Zambia: Mashabiki wavamia nyumba ya mchezaji aliyekosa nafasi za wazi uwanjani

Zambia: Mashabiki wavamia nyumba ya mchezaji aliyekosa nafasi za wazi uwanjani

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Polisi nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai kuwa walivamia nyumba ya mwanasoka wa timu ya taifa ya kandanda Alex N'gonga.

Mashabiki hao walishikwa na hasira kuwa Ng'onga. alikosa nafasi wazi za kufunga wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo Nigeria iliishinda Zambia bao 1-0

Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Kitwe ambao waliitupia mawe, kwa mujibu wa kamishina wa polisi Charity Katanga.

"Tumekamata watu watano kwa makosa ya kuharibu mali na sasa wanazuiliwa ns polisi."

Kushindwa kwa Zambia kuliipokonya fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi ambapo Nigeria walifuzu

Swali:
Kukosa umakini na kujituma kwa wachezaji wetu uwanjani; Je, kuna haja ya kuwaiga Wazambia katika hili?
 
Nawapongeza hawa wachezaji wetu bongo wangepelekwa hata JKT tu
 
Amekosea magoli wanampiga je angekuwa amefunga wangempa nini?sifa au hongera nyingi mpira pesa bhwana
 
Kama ulikuwa Ni uzembe wa makusudi walipaswa wachezaji wote wangepelekwa chuo cha mafunzo wakapige kwata kidogo Kama wakati fulani ilipotokea Ivory coast..
 
Back
Top Bottom