Zamani viwanja vilikuwa unaamka asubuhi unaenda kuwahi, ila unakuta mzazi hana ardhi anayomiliki hadi sasa

Zamani viwanja vilikuwa unaamka asubuhi unaenda kuwahi, ila unakuta mzazi hana ardhi anayomiliki hadi sasa

Umeamdika general sana, bahati mbaya ni hadithi za kusikia. Hakuna data za kuthibitisha kuwa ajira zilikiwa nyingi kuliko wahitaji.
Ajira zenyewe zilikuwa na mshahara mkubwa kiasi gani ili mtu aweze kumudu maisha ? Ajira za vibarua ndio ajira za kumtoa mtu ?
Kiufupi ajira za sasa ni nyinngi kuliko zamani na ndio maana sasa mtu anaweza kujiajiri mda wowote akiamua. Sasa hivi kila kitu ni ajira hadi uchawa, kukata viuno, kutembea tu nayo ni ajira.
Ni kitu cha ajabu sana kuamini zama za giza kulikuwa na ajira nyingi kiliko zama za teknolojia.
Kila watu na zama zao, ishi zama zako, mbona mwewe hawarithishwi chochote ila wanaishi sembuse binadamu aliezungukwa na fursa kibao. Fursa zote zipo hata ardhi ipo. Kuna watu wazazi wao hawakumiliki ardhi kariakoo ila sasa hivi wana ardhi kariakoo., ukitaka hata london au newyork utamiliki ardhi ni akili yako tu, acha lawama. Rlob Musl jazaliwa Africa huku leo anamiliki ardhi USA wewe upo wapi ? Akili, Akili, Akili huu ndio urithi mkubwa kutoka kwa wazazi wetu.
Nadhani logic sio kuwapo kwa ardhi ya kurithishwa, kitu cha msingi ni wazazi kutokuwa tegemezi kwa watoto wao ilihali walikuwa na fursa ya kujiwekeza na wakaweza kumudu maisha yao angalau uhakika wa milo mitatu kwa siku na kumudu gharama za kawaida za maisha.
Katika kitu unapaswa kujifunza hakunaga hela nyingi ama kidogo, bali kuna matumizi makubwa na madogo. Ndiyo Maana tangu Dunia kuumbwa watu wanapambana na scarcity of resources, unlimited wants and Economic choices.
Kwa kuzingatia hilo, ni namna gani unatumia kipato chako ndiyo kitu cha msingi kuliko kipato unachopata, kwa mfano ukiishi kwenye jiji kama Dsm unaweza ukaishi kwa siku kwa kutumia 5,000 na ukapata milo mitatu lakini pia unaweza ukatumia hata laki tatu kwa kupata hiyohiyo miilo mitatu. Pia kuna mtu anaishi jijini analipa kodi ya 50,000/= kwa mwezi lakini bado kuna mtu hiyo hiyo 50,000/= analipia chumba ch kulala kwa usiku mmoja.
Kuna watu wana ujira mzuri TRA lakini hawana hata kibanda lakini kuna mtu anaendesha bodaboda au mama lishe na bado analala na kuamka katika kibanda chake.
Mindset ndiyo kila kitu katika kuamua hatma ya maisha ya mwanadamu na sio kipato au level ya elimu. Yupo anayelipwa ujira mdogo ambaye anaishia kuilalamikia Serikali, lakini yupo anayelipwa ujira sawa na huyo lakini kaamua ku multiply kipato chake na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Unashindana na matoleo ya iphone wakati hata ukiwa na tecno bado utakuwa una access sawa ya JF kama wengine.
Omba Mungu akupe akili ya kijitambua unaweza kubadili changamoto kuwa fursa. Wapo waliotokea vijijini wakafika mjini na kujiapiza kujituma watoto wao wasiishi ufukara waliopitia wao, ila wapo pia waliofika mjini na kuona kama walichelewa kukutana na starehe za jiji ikawa ni mwendo wa kuvunja mifupa ingali meno bado iko
 
Kizazi cha miaka ya 1950 -1970 amabao ndo wazazi wetu walikuwa ni kizazi cha watu wazembe.

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho kimekufa na ukimwi kwa kupenda Sana ngono.

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho kinatoa vitisho vya laana .

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho hakina maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiakili.

Kizazi hiki ndo kilishikilia dini na kusahau mila za babu zetu.

Kizazi hiki ndo kizazi cha laana starehe zote kilikuwa kinaendekeza wao.

