Agrey998
JF-Expert Member
- Jul 8, 2019
- 417
- 550
Tulikuwa na zama za mawe zikaja zama za chuma zikaja zama za viwanda na sasa tupo kwenye zama za taarifa (information age) uchumi unamilikiwa na Watoa taarifa na watu wenye teknolojia kubwa zaidi. Haishangazi kuona matajiri wakubwa duniani wamewekeza katika teknolojia.
Kwa Afrika naona teknolojia inakuwa japo bado katika utegemezi mkubwa wa teknolojia ya nje , kwa nchi kama Uganda na Rwanda wanatengeneza vifaa vyao wenyewe vya mawasiliano, kwa Afrika kusini viwanda vya utengenezaji wa magari navyo ni kama makao yake ni pale Toyota ,nissan na makampuni makubwa ya magari yana vituo vya utengenezaji magari pale Afrika kusini.
Kenya na nchi za magharibi mwa Afrika ambazo ni Ghana na Nigeria wamepata fursa ya kukaribisha uwekezaji mkubwa wa makampuni makubwa ya teknolojia kama facebook, Google na twitter ambao watafungua makao makuu yao Ghana mwishoni mwa mwaka huu.
Faida zao ni nyingi katika swala la kuongeza ajira, kuongeza ubunifu na kurahisisha maisha . Na wazi kwamba miaka ya mbele matajiri wengi wa Afrika watatokea katika sekta ya teknolojia kwani hata watumiaji ni wengi kitu kinachorahisisha zaidi soko lake.
Nitoe rai kwa serikali na wananchi kuwa tujikite zaidi katika mabadiliko makubwa ya teknolojia yanayofanywa katika nyanja zote zinazogusa maisha ya watu. Elimu itolewe vyuoni kufundisha zaidi juu ya teknolojia kubwa za dunia ya sasa itakuwa haina maana mtu Kusoma namna ya kuoperate mashine za kutuma telegram miaka hii wakati hakuna mtu anaetumia telegram miaka hii.
Wapo vijana wanaojituma katika kuonyesha ubunifu wao na kutumia kile walichojaliwa, wawekezaji wakubwa na serikali wakiwaamini huenda wakatutoa sehemu moja hadi nyingine, Tuamini watu wetu tumewasomesha kwa gharama kubwa na kama wameonesha chochote kinachohitaji misaada wasaidiwe.
Katika soko hili ushindani ni mkubwa , uhitaji ni mkubwa na pia utajiri ni mkubwa zaidi hii itatusaidia kama Taifa na hata raia mfano mzuri ni nchi za mashariki ya mbali yan far east walivyo adapt kitu kinaitwa tiger economy wamefanya mapinduzi makubwa kiuchumi kwa kuwekeza sana kwenye teknolojia.
Nawasilisha.