukwama kutokana na ukosefu wa vifaa vya kuopolea zikiwamo pampu za kuvutia maji kutoka mashimoni.

Hali hiyo imetokana na kwamba takriban miili 67 bado imo ndani ya migodi hiyo, huku miili sita tu ndiyo ikiwa imeopolewa juzi asubuhi huku viongozi wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Henry Shekifu, wakiunda kamati kadhaa.

Baadhi ya kamati hizo ni ya Operesheni Okoa itakayoongozwa na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Venance Tossi, ya Maafa ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Bw. Khalid Mandia na Katibu wake ni Ofisa Madini wa Kanda, Bw. John Nayopa.

Kamati nyingine ni ya wataalamu ambayo wengi wa wajumbe wake ni wachimbaji madini.

Lakini wakati kamati hizo zikiendelea kujipanga, baadhi ya wachimbaji walionesha wasiwasi wao juu ya uwezekano wa kuopoa miili hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, mchimnbaji Sokota Mbuya, alisema mbali na vifaa kupatikana, Serikali inatakiwa kutoa msaada moja kwa moja wa chakula na posho kwa wachimbaji wazoefu, kwani eneo hilo limekumbwa na baa la njaa na hivyo kuingia mgodini na njaa ni vigumu.

Alisema maiti hawawezi kuopolewa na wataalamu wa Jiolojia peke yao, kwani hata katika maafa ya mwaka 1998 wataalamu hao na vikosi vya majeshi, walisaidiwa kupanda juu baada ya kuingia na kushindwa kutoka.

Mama Stella Shayo, ambaye pia ni mchimbaji, aliwahoji kwa kejeli viongozi wa Serikali akiwamo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Bw. Philip Marmo; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Lawrence Masha na Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja, kwamba Serikali Kuu ilifuata nini pale badala ya kuendelea na vikao huku miili ikiendelea kubaki mashimoni.

Akizungumza katika mkutano huo, Bw. Shekifu pamoja na kuwataka wachimbaji kushirikiana katika kadhia hiyo, pia alisimamisha kwa muda usiojulikana shughuli zote za uchimbaji katika migodi hiyo ya vitalu A, B, C na D.

Akizungumzia hatua hiyo, Mkaguzi Mkuu wa Madini nchini, Bw. Edwin Ngonyani, alisema Serikali hufanya kazi kwa mujibu wa sheria ya usalama migodini, inayoipa mamlaka ya kufunga migodi na moja ya sababu ni kuhakikisha kila mmoja anashiriki katika shughuli hiyo.

Waziri Marmo kwa upande wake, alisema Serikali inafanya kazi na kamati mbalimbali za maafa za ngazi zote na atapokea mapendekezo ya kamati husika ili naye atoe mchango wake.

Lakini wakati yote hayo yakiendelea, tayari wataalamu kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick waliripotiwa kutua Mererani, ili kuongeza nguvu za uopoaji huku wajumbe wa moja ya kamati wakiwa migodini tangu asubuhi kutathmini ugumu wa kazi hiyo.

Kamati hiyo inaundwa na wachimbaji, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wana usalama, Polisi.

Jumla ya wachimbaji 166 ndio waliodaiwa kuingia katika migodi hiyo huku 93 wakitoka salama na 67 wakiaminika kuwa bado hawajaopolewa. Ajali hiyo ilitokea juzi kwa mashimo kujaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Mkoa na wananchi wa Mkoa wa Manyara, kutokana na maafa hayo.

Taarifa ya Ikulu kutoka Butiama, Musoma jana, ilisema Rais alipokea kwa masikitiko, huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za janga hilo kubwa.

Alihuzunishwa kwa upotevu wa maisha ya watu ambao mpaka sasa imethibitika kuwa wamepoteza maisha.

Rais pia aliwaombea wachimbaji ambao taarifa zao hazijathibitika waweze kupatikana haraka wakiwa hai na salama na pia aliwaombea wote walioumia katika ajali hiyo wapone haraka.

Alitoa pole kwa familia ambazo zimeathirika na janga hilo na kuzihakikishia kuwa yuko pamoja nazo katika wakati huu wa majonzi na huzuni.

Kutoka Tanga Bakhya Said, anaripoti kuwa kivuko cha Mto Pangani, mv Pangani kilizama juzi saa moja asubuhi wakati kikipakia gari lililokuwa limebeba marobota ya mkonge yenye uzito wa tani nane na kusababisha mlango wa kivuko hicho kukatika.

