Kuna tatizo la Point of View.
Mimi naona Giggy kaongea vizuri sana.
Anasema yeye alikataliwa na wazazi wake tangu kabla hajazaliwa, na anaelezea kuwa hata kuzaliwa kwake kulimsononesha mama yake.
World has created her
Nafikri watu wengi wanachukia matokeo lakini si sababu ilizomfanya huyu binti kufanya hayo anayofanya.
Kwa upande wangu kwanza nampongeza mtayarishaji wa kipindi pia ninampongeza huyu binti mdogo masikini kwa ujasiri wa kufikia hapo alipo (ingawaje si pazuri lakini ni bora kuliko angekuwa jambazi)
Ni kwanini ninasema haya:
Kwanza ukiangalia histori yake ni kuwa huyu binti masikini hakuwahi kupendwa, hakuwahi kupendwa na baba yake na hakuwai kuona penzi la mama, Kama tunavyofahamu mapenzi ya hawa watu wawili ambao ndio walezi wako wakuu katika hii dunia ni muhimu lakini binti huyu hafahamu nini mapenzi ya mama au baba.
Pia ni mtoto ambaye ameanza kuonja machungu ya wamama wasiojua umuhimu wa mtoto, wamama wapelekao hasira za mabwana zao kwa watoto wao, wamama wanaoamini kuwa ugonjwa au ukilema wa aina yeyote unaletwa na malaika (watoto).
Ukimsikiliza kwa makini unaona ni binti anayetafuta penzi la mama yake, ni binti ambaye yuko tayari kufanya kitu chochote hata kuuza mwili wake ili apate mapenzi ya mama, Unaona jinsi haya maisha yalivyomhadhiri mpaka anafanya vitu vya ajabu yeye haoni kama ni ajabu kwani shida yake ni awe na mahusiano mazuri na mama yake.
Kwa kweli huyu binti ni kuwaonea huruma na pia liwe funzo kwa vijana ambao wako njiani kupata watoto pindi upatapo mtoto, mpende na mdhamini kwani mtoto hiyo ni zawadi tosha..Msiwanyayasa watoto kwa makosa yenu wenyewe au kwa makosa ya wenza wenu ukumbuke mtoto ni mtoto na hana hatia na mtoto hawezi kuchagua ni wazazi wapi nizaliwe nao.