Ile pesa tuma kwa namba hii 07!!22!!21, jina litakuja ZAMA ZIMEBADILIKA, usitumie tena ile ya zamani,hii ni karne ya 21,Mama anashukuru sana kwa hela uliyomtumia mwezi jana ilimsaidia sana kwenye shughuli za kilimo pamoja na mdogo wako katika mahitaji yake ya shule. Zama zimebadilika sana, lazima tujue kutofautisha kupiga au kupigwa, biashara za mtandaoni au utapeli vijana tuache ushamba, biashara mtandao ni fursa tusiichafue kwa utapeli, tujenge maisha kwa kuitumia kihalali.
Haya haya kumekucha! kumekucha! wakusoma ni muda wa kuwahi shule, wakulima shamba, wa mjini kuwahi ofisini wafanyabiashara vivyo hivyo, biashara asubuhi jioni mahesabu, ila tusiishi kwa kukariri nyakati zimebadilika sana, ukiacha walinzi, wanaokesha sikuhizi ni wengi, sio tu matabibu wanaofanya kazi kwa kupokezana ila ni wengi tu tunaopambana mchana na Usiku kulijenga Taifa hili ambalo wachache wasiofaa wanaendelea kulibomoa. Zama zimebadilika sana, siku hizi tunatoka kazini kuelekea kazini, ofisi sio majengo tena, tunatembea na ofisi zetu tunalala na ofisi zetu, hatusinzii, tunapumzika tu vitandani huku vidole na ubongo vinaendelea kuchapa kazi, tunafumba macho na kuzimuka kuangalia miamala, Taifa linajengwa kwa kasi kubwa sana inayochochewa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni elimu tu ndio imeshika usukani kuongoza watu kuelekea mafanikio yanayotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Zama zimebadilika sana, ni tofauti na enzi zenu babu, mtu akiwa na pesa mnajadili kazipata vipi? Mlitaka kujua anafanya kazi gani, na akijenga na kuendesha magari mlimtenga mkiamini ushirikina au kapata pesa za kishetani, siku hizi hatuna hizo, tunauza na kununua tukiwa tumelala, tunajadili biashara tukiwa tunafanya mazoezi ya viungo tunajenga tukiwa ufukweni kubalizi na tunalima tukiwa sokoni, ni elimu yako tu ya shule au mtaani,urafiki wetu sikuhizi hauishii tu kushirikiana kwenye sherehe au kufarijiana wakati wa matatizo tu, sikuhizi urafiki wetu ni mtandao wa kupeana michongo.
Elimu Elimu Elimu imeleta mapinduzi makubwa sana kuna wakati tutake au tusitake huyu Mzee, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Baba wa Taifa tumpe heshima sana kwa kuwa na maono makubwa kiasi cha kutambua na kuanzisha vita dhidi ya maadui wakubwa watatu, Ujinga,maradhi na Umaskini, najua wazee hawakumwelewa haraka ila kilichofuata ni historia, kama kuna wazee bado hawataki kuwapeleka watoto shule,washtuke zama zimebadilika. Wanaturudisha nyuma sana tumechoka kuelekeza vijana jinsi ya kutumia simujanja.
Wakusoma, onesheni mlichofuata vyuoni Zama zimebadilika sana, sio muda wa kukariri tu kanuni za mning'iniko na kurudi kubweteka mkisubiri ajira, Teknolojia inawapa jukwaa kuonesha ulicho nacho, teknolojia itakukutanisha na waajiri, teknolojia itakukutanisha na wateja, teknolojia itakupa soko ambalo linaweza kukufanya usitake tena kuajiriwa. Umesoma biashara tumia teknolojia kutengeneza soko mtandao, mhandisi njoo na ubunifu wako kwenye mitandao ya kijamii, mwanasheria fungua ukurasa YouTube, toa mafunzo ya sheria, Mwalimu fundisha kwa njia ya mtandao, msanii onesha kazi zako kwa mtandao, fanya sanaa zako mbashara kupitia mitandao ya instagram, Facebook na YouTube Mwanataaluma tukutane LinkedIn na mwandishi njoo jamii forums tuandike nyuzi mbalimbali kuelimisha jamii, tunaajiriwa na watu kutumikia watu na watu wako kwa mitandao.