Zamani ardhi kupata ni sawa na bure Ila unakuta mzazi hana ardhi anayomiliki.
Na wewe sahivi bado ardhi ipo nenda kakamate

Ova
 
Mwanangu wa kiume firstborn majuzi nilimpeleka kwenye eneo ninalotaka kujenga....nikamwambia hapa nakujengea wewe na mdogo wako....ukikua upatunze vyema....akijibu "hapa ni pakwako,Mimi kwangu nitajenga nikiwa mwanajeshi"...na yupo 9 yrs old.Sasa wewe mkuu,sijui unawaza nini...ndo mnaoua wazazi ili mrithi mali
 
Mimi sina hata kipande cha ardhi nikifa wachimbe kaburi wanizikepo, sina. Ila nina mashamba ya kulima tena nachagua yale yenye rutuba!!!

Sijajenga, ila nina nyumba safi tu ya kuishi. Vyote hivi nimekua nimekuta vipo na vingine vimenunuliwa nikiwepo. Kazi yangu nafanyia kwenye mashamba ya wazazi.

Wazee wangu hua wanasimulia jinsi walivyopata vile tulivyo vikuta, baba hua anatuambia hana shamba wala kiwanja alichonunua kwa zaidi ya elfu hamsini, halipo!! Mengi ni ya 20 na ni makubwaa na wakati anayanunua yalikua mapori tu na kuongeza kua alinunua kwa watu waliokatiwa bure na serikali yaan kaz yao ilikua kuhesabu miguu, kupanda katani/ mkonge au minyaa kwa ajiri ya mipaka halafu ukiamua utalima ukitaka unaliacha liwe pori.

Kuna wazee waliwahi maeneo ambayo kwa sasa ni migodi ya dhahabu, mzee wangu anayo japo hayana dhahabu kivile ila ndio yananilisha kwa sasa.

Kwenye utaftaji mzee anasema hakua na bahati sana kama baadhi ya marafiki zake ambao walishika sana pesa kumzidi yeye, lakini huwezi amini wazee wenzake hao kina pondamari kifo chaja ndio ninaofanya nao kazi ya uchimbaji dhahabu kwenye mashamba ya rafiki yao baba yangu nikiwa kama msimamizi wao!!!

Kuna mzee xx alianipa stori juzkati ambayo baba hakuwahi kunisimulia ila nilipo muuliza alisema ni kweli, zamani wakiwa vijana mzee wangu aliona shamba linauzwa elfu15 akaenda kwa rafiki yake huyo xx akamwambia wachangie walinunue then wagawane, bwana xx akamwambia mzee sina shida na kulima kama huna hela nikuazime utarudisha. Mzee akawa amenunua lile shamba ekari9 kwa elfu15 ya mkopo.

Miaka saba baadae lile shamba lilitema dhahabu ambazo ndio zilimpa mtaji mzee. Mzee xx ana nyumba ya tope ndogo tu familia kubwa hana hata shamba la kulima anaomba kwa mzee wangu kwa miaka mingi sana analima mashamba yetu hadi kuna watu wanajua ni mashamba yake.

Mashamba yote na viwanja ambavyo walinunua kwa chini ya laki moja kwa sasa yanauzika kwa kwa bei kubwa kuanzia milioni 10 hadi 200m. Wazee kww sasa ni wakulima na wafugaji tumesoma tumekosa ajira nasasa tumejiajiri kwenye ardhi ya wazee wetu. Ardhi ni MALI.

Mleta maada hata kama hana ardhi bado ana haki ya kukosoa asipuuzwe kwa hoja dhaifu za kuzaliwa na kulelewa wala kusomeshwa.
 
Kizazi cha miaka ya 1950 -1970 amabao ndo wazazi wetu walikuwa ni kizazi cha watu wazembe.

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho kimekufa na ukimwi kwa kupenda Sana ngono.

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho kinatoa vitisho vya laana .

Kizazi hiki ndo kizazi ambacho hakina maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiakili.

Kizazi hiki ndo kilishikilia dini na kusahau mila za babu zetu.

Kizazi hiki ndo kizazi cha laana starehe zote kilikuwa kinaendekeza wao.

Zamani ardhi kupata ni sawa na bure Ila unakuta mzazi hana ardhi anayomiliki.
Mkuu,

Unaona ni bora usingezaliwa kabisa?
 
Hata sasa kuna maeneo ukienda ni nguvu yako tu kufyeka utapoishia ndio e eneo lako.

Jiandae nawe kuja kulaumiwa.
 
Licha ya kwamba wachangiaji wengi wamejaribu kukupinga lakini mada yako ina Ukweli mchungu Sana. Wakati wa miaka ya 1950-1980's Ardhi ilikuwa inapatikana kwa urahisi Sana hapa Tanzania, tena ilikuwepo ya kutosha Sana, lakini Watu wengi wa nyakati hizo hadi leo wengi wao hawana ardhi wanayomiliki.
Hata sasa bado ardhi ni ya kutosha sana
 
Back
Top Bottom