niwaellyester1
Senior Member
- Sep 7, 2010
- 123
- 22
Zantel walipoanza na service yao ya 2GB kwa wiki kwa 10,000/- ilikuwa poa sana (2.4 - 3.0Mbps) na mimi nilikuwa mteja wao wa kudumu, nikawa naweza angalia mpaka premier league online. Sasa wamepata wateja wengi sana badala ya kuongeza bandwidth, wakaacha the same, wote tunashare humo humo, hata 512 KBps haifiki ukipima (Speedtest.net - The Global Broadband Speed Test). Nimewamwaga, natumia VODA, nikiweka 10,000/- napata 400MB (60MB kwa siku),
much better kuliko hiyo ya 2GB ya Zantel, ambayo
kutokana na speed yao ilivyo ndogo najikuta natumia
maximum ya 500MB kwa wiki (25%)
Kati ya makampuni haya ni wepi wenye huduma rahisi ya mawasiliano ya internet na ya uhakika?
Nataka kuunganisha compyuta yangu na intanet, lakini matangazo yao ya biashara yananitia wazimu.
Duuh niponjia panda natumia voda nikiwa mikoani na sasatel Dar,
Voda kimeo, sasatel angalau,
nataka nijaribu ttcl broadband naona wengi wanaipigia chapuo, sijui imekaaje ktk kujiunga
vipi gharama zao za connection, namaanisha gharama za kuvuta waya hadi nyumbani na kuunganisha kwa pc? kama nipo jirani na nguzo zaoUkweli ni kwamba TTCL Broadband ni nzuri sana kutokana na kasi yake. However, ili kujiunga:
-Ni lazima uwe na laini ya simu ya mezani
-Na simu za mezani hazijafika kwenye maeneo mengi mapya ya jiji kwa hiyo ni kama kichekesho kwamba Ukifika Mbezi Mwisho na kuendelea mbele hakuna TTCL ya simu za mezani na kwa maana hiyo huwezi kupata Broadband Internet. This is very Funny seeing how this is the Capital City of TZ!
-Lakini pia hata ukiwa na laini ya simu ni lazima uwe within 500 metres kutoka Exchange yao ili uweze kupata Internet. (Hili la metres naomba liwe kwenye mabano hadi nitakapohakikisha vema huo umbali)
-Hii maana yake ni kwamba unaweza kuwa na laini ya simu pale Kimara ama Mbezi Mwisho lakini kama iko umbali wa zaidi ya Metres 500 huwezi kupata Internet.
-Naamini kuna wengine wenye kufahamu zaidi watachangia katika hili....
Jaribu Zain (Airtel) ama Voda (mahali inapopatikana 3G). Kama 400MB kwa mwezi zinakutosha, basi Airtel wanakufaa, wanatoa hizo 400MB kwa mwezi kwa 2500/-.zantel wapo slow sana kwa speed
Kuna site nyingi, jaribu kwanza ATDHE.Net - Watch Free Live Sports TV lakini kama una slow connection kama ya Zantel hutainjoiNawezaje kuangalia ligi ya Uk?
Speed ikoje?,
Modem zao zauzwa @ 70,000/= na zinakuwa na 3-GB
Wanajamii,
Mimi ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hizi za simu na nina uelewa mpana wa hizi huduma na zitolewavyo.
Kampuni kama TIGO imechelewa sana kuwa na modem zake based on internet services ila tayari wameshaweka sokoni na zinapatikana, nilibahatika kupita na kukutana na mtaalamu mmoja wa tigo katika moja ya vituo vyao vya huduma na kukuta modem zikiuzwa @ 70,000/= ambapo packages zao za internet ni kama ifuatavyo:
BB7(1-week) ni tsh:10,000/=
BB30 (1- month) ni tsh: 20,000/=
BB90 (3-months) ni tsh: 80,000/=
BB180 (6-months) ni tsh: 150,000/=
NADHANI HAWA JAMAA WA TIGO TAYARI WANAZO REASONABLE PRICES UKILINGANISHA NA NETWORKS ZINGINE NA NIMEIJARIBU IKO so friendly in using.
Ikumbukwe kwamba SASATEL are highly based on providing internet services ikiwa ndio kama their business heart na wame-invest a lot katika huduma hizi na ndio maana huwezi kuwaona wakiwa katika competitive promos kama wengine wafanyavyo, sijui hawa wapya AIRTEL wataingiaje sokoni kwa hivi sasa kama ilivyo kwa VODAFONE tangu walipochukua hatamu...lets see!!