Akizungumzia juzi mchana baada ya ajali hiyo katika eneo la tukio, katika gati la ng'ambo ya Bweni, Mkuu wa kivuko hicho, Bw. Marko Manyala, alidai kuwa chanzo cha ajali ni uchakavu wa milango ya kivuko hicho.

Bw. Manyala alisema katika ajali hiyo hakuna abiria wala mfanyakazi aliyepata madhara kwa kuwa kilizama katika gati kabla ya abiria kuingia.

"Tulianza kazi saa 12 asubuhi na tulivusha basi na abiria, lakini dereva wa gari lililobeba marobota aina ya Mitsubishi T 416 AMG lililokuwa na uzito wa tani nane kabla ya abiria kupanda, tulimruhusu aingize gari lake na baada ya kuingiza tairi za mbele alifunga breki ghafla na uzito wote ukawa nyuma ya mlango, ukakatika likabaki linaning’inia na sehemu kubwa ya kivuko ikawa imeshikilia majini," alisema Bw. Manyala.

Alisema maji yalivyozidi kujaa kivuko hicho kilizidi kufunikwa na maji lakini walivuta gari hilo ambalo nusu lilikuwa nchi kavu kwenye gati na nusu kwenye kivuko.

Wakati hali hiyo ikitokea Naibu Waziri wa tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi Selina Komba alikuwa katika ziara ya siku tatu kutembelea miradi mbalimbali ya wananchi na kusikiliza maoni na kero zao na alipangiwa kuvuka ng’ambo ya pili ya Mto Pangani, ambako ndipo ilipo sehemu kubwa ya Wilaya.

Naibu waziri huyo alilazimika kuvuka kwa kutumia boti na pia alijionea hali halisi ya kivuko hicho na amekiri kuwa malalamiko ya wananchi na viongozi wa wilaya ya Pangani yana msingi sana.

Wakati haya yakitokea, msafara huo wa Naibu Waziri pia uliongozana na Mbunge wa Pangani, Bw. Rished Abdallah.

Jana mafundi wa kivuko hicho walikuwa wamefunga mapipa na kuweka pampu za kutolea maji, ili kukifanya kiweze kuelea ili waanze ukarabati wa bodi na mashine ambazo zimeingia maji ya chumvi.


majira
 
merre.jpg

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Bw. Khalid Mandia (wa pili kulia) na wachimbaji wadogowadogo wakishuhudia baadhi ya miili ya wachimbaji walioopolewa kutoka migodi ya Tanzanite Mererani juzi katika Kituo cha Polisi cha Merererani. (Picha na Said Njuki)
 
Mwenyezi Mungu awarehemu vijana wana-apollo. Niliyoyaona Mirerani jana yamenipa simanzi. Kuna mengi zaidi ya yanayoandikwa magazetini. Naendelea kutafakari na siku chache sijazo nitarejea kutoa mang’amuzi yangu.
 
No safety yeyote katika hayo machimbo na nina uhakika hakuna kodi inayokusanywa kutoka kwa hawa wachimbaji ili kuendeleza wananchi wa eneo hilo kutokana na huo utajiri mkubwa,yaani ni hasara juu ya hasara,na pande zote zina loose tuu...RIP!
 
No safety yeyote katika hayo machimbo na nina uhakika hakuna kodi inayokusanywa kutoka kwa hawa wachimbaji ili kuendeleza wananchi wa eneo hilo kutokana na huo utajiri mkubwa,yaani ni hasara juu ya hasara,na pande zote zina loose tuu...RIP!

Jamani nimeona habari hii ya watu kufa machimboni haijapewa uzito wowote a vyombo vya habari .Nimebaki nashangaa kwamba si CCM na NEC yao wamesema lolote na hata Waziri Mkuu kufika katika tukio ama Rais kusema lolote .Maisha ya watu 100 ni jambo kubwa kufa kwa mara moja .Najiuliza kama wawekezaji hawana vyombo vya kuweka kuvuta hata maji na kupata miili ya wahanga wale .Jamani ni kweli CCM kwanza na Watanzania na Tanzania baadaye ?
 
Leo ni siku ya pili our Commander in Chief ana behave kama Bush wakati wa Katrina

hajakanyanga kwenye eneo ya janga la kitaifa

says alot about this man and his priorities init?
 
mererani.jpg
Relatives wait yesterday on the hill top where miners are still trapped underground after floods swept through pits in Mererani, Manyara Region, the only place where the blue gemstone tanzanite is found in in the world.
 
Leo ni siku ya pili our Commander in Chief ana behave kama Bush wakati wa Katrina

hajakanyanga kwenye eneo ya janga la kitaifa

says alot about this man and his priorities init?

