Zamani waafrika walipelekwa utumwani kwa lazima Leo waafrika wanalilia kwenda utumwani kwa hiari

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Ukiingia online pana diaspora kibao wanatoa connection jinsi gani mtu anaweza kwenda Ulaya, marekani,china, Singapore, Japan, Brazil, latin American, Canada nk ni wewe na wanatoa information zote ni wewe tu uza shamba lako la urithi uwahi njiapanda ya Ulaya kama umechoka kubadilisha sori ya viatu kwa Mangi baada ya kutembeza bahasha kila ofisi ukijaribu kuokota kazi mwaka wa kumi huu tangu umalize chuo huku ukiilaumu ccm ndio chanzo cha ugumu wako wa maisha baada ya kushindwa kuigeuza elimu yako kuwa fikra ya kubadili maisha yenu kijijini mlipojenga nyumba juu ya ardhi yenye rutuba iliyojaa madini na maji tiririka mwaka mzima.

Sio vibaya maisha popote wao wanakuja kwetu baada ya kukimbia maisha magumu kwao wanakuja kwetu wanaona fursa wanatoboa wanakuja na akili wanachota pesa wanaondoka nasi tunajazana kwenye balozi zao baada ya kwenda kwa waganga au kwa mitume na manabii kupakwa mafuta ili tusinyimwe visa hakika ukifika kule uhakika wa KAZI zipo unapata unatuma home ili kupunguza gap la umasikini.

Wapo wanaoenda kwa ndoa, kazi, masomo,utalii nk kila mmoja na bahati yake.
 
Kila ndoto ya kijana wa kiafrika ni kuikimbia nchi yake aende nchi nyingine iliyojengwa tayari
 
Ukiingia online pana diaspora kibao wanatoa connection jinsi gani mtu anaweza kwenda Ulaya, marekani,china, Singapore, Japan, Brazil, latin American, Canada nk ni wewe na wanatoa information zote ni wewe tu uza shamba lako la urithi uwahi njiapanda ya Ulaya kama umechoka kubadilisha sori ya viatu kwa Mangi baada ya kutembeza bahasha kila ofisi ukijaribu kuokota kazi mwaka wa kumi huu tangu umalize chuo huku ukiilaumu ccm ndio chanzo cha ugumu wako wa maisha baada ya kushindwa kuigeuza elimu yako kuwa fikra ya kubadili maisha yenu kijijini mlipojenga nyumba juu ya ardhi yenye rutuba iliyojaa madini na maji tiririka mwaka mzima.
Sio vibaya maisha popote wao wanakuja kwetu baada ya kukimbia maisha magumu kwao wanakuja kwetu wanaona fursa wanatoboa wanakuja na akili wanachota pesa wanaondoka nasi tunajazana kwenye balozi zao baada ya kwenda kwa waganga au kwa mitume na manabii kupakwa mafuta ili tusinyimwe visa hakika ukifika kule uhakika wa KAZI zipo unapata unatuma home ili kupunguza gap la umasikini.
Wapo wanaoenda kwa ndoa,kazi, masomo,utalii nk kila mmoja na bahati yake.
Ungekuwa na akili usingelaumu wanaokimbia maisha magumu bali ungewalalamikia miungu watu washenzi ,wakatili ,wezi , wabinafsi wasio na maono na wapumbavu wanaoongoza haya mataifa ya Afrika na kujiita viongozi
 
Samahani, neno "Utumwani au utumwa" lina maana gani kama lilivyotumika kwenye huu uzi?

Asante
 
Ungekuwa na akili usingelaumu wanaokimbia maisha magumu bali ungewalalamikia miungu watu washenzi ,wakatili ,wezi , wabinafsi wasio na maono na wapumbavu wanaoongoza haya mataifa ya Afrika na kujiita viongozi
Umemaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom