Zainab Katimba: Serikali Itaendelea Kukarabati Shule Kongwa

Zainab Katimba: Serikali Itaendelea Kukarabati Shule Kongwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. KATIMBA - SERIKALI ITAENDELEA KUKARABATI SHULE KONGWE

Serikali imeendelea kutenga fedha za ukarabati wa shule chakavu nchini zikiwemo shule za msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi kadri ya upatikanaji wa fedha.

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anyeshughulikia Elimu, Mhe. Zainab Katimba wakati akijibu swali la Mhe. Vicent Mbogo ,mbunge wa jimbo la Nkasi Kusini aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhusu ukarabati wa Shule za Msingi katika Vijiji vya Kalundi, Lyapinda na Londokazi vilivyopo katika jimbo hilo.

Akijibu swali hilo, Mhe. Katimba amsema “kuanzia mwaka 2022/23 hadi 2023/24, Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ukarabati, ambapo shilingi bilioni 70.39 zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule 793 zikiwemo Shule za Msingi Chalantai, Nkundi na Sintali za Jimbo la Nkasi Kusini” amesema.

Aidha, Mhe. Katimba amesema serikali katika mwaka wa fedha 2024/25 imetenga fedha kwaajili ya ukarabati wa shule kongwe na chakavu hatua inayoendelea ni kutathimini na itakapokamilika serikali itaweka kipaumbele kwenye shule yenye miundombinu chakavu.
GbR5DVuX0AA2Iap.jpg
GbR5DVWXoAAQuo6.jpg
GbR5DV5WkAAqzcU.jpg
 
Back
Top Bottom