Zamani haikuwa rahisi kupata division three; Kwanini sahivi imekuwa rahisi sana?

Swali zuri sana,nadhani vitu vingi vimebadilika sana ukilinganisha na zamani.

Kwanza siku hizi vitabu vimekuwa vingi sana na maarifa yameongezeka.

Enzi zetu tulikuwa na uhaba mkubwa wa waalimu.Hali ni tofauti sasa kuna waalimu wengi tena wengine hawana kazi.

Elimu ya msingi imeboreshwa sana tena EM zimekuwa nyingi si kama zamani zilikuwa chache sana.

Tuliosoma zamani utakuta tunategemea 100% notice za Mwl siku hizi Watoto wana vitabu na wana uwezo wa kufanya rejea kipitia vitabu mbalimbali.
 
Utunzi wa mitihani si kama wa zamani. Hawa watoto tuko nao ni weupe kichwani. Ni shughuli pevu ukiwaambia wa derive formula to make subject equation. Ukija kwenye kiingereza nako ni shida tupu
 
Subiri waje wakupe ajira kipindi hiki ni utandawazi pambana ku reset Kama hautangukia kibuyu
 
Nimeuliza kipi kimebadilika? Je wamebadilisha kipimio?
Kaka yafaa pia ujue nani anakujibu,kama ni wa 2000 usitegemee jibu zuri,,sikuhizi siasa imeingizwa kwenye elimu pia,hakuna tena maswali fikirishi,lengo namba ya ufaulu iongezeke,shule zisifiwe kuwa zinafaulisha,hili ni janga tusichukulie poa,.ndio maana ubunifu haupo siku hizi,watoto hawaajiriki uko makazini,wanaishia kwenye uchawa!!!,,
Enzi hizo wanafunzi waliitahidi kwa kweli,ingawa leo hii materials yanapatikana kirahisi,mitandao nk,lkn ukitaka kujua vyema ni kwenye utendaji,utakuta ni ziro.
 
Nyie ndio wale Malecture Uchwara wanaojisifu kufelisha. Utasikia mimi mtihani wangu huwezi kupata 90.

Mbona haihitaji akili kubwa kutambua miaka ya resources za kujifunzia zmekua nyingi tofauti na miaka ya nyuma. Shule nyingi, vifaa vingi, walimu wengi nk.. Haikuwa hivi miaka ya nyuma.
 
Kwamba resources zikiwa nyingi unafaulu lakini kichwani hujui kitu hata what is biology hujui, kuandika barua hujui, national flag hujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…