The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Ukiingia online pana diaspora kibao wanatoa connection jinsi gani mtu anaweza kwenda Ulaya, marekani,china, Singapore, Japan, Brazil, latin American, Canada nk ni wewe na wanatoa information zote ni wewe tu uza shamba lako la urithi uwahi njiapanda ya Ulaya kama umechoka kubadilisha sori ya viatu kwa Mangi baada ya kutembeza bahasha kila ofisi ukijaribu kuokota kazi mwaka wa kumi huu tangu umalize chuo huku ukiilaumu ccm ndio chanzo cha ugumu wako wa maisha baada ya kushindwa kuigeuza elimu yako kuwa fikra ya kubadili maisha yenu kijijini mlipojenga nyumba juu ya ardhi yenye rutuba iliyojaa madini na maji tiririka mwaka mzima.
Sio vibaya maisha popote wao wanakuja kwetu baada ya kukimbia maisha magumu kwao wanakuja kwetu wanaona fursa wanatoboa wanakuja na akili wanachota pesa wanaondoka nasi tunajazana kwenye balozi zao baada ya kwenda kwa waganga au kwa mitume na manabii kupakwa mafuta ili tusinyimwe visa hakika ukifika kule uhakika wa KAZI zipo unapata unatuma home ili kupunguza gap la umasikini.
Wapo wanaoenda kwa ndoa, kazi, masomo,utalii nk kila mmoja na bahati yake.