Zamaradi acha makelele, hamuwezi ku-control kila kitu

Kuna kitu kimoja kuhusu hili suala nimeambiwa leo. Nimeelewa hoja ya wasanii vizuri sana. Kilichofanywa na Steps ni vita dhidi ya waigizaji walioamua kujitoa Steps na kufanya kazi zao kwa kujitegemea.
Kilichotokea ni kwamba, baadhi ya waigizaji wameamua kujitoa chini ya Steps, kwa sababu za wanachodai ni kunyonywa na Steps na kunyimwa haki ya umiliki wa filamu zao.
Mikataba ya Steps inakataa filamu kuwa mali ya msanii, kwa maana kuwa filamu ni mali ya Steps. Na ndio sababu Kanumba amekufa huku akiwa hana hata filamu moja ambayo ni mali yake, na Sajuki pia.
Kwa mikataba hiyo, kunafanya wasanii wasiweze kunufaika na malipo ya vituo vya TV ya kuonesha filamu zao kama vile Zuku, Azam, DStv, Continental, TV 1, Sibuka na nyinginezo. Malipo yote huenda kwa Steps.
Jingine katika mikataba ya Steps ni kutokuwa na ratiba ya uhakika wa utokaji wa filamu ya msanii husika, kwa maana ya filamu kuweza kucheleweshwa kutoka hata zaidi ya miezi sita.
Na kwa bahati mbaya, kwa mujibu wa mikataba ya Steps malipo ya filamu husika hutolewa kwa msanii baada ya mwezi mmoja tangu filamu kuingizwa sokoni. Ni hali ambayo hufanya baadhi ya wasanii kukwama kiuchumi.
Jambo hilo lilifanya baadhi ya wasanii kujiondoa chini ya Steps, kwa kuanza kusambaza wenyewe filamu zao, na kuzipeleka pia kwenye vituo vya TV na kupokea wenyewe malipo yao.
Kwa siku za karibuni kundi kubwa la wasanii linasemekana kuondoka rasmi Steps, akiwemo Aunt Ezeliel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Mtitu, Richie, Ndende na wengineo.
Hali hii imemtisha Steps, kwa hiyo ameibuka na mpango wa kuwazima wasanii waliomkimbia kwa kuwatoa sokoni kwa kuuza filamu zake kwa bei ambayo hakuna msambaji mwingine ataweza kuuza.
Kwanini Steps anaweza kushusha na wengine hawawezi? Kwanza kabisa ieleweke kwamba Steps ana kiwanda cha kutengeneza empty DVD's, ana kiwanda cha kudurufu nakala za filamu, ana kiwanda cha kuchapa posters na ana kiwanda cha kutengeneza makasha. Kwa ujumla wake anafanya mwenyewe kazi zake zote.
Kwa hesabu hiyo Steps ana Uwezo wa kuuza filamu zake na kupata faida hata kama ataziuza shilingi 700 kwa bei ya jumla. Hii ndio sababu ya vilio vya wasanii na kupaza sauti.
Ukiliangalia hili suala juu juu tu unaweza usione hoja, na pengine kwa sababu wanashindwa kufafanua kwa kila mtu tatizo lao na bei Mpya na Steps kama walivyonifafanulia mimi.
Binafsi, nimeelewa hoja yao na nafikiria namna ya kuwasaidia.
Ova
 

Kama wamejitoa ina maana wanajiamini. wanaweza kufanya biashara bila steps, sasa wanacholia nini ikiwa mtu kaamua kushusha bei ya bidhaa zake wao wakomae na bei zao kama filamu zao zin! ubora watu watazichukua kwa bei yoyote.
 
Bora umwambie tena inaonekana hajui hajui uchumi huyoo mrs ruge
Hili ndo tatizo kubwa... hafahamu kwamba Profit is a function of Total Revenue and Total Cost! Revenue ikiwa constant na ukakata/ukapunguza gharama za uzalishaji, profit inaongezeka... likewise, cost ikiwa constant na mapato yakaongezeka, profit pia hupanda. Mapato yanaongezeka ama kwa kuongeza bei au kuongeza mauzo... always it's bad idea kuongeza mapato kwa kuongeza bei especially kama kuna close substitutes... na haya ma-DSTv, Zuku, Startimes & Co, ni close substitutes coz' kote huko kuna movie za kibongo; so the best way to increase revenues is through increasing sales... mauzo yanaongezeka kwa ku-cut down price huku ukiongeza unit production! Mambo kama haya Zamaradi hawezi kuyaelewa kwahiyo tusimlaumu...

Lakini tukija kwa upande mwingine, Zamaradi na wenzake wana kila sababu ya kulalamika! Unaposhusha bei kuna two direct effects, mosi ni hiyo ya kujiongezea mauzo but second, ni ku-cut down competition! Si kweli hata kidogo kwamba watakaoathirika na pirates coz' hawa wezi wa kazi za wasanii hawanaa production costs kubwa... all they need to have is just PC a with multiple burners, Disk Printer, a bunch of low quality empty CDs ambazo huuzwa sh. 100/- and cartridges... that's it... kwahiyo hawa hata wakiuza kwa sh. 500/- bado hawapati hasara coz' they don't have movie production cost ambayo akina Zamaradi wanayo! Jibu sahihi ni kwa akina Zamaradi nao kuongeza mauzo through price cut kama walivyofanya Steps lakini suala la kuongeza mauzo nalo is directly related to your distribution channels... hili la distribution channels ndilo litakalokutofautisha wewe na mtu kama Bakhresa endapo leo utaamua kuanzisha a milling business manake unaweza kujikuta unashindwa kusambaza even within Kinondoni wakati mwenzako anafika hadi Kanyigo!
 

Exactly nahis kinachowapa presha ni distribution, steps lazima ana connections so atawazidi tu, sijui sasa hapo watatumia mbinu gani aisee kazi nyingine hizi.......
 
Exactly nahis kinachowapa presha ni distribution, steps lazima ana connections so atawazidi tu, sijui sasa hapo watatumia mbinu gani aisee kazi nyingine hizi.......
Steps ni kampuni kubwa kwahiyo distribution kwao sio tatizo hasa ikiwa tunataka kuwalinganisha na akina Mtitu. However, if they work together, wanaweza kuwatikisa Steps kwa sababu, wao (wasanii) tayari wanakuwa na at least TSh. 10 million less in cost as compared... yaani, ikiwa wametengeneza movie ya sh. 10million na ikauzwa kwa Steps kwa sh. 20 million, then, ina maana for same movie katika hatua hiyo ya awali, kama msanii anaamua kuuza mwenyewe gharama yake hapo inakuwa sh. 10 million wakati kwa Steps ingekuwa sh. 20 million.
 

nadhani watakuwa wamekuelewa kama nilivyokuelewa mie.
Big up mkuu. Maana yawezekana hata wenyewe walikuwa hawaelewi wanachodai ni nini teh teh
 

hua unaongea points hadi unakera sana japo mi si mshabiki wa bongo movie
 

watu mna mapoints hadi mnakera
mi naona bora steps washushe bei ili nianze kumnunulia housegirl wangu movie maana za kukodi zinachosha
 
watu mna mapoints hadi mnakera
mi naona bora steps washushe bei ili nianze kumnunulia housegirl wangu movie maana za kukodi zinachosha
Ya kwangu ikishakuwa tayari am very sure utaipenda tu na haitakuwa tena ni product kwa ajili ya house girl wako pekee!!!
 
nadhani watakuwa wamekuelewa kama nilivyokuelewa mie.
Big up mkuu. Maana yawezekana hata wenyewe walikuwa hawaelewi wanachodai ni nini teh teh
Na labda kingine wasichokijua au wasichotaka kukijua ni kwamba hao Steps wana haki ya kuuza kazi zao hata kwa sh. 500/- na usiwafanye chochote!! Jana nilimsikia mmoja wao akisema kwamba serikali inatakiwa kupanga bei kama inavyofanya kwenye mafuta... hapa tena hawafahamu kwamba inachofanya serikali kwenye mafuta ni kuweka ceiling price... kwamba mathalani, ceiling price ya petrol ni sh. 2000/- kwa maana kwamba mtu haruhusiwi kuuza zaidi ya 2000/- lakini anaweza kuuza hata kwa sh. 1000/- kwa lita... labda alitaka kumaanisha price floor kama ile ya wakulima!!!!!
 
Kama wamejitoa ina maana wanajiamini. wanaweza kufanya biashara bila steps, sasa wanacholia nini ikiwa mtu kaamua kushusha bei ya bidhaa zake wao wakomae na bei zao kama filamu zao zin! ubora watu watazichukua kwa bei yoyote.

