Zama za Magufuli wanasiasa wanaume wamebaki CHADEMA

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
ZAMA ZA MAGUFULI NI RAHISI KUWAJUA WANAUME NA WANAWAKE!

NA Luqman Maloto

KUNA "male" yenye kumaanisha jinsia ya kiume na "man" ambayo maana yake ni mwanaume. Kuna "female" yaani mwenye jinsi ya kike na "woman", mwanamke. Awamu ya President Magufuli ni rahisi sana kuijua tofauti kati ya wenye jinsi ya kiume (males) na wanaume (men), kisha females na women.

Enzi za Jakaya, mtu fulani mpenda maridhiano, angeweza kukung'ata akitabasamu. Mwenye falsafa ya nesi mchoma sindano watoto, anambembeleza mtoto pipi kumbe anamchoma sindano. Mtoto anashituka imo!

Kipindi hicho wanasiasa radical walikuwa wengi. Wanaharakati wa kuikosoa Serikali walikuwa wa kumwaga. Waandishi wa habari za uchunguzi unaoibua madudu ya Serikali waliongezeka, wachambuzi wakosoaji kila chombo na mitandaoni.

Zama hizi za President Magufuli, falsafa kama Juma Nature "weka ugoko niweke jiwe", au Cuf zamani "jino kwa jino", wanasiasa radical wametoweka, wengi ni waunga juhudi. Wanaharakati wamekuwa adimu, siku hizi kuna wanaharakati watetezi wa Rais. Waandishi wakosoaji nao ni adimu.

Dhahiri, kipindi cha Jakaya kwa sababu ya uhuru mkubwa, hata wavulana walikosoa, wasichana pia walipaza sauti. Kipindi hiki, inahitaji kuwa mwanaume au mwanamke kweli ili ukosoe na uwe mwanaharakati.
Inahitaji uanaume kuwa mwanaume na uanamke kuwa mwanamke. Uanaume ni kuwa thabiti kimsimamo, kimatendo na kauli. Sio leo kitisho kidogo unakwenda kupiga magoti. Kuomba radhi ni tendo jema kama ni la ridhaa na kukiri makosa, sio huna kosa lakini unaungama kwa woga. Dude, you're not a man, you're just a male!

Ndio maana zama hizi za Magufuli imekuwa rahisi kumtambua Prof Mussa Assad kuwa ni mwanaume. Yes, Assad is a man. Tundu Lissu, ooh! He's a man. Uzuri kila mtu anajua kuwa Lissu ni mwanaume. Hata wasiompenda wanajua. Na wanakiri kimyakimya.

Bernard Membe, aisee jamaa mwanaume, tena na nusu. Mbishi sana halafu hayumbi. Utadhani alizaliwa Maweni, Kigoma.

Freeman Mbowe, loh! Mali zake nyingi zimepotea. Yumo tu! Anasalitiwa na waunga juhudi, bado imara. Mbowe is a man, really a man!

Zitto Kabwe, hakuna wakati amejipambanua kuwa radical kama sasa. Hata wote wakiona maziwa, kama yeye kaona ni tui la nazi atasema. Atakejeliwa, yeye yumo! Zitto is a man.
John Heche na Boniface Jacob, wale majanki ni wanaume. Katika hamahama ya kutoka CCM kwenda upinzani kwa mkumbo wa Lowassa, mwanaume aliyebaki ni Milton Mahanga. Wengine wapo wapi? Nionesheni!

Basi bwana, zamani nilimchukulia poa Lazaro Nyalandu. Kumbe Nyalandu is a man. Aliacha ubunge awe mwanaharakati. Nani anaweza? Maalim Seif hajawahi kuwa mvulana kwenye siasa. Alikuwa mwanaume wakati wa Mwalimu Nyerere, ni mwanaume hata sasa.

Halima Mdee is a woman. Tena handsome woman. Usimwite beautiful woman. Halima sio mdada madeko. Mahabusu kama picnic, halafu yupo tu.

