Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Naibu Waziri OFISI YA RAIS TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha inarejesha mawasiliano katika maeneo ambayo miundombinu ya barabara imekatika kutokana na athari za mvua hasa katika barabara za wilaya ili kuhakikisha barabara hizo zinapitika.
Mhe. Katima amesema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha masalı na majibu takati akijibu swali la nyongeza la Mhe. Dkt. Florence George Samizi, mbunge wa jimbo la Muhambwe alitaka kujua lini serikali itapeleka fedha za dharura kwaajili ya ukarabati wa barabara na madaraja katika jimbo hilo lililopo katika wilaya ya Kibondo.
“Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi Milioni 105 kwaajili ya kufanya jitihada za kidharura katika jimbo la Muhambwe na fedha hizo zinakwenda kujenga Boksi Kalavati na kufanya marekebisho maeneo yaliyopata athari kubwa ya mvua” amesema Mhe. Katimba
Aidha, Mhe. Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 3.3 kwaajili ya ujenzi na matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 110 na ujenzi wa karavati 32 katika wilaya ya Kibondo mkoa wa Kigoma.