Mkuu nimeeleza kwa kirefu ili nieleweke. Pengine hukunisoma au umenielewa vibaya ama kuna hoja unaikwepa. Angalau ungenisoma ndio tungeweza kujadili.
Ova
 

Gharama za kutengeneza filamu kwa msanii na kwa Steps zinaweza kufanana mkuu. Kwa sababu filamu ni tofauti na muziki ambao anaweza rekodi msanii peke yake na akalipa studio tu.
Lakini filamu lazima alipe wasanii wa kushirikiana naye, wapiga picha na mambo mengine ya msingi kama ambavyo Steps atalipa na msanii atalipa, kwa hiyo gharama zitacheza mle mle tu.
Anachowaua Steps ni kwenye zoezi la kuzalisha nakala za filamu kama nilivyoeleza katika comment yangu ya awali, kwani ana viwanda vyote vya kuzalisha nakala za filamu.
Alichopaswa kufanya Steps ni kusikia kilio cha wasanii na kurekebisha mikataba yake hasa kugawana umiliki wa filamu ili hata baadaye familia ya msanii ipate hata malipo ya kuoneshwa kwenye TV.
Ova
 
movie za bongo iuzwe hata sh 200,kwanza hazina quality,ukiangalia movie inapoanza ushajua inaishaje,ukinunua movie ukishaangalia unaanza kujiuliza kwanini nimenunua hata!
huwezi kuuza bei ghali movie ambayo utadhani wameshut kwa kutumia simu.
 
watu mna mapoints hadi mnakera
mi naona bora steps washushe bei ili nianze kumnunulia housegirl wangu movie maana za kukodi zinachosha

tokea lile tukio la house girl wa uganda naona sahivi hawa watu wanaheshimika sana!' wengine wamewanunulia mahouse girl wao Vitz zakwendea masokoni ...........

Grand PA
 
Nilichomaanisha kuhusu gharama ni kwamba, wakati msanii anatengeneza filamu mwenyewe... akishalipa crew team na gharama zingine kisha total cost kufikia sh. 10million; hiyo inakuwa ndio production cost ya msanii husika!

Kwa upande wa Steps; huyu ana option mbili... ama ya ku-act as Executive Producer or Distributor. Akifanya as Executive Producer, ni kwamba itabidi amtumie producer ambao kibongo bongo ni wasanii wenyewe... kwahiyo, ikiwa filamu ya hapo juu gharama zake ni sh.10 million kv ni yake mwenyewe, kama kazi angepewa na Steps, hapo Steps wangelazimika kulipa zaidi ya 10 million... ten million ni kwa ajili ya production cost na ya juu ndo malipo ya producer... kwahiyo, in most cases, Steps wangetoa kama 20 million ili huyu producer azitawanye kwenye idara mbalimbali na zitakazobaki ni fungu lake. Alternatively, aki-work as Distributor, ina maana filamu ya msanii ambayo ameitengeneza kwa 10 million, akiipeleka Steps, katika mazingira ya kawaida atauza zaidi ya 10 million ili apate cha kwake!

Mtu ambae anaweza kufanana fanana gharama na steps ni wale ambao wanafanya kazi as executive producers na hawana kofia ya u-producer... hawa ni aina ya watu kama akina Zamaradi! Lakini ukimchukulia mtu kama Mtitu... mwenyewe ni producer , executive producer na director... kwahiyo huyu hana gharama za kumlipa producer and in most cases hata director! Si ajabu main character akawa mwenyewe pia... producer, director na main character ndio wanalipwa pesa nyingi... mtitu hapo, anajilipa mwenyewe wakati Steps atalazimika kuingia mfukoni unless tuingize dhana za kiuchumi kama vile kuingiza imputed costs!
 
Ya kwangu ikishakuwa tayari am very sure utaipenda tu na haitakuwa tena ni product kwa ajili ya house girl wako pekee!!!

hahaaaaaa usijali ikifkia hadhi ya movie za kuambiana au kanumba sawaa
 
tokea lile tukio la house girl wa uganda naona sahivi hawa watu wanaheshimika sana!' wengine wamewanunulia mahouse girl wao Vitz zakwendea masokoni ...........

Grand PA


hahahaaaaaaaaaaaa
umenifurahisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…