Zama hizi za Internet, serikali kuminya uhuru wa taarifa ni kujidanganya

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kwa mujibu wa Taarifa za TCRA ambazo zimenukuliwa katika mtandao maarufu wa Wikipaedia, idadi ya Watanzania wenye kumiliki vyombo vya mawasilaino kwa maana ya Simu ni milioni 43.5 kati ya wananchi milioni 53.8

Hii inamaanisha kuwa takriban asilimia 80.8 ya wananchi wanaweza kupashana habari na kuwasiliana kupitia simu.
Wakati huo huo Wananchi wenye kuaccess Internet ni milion 22.3 sawa na asilimia 41.4 ya wananchi wote

Kwa hiyo hii inamaanisha kuwa wananchi wanao uwezo wa kupata taarifa za ndani ya nchi na nje ya nchi kupitia mtandao hata kama serikali inabana magazeti na television

Hii inakuonyesha kwa nini Rais Magufuli amewahi kutoa kauli ya kutamani malaika washuke wafungie mitandao. Hata hivyo pamoja na kuleta sheria za mitandao na kujaribu kabana content zitolewazo mitandaoni bado wananchi wanaweza kupata access ya taarifa mbadala

Kwa hiyo CCM na serikali yake wasijidanganye kuwa wanaweza kubana Taarifa au kueneza propaganda kiasi kwamba wakaweza kuwadanaganya watanzania muda wote

Cha msingi ni kwamba Wapinzani waandae strategy na wawekeze katika internet na mitandao ya kijamii, itawasaidia sana kufikisha ajenda zao kwa umma

Kwa taarifa zaidi juu ya hali ya matumizi ya Internet nchini unaweza kuipata hapa:

List of mobile network operators in Tanzania - Wikipedia.

Tanzania internet users hit 23 million; 82 percent go online via phones: regulator
 
..serikali inatakiwa ipanue, na ipanue kwelikweli.

..kwasababu wakibinya kidogo tu, kidooogo tu, wanakuwa wamewapa point wapinzani.
 
Hakuna chama cha upinzani ambacho kimejiandaa kuunda serikali coz kushinda uchaguzi vyama vya upinzani hasa kwa nchi za Africa ni mchakato mrefu na mipango ya muda mrefu kitu ambacho hakuna chama cha upinzani Tanzania wameshafanya hata robo nadhani wao wanagombania kuwa ni chama gani kitakuwa chama kikuu cha upinzani

"Wananchi wenye kuaccess Internet ni milion 22.3 sawa na asilimia 41.4 ya wananchi wote " Hahahaaaa ulishajiuliza Tanzania ni mambo gani au vitu gani vinafatiliwa au kugoogle sana kwenye Internet utashangaa sana nikwambie kitu watanzania hawafatilii siasa kwenye mitandao ni asilimia chache sana hata ukifanya utafiti utagundua ni Twitter tu ndo wanafatilia siasa but sehemu au mitandao mingine nadhani unajua nn kinafatiliwa sasa jiulize Twitter ni watanzania wangapi wana account huko??

Tanzania bado main stream media(TV,Magazeti,Radio) bado zinanguvu sana na bado zinafatiliwa na watu wengi kwa sababu kupata taarifa huko ni free au cheap kulinganisha na mitandaoni ambapo lazima uwe na bando kitu ambacho mtu wa mikoani hawezi kununua GB 4 eti kumuangalia Tundu Lissu akiutubia You tube nazungumzia nchi kwa ujumla si mijini tu CCM si wajinga kuwabana huko wanajua nini wanafanya hapa ungewashauri wafungue vyombo vyao vya habari kama Radio na TV ambazo watakuwa na mamlaka navyo hata kwa wenzetu ambapo Dunia imeamka bado TV ,Magazeti na Radio zina nafasi kubwa sana ktk Ulingo wa kupashana habari pia kwa mfumo uliopo ni mpumbavu pekee anayeweza kusema Lissu au upinzani utachukua nchi ktk miaka hiii 10 au 15 ijayo bado sana .
 
Umeongea vyema. Lakini swali langu, kwanini kila siku mnayalilia magazeti, redio na televisheni hazitangazi habari zenu?


TUKUTANE OKTOBA 28!
 
