Zamaradi kuasili mtoto

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Host wa Program ya Take One kupitia CloudsTV , Zamaradi Mketema ametangaza nia yake kuwa anataka kuasili mtoto ili kutimiza ndoto yake aliyokuwa nayo tangu akiwa mwanafunzi .

Host wa Program ya Take One kupitia CloudsTV, Zamaradi Mketema. Akizungumza na mwanahabari wetu, Zamaradi ambaye pia ni mwigizaji, alisema amekuwa na nia hiyo kabla hajajaliwa mtoto hivyo hata alipopata bado anataka kutimiza ndoto yake hiyo.

"Naumia sana ninapoona watoto yatima japokuwa na mimi ni yatima lakini nia hiyo nilikuwa nayo, natamani sasa kukamilisha ndoto yangu hiyo kwa sababu naamini kabisa nitaweza na Mungu atanisimamia, " alisema Zamaradi .
 
Huyo mtoto mwenyewe aliyenaye kumtunza ni shida sasa huyo wa kuasili je.
 
Mbona umestuka madamee...au kwa sababu kataja mambo yako asubuhi asubuhi....

Kama ulikuwepo.....asubuhi yote hii hata riziki hatujazikamata tunaanza kusoma haya, aisee.
 
Huyo mtoto mwenyewe aliyenaye kumtunza ni shida sasa huyo wa kuasili je.

Ahaha ahahah si ndio apo, ayo mambo awaachie akina madoma wenye fani na pesa zao, wanatak wa asili mtoto baadae wamfanye houseboy/girl
 
Huyo mtoto mwenyewe aliyenaye kumtunza ni shida sasa huyo wa kuasili je.[/
Baba watoto Boss Ruge anahudumia mtoto wake mbona..ila Ruge ni noma khaaa...!!kila mtu na mikato yako..mie walaa..!!
 
 
Huyu anatafuta housegirl tu hana lolote aasili kwan ndugu zake wameisha wa kuwasaidia basi awachukue yatima kama atawaweza wotee
 
Kwanini watu mnapinga kila jambo? Muacheni amuasili, akishindwa kumlea basi ndio mumhukumu! Tusiwe too much negative wakuu!
 
Hana pesaa wewee
Pesa zipi ambazo hana? Anafanya kazi halafu asiwe na pesa za kuwatunza watoto wawili? Wewe kwenu mmezaliwa wangapu na wazazi wako walikuwa matajiri kiasi mpaka wakulee? Ndg zanguni wapi watoto yatima wengi sn wanaotamani kuishi bt Huyo maisha ya chini ya kula vitumbua na chapati, tuwaunge mkono mioyo ya upendo wanaotaka kusaidia wengine
 
Kwani ''KUASILI'' mtoto maana yake nini???

Naona wengi mmeelewa humu kasoro mimi tu.....

kuasili mtoto ni kitendo cha kisheria kumchukua mtoto ambae si wako wa kumzaa na kumlea kama wako ,mara nyingi mtoto huyo anaweza kua yatima au anaishi kwenye mazingira magumu, sujui nkuelezeeje lakini ni hivyo yani anakua wako kabisa anaweza tumia hata jina lako lakini kitendo hiki kinasimamiwa na sheria na makubaliano kati yako wewe unaeasili na wazazi au walezi wa huyo mtoto. kwa kiingereza wanaita ku "adopt"(kama sijakosea spelling)
 
Nasikia ruge kafa kaoza pale, kamjengea nyumba nzuri na miradi kamfungulia yani chochote anachotaka hakosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…