I think this issue is more critical than the Tabata "Dampo" saga and I expect opposition leaders to rush there to offer material and psychological assistance that maybe needed. It is about showing leadership and so far the government leaders have failed!.
 
I think this issue is more critical than the Tabata "Dampo" saga and I expect opposition leaders to rush there to offer material and psychological assistance that maybe needed. It is about showing leadership and so far the government leaders have failed!.

Nina habari kwamba Zitto wa first to the scene.Sina uhakika lakini Marmo kaenda juzi na alikuwa so relaxed .JK na CCM walikuwa anakula na kusaza Butiama.Jamani watu kufukiwa ni issue kubwa sana nimeshangaa mno treatment waliyo pewa hawa victim sijaelewa ni kwa nini ama what sort of message is being sent .
 
Nina habari kwamba Zitto wa first to the scene.Sina uhakika lakini Marmo kaenda juzi na alikuwa so relaxed .JK na CCM walikuwa anakula na kusaza Butiama.Jamani watu kufukiwa ni issue kubwa sana nimeshangaa mno treatment waliyo pewa hawa victim sijaelewa ni kwa nini ama what sort of message is being sent .

Tatizo ni kuwa hii imekuwa ndiyo kawaida. Tutalia na kulalama pale yanapotokea lakini kesho ni kama kazi! Maisha yetu hayana thamani kwa jamii nzima na sio viongozi peke yake. Tumejifunza nini kutokana na ajali za maboti kuzama, treni kuanguka na kila kukicha hizi za mabasi! Hamna kitakachobadilika. Wenye machimbo wataendelea kudunda bila kuwekeza kwenye usalama wa wachimbaji na vijana wataendelea kujitosa humo mpaka ajali nyingine kama hii itakapotokea. Hatuogopi ukimwi tutaogopa hili?
 
Tatizo ni kuwa hii imekuwa ndiyo kawaida. Tutalia na kulalama pale yanapotokea lakini kesho ni kama kazi! Maisha yetu hayana thamani kwa jamii nzima na sio viongozi peke yake. Tumejifunza nini kutokana na ajali za maboti kuzama, treni kuanguka na kila kukicha hizi za mabasi! Hamna kitakachobadilika. Wenye machimbo wataendelea kudunda bila kuwekeza kwenye usalama wa wachimbaji na vijana wataendelea kujitosa humo mpaka ajali nyingine kama hii itakapotokea. Hatuogopi ukimwi tutaogopa hili?

ONce agaian I am not happy at all na jinsi JK alivoamua kuweka kikao cha CCM mbele ya janga la kitaifa kama hili

In short I dont have a COMMANDER IN CHIEF
 
Jana jioni Rais Kikwete alipata nafasi ya kutembelea eneo la Mererani ambapo wachimbaji wadogo karibu sabini wanahofiwa kufa baada ya mashimo ya madini ya Tanzanite kugubikwa na maji. Katika salamu zake za Pole Rais alisema mambo kadhaa akiwapa pole.

Hata hivyo lililonigusa ni lile la kusema kuwa "tumekuja hapa kutafuta chochote, lakini hatukutegemea haya, sisi tunapanga na Mungu anapanga".. Kwa kadiri nilivyomuelewa ni kuwa yaliyotokea Mererani ni kazi ya Mungu na aliahidi kuwa baada ya uchunguzi na utafiti wa kina basi machimbo hayo yatafunguliwa mara moja. Tamko hilo lilipokelewa kwa makofi na wanaapolo.

Je, yaliyotokea Mererani yangeweza kuepukika au tukubali kuwa ni kazi ya Mungu kama yaliyotokea MV. Bukoba, Ajali ya Treni Dodoma, Ajali ya Basi Singida, vifo vya watu Dar sababu ya mafuriko n.k ? Tukubali kuwa ni kazi ya Mungu "haina makosa"?
 
Game, Rais Kikwete alikuwa Simanjiro jana Jumatatu jioni na alitoa pole zake na kuelezea kuwa hiyo ni kazi ya Mungu na kuwa "Sisi tunapanga na Mungu anapanga" na akaagiza misaada katika kuokoa au kuopoa miili. Binafsi kilichonisikitisha ni kuwa katika kuzungumza kwao na wananchi J'pili Kamati Kuu ilishindwa hata kutoa tamko la pamoja la rambirambi au pole kwani walikuwa wanafikiria kitu kimoja tu ili kukilinda na kukienzi...
 
Back
Top Bottom