Uchaguzi wa mwaka huu, kampeni kubwa zitafanywa mitandaoni

Mkuu wazo lako kwenye post namba moja ni zuri sana. Ila sio wananchi 43m ndio wanamiliki simu, bali line za simu zinafika idadi hiyo. Watanzania tuko karibu 60m, ina maana kama watu 43m wangekuwa wanamiliki simu, hiyo ni kusema kila watu watatu, wawili wanamiliki simu jambo ambalo si kweli. Wangalau ukisema watu karibia wote wenye umri wa kupiga kura wanamiliki simu, bila kujali ni smart phones au vile vitochi vya game la nyoka. Ni kweli wapinzani wanaweza sana kutumia mitandao kufikia watu wengi, maana kwenye mitandao watu wanapata watakacho, na sio wanacholishwa na watawala. Hapa ni juu ya kujipanga maana wangalau ndio njia ili wazi kwa sasa.
 
Mitandaoni ukiacha jf wapinzani wameshapigwa

Kinawashinda nini hao washindi wa kwenye hiyo mitandao mingine kuja kushinda na hapa jf? Kimsingi hoja zilizoko humu mitandaoni sio za kusaka mshindi, bali ni eneo lenye uhuru wa kutoa hoja za ukweli, maana platform nyingine zimeshatishwa kuongea ukweli. Kama mmejaza watu wa kuja kusaka ushindi mtaishia kutukana na hoja za kichovu, huku ukweli ukibaki kama ulivyo.

Mfano halisi miaka hii mitano mmekuwa mkijilisha upepo kuwa upinzani umekufa, kisa mlitumia watu wasiojulikana, kuua, siasa chafu zote, kununua wapinzani, kunajisi chaguzi zote ili ionekane mnakubalika sana. Matokeo yake saa hii mmepanick kwa kile mnachokiona maana ukweli hata ufanye hila vipi, ukweli hubakia hivyo hivyo.
 

Huko youtube na facebook wamejaza jeshi la mtandaoni la vijana la kutukana na kukejeli wapinzani huku wakisifu sana ishu za Magufuli na serikali. Lengo ni kushape public opinion.

Hata hivyo waliowengi wenye kuipinga serikali hawathubutu kucomment huko kwa sababu ID zinakuwa wazi, watu wanaogopa usalama wao!
 

Huyu jamaa ndio kila mara utasikia nenda kule facebook ukaone maoni ya wananchi. Anadhani sijui tuna upeo mdogo kiasi hatujui nini kinaendelea kwa hili kundi lililomwaga huku mitandaoni. Nakumbuka kuna wakati akina Nape na Kinana kwenye mwaka 2012-2013 nao waliamua kuingiza vijana mitandaoni kwa kile kilichoitwa kujibu mapigo. Walipokuja hawakuwa na hoja bali kumwaga matusi mazito mazito, na kuvuruga mijadala kwa kuprovoke watu. Ila bado walichemka baada ya muda mfupi, maana watu wako stable kwenye hoja.
 
Kwa jinsi mnavyojadiliana mmenikumbusha hadithi ya "Mkutano wa Panya" wa namna ya kumfunga paka kengele. Ahahahahahahahahah!


TUKUTANE OKTOBA 28!
 
Kwa jinsi mnavyojadiliana mmenikumbusha hadithi ya "Mkutano wa Panya" wa namna ya kumfunga paka kengele. Ahahahahahahahahah!


TUKUTANE OKTOBA 28!

Hili ni jukwaa huru, na maoni yanajadiliwa wazi peupe maana sio mawazo ya wachawi.
 

Huku JF hawapawezi kwa sababu watu wanatumia ID zilizojificha kwa hiyo wakileta ujinga wao wanajibiwa kwa nguvu zote bila hofu.
Ila kule kwenye ID halisi, wenye kuipinga serikali na Magufuli wanaishia kusoma comment tu na kusepa zao, hawacomment kwa sababu ya nongwa ya serikali hii kuweka watu ndani kwa comment za mitandaoni wasizozipenda!
 

Mojawapo ya sifa za utawala usiokubalika na wengi (dikteta) ni kuminya vyombo vya habari.

Kwa hofu waliyo nayo CCM na Magufuli wao, sitashangaa wakiamrisha internet izimwe nchi nzima!

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…