Zama zimebadilika sana,sikuhizi hatuhitaji kushinda mashambani na kujitesa sana ili kupata mavuno mengi, kilimo sio laana kulima ni zoezi lililotukuka linalowezesha Taifa na watu wake kupata chakula na mazao ya biashara, vijana sasa wanatoka mjini kwenda mashambani tofauti na zamani, watu walilikimbia jembe na kwenda mjini wakidhani kuna maisha ya bwelele.Kilimo sikuhizi ni biashara kubwa, ardhi inazidi kupanda thamani,zamani aliheshimika mtu kwa vitu alivyo navyo mwenye gari alionekana bora kuliko anayemiliki ardhi, sikuhizi ardhi ndiyo kila kitu, amkeni vijana ardhi ni mali tena mali hasa isiyohamishika, ujanja ni kumiliki hati miliki ya ardhi funguo ya gari ni ziada tu, tumiliki ardhi, tuilime na kuitunza yajayo yanafurahisha sana.
Wazazi tusiuze ardhi ovyo tuwafundishe watoto kuilima na kuitunza, hiyo iwe elimu ya awali kabla hatujawapatia elimu ya msingi, wajue kupanda miti na wajue kuyatunza mazingira, shuleni waongezewe elimu zaidi juu ya mazingira, ifike wakati wasomi wapimwe kwa namna wanavyoithamini ardhi na kuyatunza mazingira yao, vijana zama zimebadilika, kilimo sio ushamba, unaweza lima wakati wowote ukiwa popote, mjini au kijijini, unaweza ukawa instagram mbashara na baada ya hapo ukafuatilia maendeleo ya mashamba yako au masoko kwa ajili ya mazao, Tanzania ni kubwa mno, na mabonde ni mengi yanayofaa kwa uwekezaji katika kilimo, walioko Mbeya, Morogoro, Katavi, Kagera na mikoa mingine ambayo sikuitaja watakuwa mashahidi kwa hili.nasisitiza tena kilimo sio laana wala sio ushamba na sio lazima uwe kijijini kuitwa mkulima.
Tuache ushamba mitandaoni,ukimiliki kundi la whatsapp, telegram au ukiwa na wafuasi wengi kwa ukurasa wako Facebook,Twitter,Instagram,tiktok au YouTube ni fursa hiyo, usiitumie kusambaza mambo yanayoharibu au kukiuka maadili ya jamii, wala usitumie kama sehemu ya kueneza siasa za chuki na visasi, la! Tumia taaluma yako au ujuzi wako kuwabadili hawa wafuasi wako kuwa wateja wa taaluma yako, msusi tangaza bidhaa zako,fundi tengeneza na tangaza nguo,viatu,samani, picha za nyumba ulizowahi kujenga, mkulima tafuta au watafutie wengine soko, dalali unganisha watu kwa urahisi epuka utapeli, msanii nadi kazi zako za sanaa,tafutia watu ajira na mwandishi andika machapisho yatakayoleta tija na msaada kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Zama zimebadilika sana,zamani tulipima muda kwa kutazama jua, na tulipima homa Kwa mikono, lakini mambo ni tofauti sasa usiamue kitu chochote kwa kutazama,kuhisi au kwa mazoea, tupime afya zetu mara kwa mara na tuzingatie kanuni za afya, Taifa linajengwa na watu wenye afya bora kimwili,kiakili na kijamii, tule chakula bora, tulale mahali Salama, tuvae nadhifu na tuwe na muda mwafaka wa kupumzika na kuburudika.
Zama zimebadilika,tusifiche watoto na wenye ulemavu wakati wa zoezi la sensa. sensa sio zoezi la kupuuza,watoto wakihesabiwa hawatapungua wala hakuna uhusiano wowote na ushirikina. Kutokana na Sensa Taifa litakuwa na takwimu sahihi ya watu na nguvu kazi ya Taifa, litafahamu na kufanya mgawanyo mzuri wa rasilimali na majukumu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Zama zimebadilika Sensa ni kwa faida ya jamii na Taifa kwa ujumla.
"JIANDAE KUHESABIWA"
"JIANDAE KUHESABIWA"
Upvote
1