Fatma Karume ni mwanamke sana. Naye ni handsome woman. Mtoto wa Rais, mjukuu wa Rais, alizaliwa na kijiko cha fedha mdomoni, lakini attitude za kiharakati kama alichangia wodi na Bibi Titi.
Maria Sarungi ni mwanamke. Mtoto wa kigogo, amesoma na kuishi nje lakini utadhani alikulia Rorya. Labda asili inambeba.
Esther Matiko ni mwanamke sana. Inawezekana ni matunda ya kulishwa kichuri! Unaulizia Mama Bisimba? Hajawahi kuwa msichana. Ni mwanamke kila siku.

Genius Masoud Kipanya ni mwanaume sana. Tangu wakati huo mpaka sasa. Bila woga, katika point kila siku.

Sugu wa kwenye muziki mpaka siasa, ni yuleyule, ameendelea kuwa mwanaume. Jela na kutoka. Bado kwenye point. Sikosei hata kidogo nikisema Peter Msigwa ni mwanaume.
Godbless Lema hajawahi kuwa mvulana. Kama ambavyo Jenerali Ulimwengu amebaki mwanaume tangu enzi za Ben Mkapa mpaka leo.

Unajua hata yule Mdude wa Chadema ni mwanaume. Godlisten Malisa ni mwanaume. Ado Shaibu. Bob Chacha Wangwe. Ni majanki wadogo lakini wamevuka uvulana kwa ujasiri.

Mansour Himid, Juma Duni, Jussa Ismail, Nassor Mazrui ni wanaume. Nawe ongeza wa kwako ambao unaona kuwa katika zama hizi wavulana na wasichana wamekuwa wengi, angalau wanaume na wanawake wa kweli wanajipambanua. Wanajisimamia, wanajiheshimu, hawayumbi kijinga.

Ndimi Luqman MALOTO
 
We jamaa hujielewi, umetoka kubandika bandiko lenye extremely tribalism, ukidai hakuna mfungwa hata mmoja Kutoka Kilimanjaro ameachiwa kwa msamaha wa Raisi....
 
Kanywe ulanzi ndio urudi hapa, mimi naandika kilichopo kwenye jamii, endelea KUANGALIA TBC TAIFA, UKWELI NA UHAKIKA
 
Kwa taarifa hao unaowasema ni wanaume bado pia ungewaunga na wale unaowabeza, kabla ya lisu kusema haji mpaka ahakikishiwe ulinzi alisema, haogopi mtu na akiruhusiwa tu atakanyaga ardhi ya tanzania, mpaka wengine mkasema kitanuka, mara atarindwa na UN saaa mbona nae kawa muoga kama unaowasemea? Akanyage mwamba aache uoga, kumbuka juzi jamaa kubwa lao kaenda kutafuta maridhiano ya kitaifa, wanasema kama huwezi kupambana nae ungana nae, sasa jamaa anataka kuungana nae, hao walio chini yake wataitwaje male, au man?
 
Lissu hajawa mwoga, anamsoma JIWE
 
Mwaka huu usipopandishwa ,,class” Uchagani basi tena kwa maana siyo kwa jitihada hizo.
Hakuna kiti kibaya kama kuzaliwa low class kwenye jamii inayopractice caste system.
 
We jamaa, mawazo na maoni yako ya kihaini sana. Una roho ya mvuruga amani na mjenga chuki
 
Angalia mubashara kwenye T.v. Rais wetu mpendwa Magufuli anawaongoza Watanzania kupokea dege jingine

Awamu inayoacha alama

Tafuta habari Rais Magufuli sio wa kwanza kupokea ndege

Huko duniani ni kawaida tu
Hebu nisaidie, nasikia kuna watu wanapokea ndege huko Mwanza, mimi sijaelewa ndege huwa inapokewaje?

Si vibaya ukitujuza tumelipa dollar ngapi mpaka ndege kukubaliwa iondoke kuja Tanzania? Na deni limebaki kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom