Zama hizi za Internet, serikali kuminya uhuru wa taarifa ni kujidanganya

Wameshindwa nini kuwajaza na hapa jf?
 
Inasemekana Lissu ataruhusu tena kupata watanzania kupata habari kwa wakati iwapo atashinda
 
Umeongea vyema. Lakini swali langu, kwanini kila siku mnayalilia magazeti, redio na televisheni hazitangazi habari zenu?


TUKUTANE OKTOBA 28!
Una taarifa kwamba,huko Namtumbo mkoani Ruvuma vijana wa CDM walitaka kumkafini ndugu yenu aliyempora mgombea wa CDM fomu za udiwani akiwa ametumwa na mwenyekiti wenu wa UVCCM???

Bado kidogo mtaanza kutuelewa
 
Wameshindwa nini kuwajaza na hapa jf?
Hapa JF wanakutana na watu wenye hidden ID's wanawajibu bila kuhofia kupotezwa ndiyo maana kila wakijaribu hapa JF wanafeli.
Kule kwingine watu wanawaacha tu maana wanahofia usalama wao kutokana na IDs zao kuwa wazi
 
Internet nayo itafungwa mpaka baaada ya uchaguzi
Then wataendeshaje shughuli za serikali ikiwemo makusanyo ya mapato mfano control number,
Mzungu ana akili Sana kuleta control namba afrika
 
Tv- ni kuona na kusikia
Radio- ni kusikia zaidi
Mitandao ya kijamii - utafute habari uisome

Sasa utaona huku kwetu tv na radio vinagusa watu wote.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuja wanaukimbiza upepo, niwashauri upinzani waongee na tv binafsi za Kenya wanunue airtime ziwarushie matangazo yao live stream au recorded mfano citizen hizi zipo kwenye decoder zote hii itasaidia watz wengi kupata taarifa za mikutano yao pasipo haja ya citizen kulazimika kuja nchini kuripoti.
Hawa wakuja wenye mawazo ya kijima watatushinda vipi akili, hawana uwezo wa kuzibiti habari zisisambae, yaani wadhibiti Bluetooth, flash, cd na nk. Wao wabakie na media zao sie twende na za nje
 
Mojawapo ya sifa za utawala usiokubalika na wengi (dikteta) ni kuminya vyombo vya habari.

Kwa hofu waliyo nayo CCM na Magufuli wao, sitashangaa wakiamrisha internet izimwe nchi nzima!

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza...
Haisaidii kitu tutatumia Bluetooth,flash,cd, VPN,pia hicho kitu cha kuzima internet hawawezi means watakusanyaje mapato kupitia control number, hawawezi media control Hawa wakuja.
Wanavuna walichopanda anga limeshawakataa
 
Nimeongea sana hili suala uliloandika hapa.
Watu wenye kufanya kampeni au wenye mahaba au wasiojielewa watakupinga hadharani au watakutukana kabisa lakini huu ndiyo ukweli wa mambo.

Wasubirie October 28, 2020 wataona uhalisia labda beberu atie mkono wake kama sehemu zingine walikotia mkono na kupi ndua meza kibabe.
Lissu au Membe labda watasaidia tu kuokoa viti angalau vitatu au vinne vilivyokuwa viende kwa CCM ndani ya bunge.
 
Why mpo bize kuuwa upinzani,plus sheria kandamizi kila siku.
Habari zitawafikia tu watu,sio kila mtz ana mawazo ya kijima,zitatumika hata tv za nje iwe live au recorded na sio lzm waje nchini watatumiwa habari watarusha je mtazuia na decoder zote, mtazuia Bluetooth,cd,flash nk.
Kuzuia habari Ni sawa na kuzuia upepo usisambae.
Hotuba yote ya Lisu ipo citizen Kenya vipi mtazuia na media za nje zisiripoti wakiwa kwao pasipolazimika waje nchini kuchukua habari,
 
Mkuu unapozungumzia Ushindi wa uchaguzi si ushindi wa kubet au ushindi wa Yanga na Simba uchaguzi ushindi wake unaamua maslai mapana na muelekeo wa nchi ktk kipindi cha miaka 5 pia unatakiwa kujua kuna wakt Democrasia inaweza kuzuiwa nikupe mfano tu kuwa waandamanaji walipigwa tena mbele ya Ikulu ya Rais wa US ambae wote tunaamini ni Baba wa haki za binadamu na Democrasia unajua walipigiwa nini ?

Wamepigwa kisa Donald Trump apate kupita kwenda kupiga Picha mbele ya kanisa huku ameshika bible
 
Demokrasia Ina mipaka yake sio kila kitu ni huru lkn huwezi wanyima wengi haki kwa maaslai ya wachache
 
Ccm Ni chama Cha zamani, nyakati hizi lazima kipate wakati mgumu kukabili hoja kinzani. Wao wanaishi miaka ya nyerere Kule, wananchi wanaishi miaka ya kidigitali. Sishangai ccm na serikali yake kuhangaika na redio na TV Yani hawajui kabisa hivyo vyombo kwa Sasa Dunia inaviacha na walimwengu(watanzania) sio wale wa 1960s
 
Hawana ujanja huo sababu awazimiliki media,hizi ni zama za dotcom sio zama za zidumu fikra za mwalimu hichi ni kizazi huru.
Tuliwaonya ccm msizuie wapinzani kufanya siasa hawakusikia wao wametamba miaka mitano pekee yao,leo wananchi wanataka wasikie wapinzani watasema nini,wanawazuia.Ccm hawna jipya la kuongea kwa wananchi yoote washaongea kwa miaka 5 ZAIDI YATAKUWA NI MARUDIO TU nayo ni mabeberu,sgr,ndege,flyover,stiglers kipi kipya wanacho zaidi ya hivo.Huku wapinzani wanazvyo zaidi ya 70 vya kuongea
 
CCM hawana Jipya, ni marudio tu ya SGR, Ndege, Stieglers

Wananchi wameyachoka hayo wanataka kusikia upande wa pili wa shilingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…