Zamani kuchezea Yanga SC ilikuwa heshima na ufahari

Zamani kuchezea Yanga SC ilikuwa heshima na ufahari

Yanga ya miaka ya 1990'S hadi majuzi ndio ilikuwa bomba,mimi sijui tatizo la yanga kwa sasa hata kama hela hakuna inatakiwa viongozi wahamasishe wachezaji na kuwa wamoja kwenye shida na raha na matokeo mazuri yangeonekana.Tulikuwa tunaenda vizuri hadi katikati ya msimu ila alipoondoka kocha mambo yakaanza kuharibika kila siku.Sijawahi ona yanga inafungwa mechi nyingi hivi kama msimu huu. Nafikiri tunahitaji viongozi wapya haraka sana ili tujipange mapema kwa mashindano ya CAF yanayoendelea na msimu ujao wa ligi kuu.
 
Timu gani bora iliyo mkoani kwa mfano?


Ubora kwa uchezaji ziko nyingi kama vile Ndanda FC, Mbeya City, Mtibwa Sugar, Singida United.....si umeona uchezaji wao? Wako fiti kiuchezaji shinda Simba na Yanga.
 
="donbeny, post: 27320161, member: 164867"]Yanga ya miaka ya 1990'S hadi majuzi ndio ilikuwa bomba,mimi sijui tatizo la yanga kwa sasa hata kama hela hakuna inatakiwa viongozi wahamasishe wachezaji na kuwa wamoja kwenye shida na raha na matokeo mazuri yangeonekana.Tulikuwa tunaenda vizuri hadi katikati ya msimu ila alipoondoka kocha mambo yakaanza kuharibika kila siku.Sijawahi ona yanga inafungwa mechi nyingi hivi kama msimu huu. Nafikiri tunahitaji viongozi wapya haraka sana ili tujipange mapema kwa mashindano ya CAF yanayoendelea na msimu ujao wa ligi kuu.[/QUOTE]
Zamani Yanga ilikuwa inapambana hata nyakati ngumu.
 
Kwa hali inavyoendelea hapo klabuni kwetu naona kuanzia wachezaji, benchi la ufundi mpaka viongozi hakuna anayejali wala kujivunia Yanga. Sasa tunafungwa hovyo hovyo na timu za kawaida kabisa tena mfululizo.

Hakuna anayejali. Katika mechi tisa zilizopita za mashindano Yanga imepoteza mechi sita, sare mbili na kushinda moja. Hii Yanga kweli timu ya wananchi?? Kweli?? Afadhali wangeshuka daraja kabisa..... No spirit, no fight, no hunger. Yanga hii nembo ya uhuru na taifa hili... kweli inakuwa hivi?...khaaaahhhh.

Lazima uelewe kwamba si kila mara timu inatakiwa kujitoa muhanga ili ipate ushindi. Inashangaza kwamba hakuiona timu ilivyopambamna kwa muda mrefu ikiwa miongoni mwa timu mbili za juu. Inapofikia hatua ya kukosa nafasi ya kwanza ya ubingwa ilhali nafasi ya pili haina umuhimu tena na wala timu haiko hatarini kushuka Daraja, kuna haja gani ya kuwachosha wachezaji wachache wasio majeruhi kupigania ushindi, badala ya kuelekeza nguvu kwenye mashindano makubwa zaidi inayoendelea nayo? Mpenzi anayetumia hali hiyo kuanzisha zengwe lisilo la lazima klabuni hana tofauti ni kigwagula Akilimali kinachotumia kila changamoto inayoitokezea timu kutafuta kiki.
 
Yanayojiri huko Kenya ni ushahidi kwa niliyoyasema.
 
Usijivunje moyo kijana, Yanga si timu ya maana, ni sawa tu na timu zingine za Premier League. Miaka yote walikuwa wanabebwa tu. Kama TFF wakiwa makini na marefa wao usije kushangaza both Simba na Yanga zinashuka daraja. Zenyewe ni timu kongwe hapa nchini ila si bora kama wananchi wengi wanavyofikiria, just angalia uchezaji wao then linganisha na vipaji kama vile Ndanda, Singida United, Mbeya City....hapa ndipo utashangaa kwanini hizi timu kongwe si lolote si chochote.
umeisahau Lipuli mkuu...
 
Kwa sasa ushindi inakuwa ngumu.. hakuna mtu wa kupaka Grease team pinzani.. hakuna mtu wa kupaka Grease marefarii.. lazima vyuma vibane . kwa sasa mpira ni uwanjani na watu woooote wanaona unachezwa live kabisa bila chenga.
 
Kwa sasa ushindi inakuwa ngumu.. hakuna mtu wa kupaka Grease team pinzani.. hakuna mtu wa kupaka Grease marefarii.. lazima vyuma vibane . kwa sasa mpira ni uwanjani na watu woooote wanaona unachezwa live kabisa bila chenga.
Na Mikia alicheza kihalali siku ile tu na Kagera Sugar.
 
Back
Top Bottom