Zamaradi mketema: Naongeza tena watoto wawili

Zamaradi mketema: Naongeza tena watoto wawili

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, kinachorushwa kupitia Clouds TV, Zamaradi Mketema ‘ Zama ’ amefunguka kuwa , ataongeza tena watoto kwani tangu amejifungua mtoto wa pili ameona nyumba imekuwa na raha sana .
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, kinachorushwa kupitia Clouds TV ,

Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni, Zamaradi alisema , ameshangazwa na furaha iliyotawala kwake na mzazi mwenzake na kwamba siku si nyingi atabeba mimba nyingine mbili fasta .
“Yaani watoto ni furaha kubwa , mimi nitaongeza tena wawili wa haraharaka maana nimegundua kuna kitu kinaongezeka kila unapoongeza mtoto mwingine ndani ya nyumba ikiwa ni pamoja na baraka , ” alisema Zamaradi .
 
Mimba ana beba yeye, Raha anaona yeye , kutapika yeye , hospital yeye, azae Hata 20 Kwa Raha zake, wala Asiseme afanye tuuu , wamezaa watu kweli seuze yeye tia mchuzi pangu pakavu....
 
Namtakia kila la kheri.

Amezaa wapili na baba wa mtoto wa kwanza? Au alishaolewa?
 
Wala haipendezi "kujizalia zalia" nje ya ndoa. Wataoana lini na huyo "mvunja amri ya sita" mwenzie?

Madai ndo anatujibu tulivyomchamba kuzaa nje ya ndoa.
 
Back
Top Bottom