Zamani mtu akiwa na mahusiano na CCM aliitwa Mamluki na Chama chake kiilitwa ‘CCM B’. Wapinzani walikataza mahusiano na CCM

Zamani mtu akiwa na mahusiano na CCM aliitwa Mamluki na Chama chake kiilitwa ‘CCM B’. Wapinzani walikataza mahusiano na CCM

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF yeye tayari ameonyesha wazi kumuunga mkono mama, juzi kati lipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari alikwenda mbali sana kwa kuonyesha yupo tayari kumfanyia mama kampeni 2025.

Prof. huyo ambaye ndiye muasisi na muanzilishi wa vuguvugu la vyama vingi Tanzania alimalizia kwa kusema 2025 mama anatosha kugombea kiti cha Urais. Inatia shaka kwani tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi 1995 Prof. huyu ambaye hajawahi kukosa kugombea uchaguzi mkuu mpaka leo kwani amegombea zaidi ya mara 5 sasa bila kuwa Rais.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe tofauti na zamani ambapo alikuwa anawazuia makamanda kuwa karibu na Ma CCM na kuwafukuza wengi aliodai ni mamluki leo imekuwa ni tofauti kabisa kwani tayari amekaririwa mara kadhaa akimpongeza mwenyekiti wa CCM na kumuunga mkono mama. Mwenyekiti huyo tayari ameonekana kuwa na mahudhulio mengi pale Ikulu kuliko kiongozi yeyote wa upinzani tangia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Mzee huyu amekwenda mbali zaidi kwa kubadili gia angani kwa kuwaambia makamanda kuwa kwa sasa hataki kamanda mwenye fujo na kuwataka watulie mama anajenga nchi.

Zito ambaye leo hii ukimsikiliza unaweza usielewe kuwa ni yeye au kapandikizwa mtu ndani yake, Mh. huyu ameonekana katika vyombo mbalimbali vya habari akiunga mkono kilakitu anachofanya mama tofauti na zamani alikuwa anapinga kilakitu. Juzi juzi Zito hakuonyesha mapenzi yake kwa awamu ya 6 bali mahaba kwa kenda mbali zaidi kwa kuonyesha chuki kwa awamu ya 5 kwa kusema wote waliokuwa wanampenda JPM na wakazikwe pembeni ya kaburi lake kule Chato.

Ndugu zangu maisha yanaenda haraka sana na kushangaza, sosayati imecheji up side down. Jana nilikuwa kitaa katika kijiwe mwanachama wa CCM na Chadema wanabishana nilitaka kudondoka nizimie.
Yule mwanachama wa CCM alikuwa anatilia shaka hii awamu ya 6 hasa akisema hari ya maisha imekuwa ngumu sana kipindi hiki bidhaa kupanda kwa kasi huku akiwa kama anakosa imani na mwenyekiti wake Chifu Hangaya. Lakini yule mwanachama wa Chadema alimkingia kifua mwenyekiti wa Ccm kuwa mama anaupiga mwingi kwanza amefanya Royo Tuwa pia anasafiri nje hili kuleta vijiela na muda si mrefu mambo yatakuwa mauri.

Mimi mtoto wa mchungaji sielewi nipeni mwongozo kwani wananchi kwa sasa nani atawasemea?
 
Ntoto ya nchunga kondoo acha uchonganishi basi,huu ni muda wakutibu makovu yaliyoletwa kwao na waupande wako wenye mawazo na mitazamo ya chuki.Hivyo maswali na hoja hizi Kwa Sasa ni mbinu za kumkwamisha yanayofanywa kuliponya taifa .
 
Punguza stress.
"Kama unampenda jiwe nenda ukazikwe naye Chato"....by Zitto Ruyagwa Kabwe.
 
Back
Top Bottom