Zamu ya nani Jumapili? : Ni zamu ya Mtibwa Sugar.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Baada ya Mnyama mkali mwituni, asiye na masihara kabisa akiwa mawindoni, Simba SC kutakata ipasavyo, katika kila windo analoingia.. Sasa ni zamu ya vijana toka Manungu [Mtibwa Sugar] kukutana na dhahama lake.

Lini? Ni jumapili ya wiki hii [ 11.09.2016] katika dimba la Shamba la Bibi ambapo Mnyama anahistoria kubwa sana katika uwanja huo.

Ombi langu kwa Thobias Kifaru na vijana wake.
Kabla ya ligi kuanza Kifaru alitamka.. "Mtu yoyote ambaye ni mwanamichezo atakubaliana nami, Yanga ndo bingwa wa msimu huu, Azam itamaliza nafasi ya pili na Simba nafasi ya tatu".
Naheshimu mawazo yake, ila najiuliza kama tatu bora ndo ziko hivyo, Mtibwa wanashiriki ligi ili iweje??

Kifaru na Vijana wako, 11.09.2016 tutawaonesha ni kwa jinsi gani tumejipanga vyema kuibuka mabingwa wa VPL msimu huu na kuwa "wawakilishi bora" wa Kimataifa na si kuwa "wawakilishi uchwara".

Baada ya kutoa suti Mtwara.. Mtaa wa pili nako hali ya hewa ikoje??
Katibu wao aibuka.. “Sisi tumeondoka leo Mtwara, tutafika Dar es Salaam mchana na hatutafanya mazoezi leo. Kesho ni Ijumaa na keshokutwa Jumamosi tuna mechi nyingine, wakati Simba waliocheza jana Dar es Salaam wana mechi nyingine Jumapili”.
Kwanini myaone haya leo wakati ratiba imetoka muda sana?
Nishaanza kuona dalili za mtu kukimbia uwanja 01.10.2016.

SIMBA SPORTS CLUB, NGUVU MOJA.
 
Msimamo wa VPL mpaka sasa nao uko hivi, [emoji116]

Mtaa wa pili siwaoni kabisa.. Sijui wako namba ngapi?
 
Reactions: PNC
Mechi 5 za nyumbani zitawafanya muongee sana.... Mtakapo enda mikoani..... na soka lenu la pasi pasi......
 
Eeti mechi 5 nyumbani mfululizo afu wanalalamika Yanga anabebwa .....
 
Eeti mechi 5 nyumbani mfululizo afu wanalalamika Yanga anabebwa .....

Mkuu Yanga ndo washaanza kulalamika mapema kua Mnyama anabebwa, na hii ni kutokana na vipigo mfululizo tunavyotoa..

Katibu Mkuu wa Yanga alinena haya baada ya timu yake kutoa suti na Ndanda "B".. “Sisi tumeondoka leo Mtwara, tutafika Dar es Salaam mchana na hatutafanya mazoezi leo. Kesho ni Ijumaa na keshokutwa Jumamosi tuna mechi nyingine, wakati Simba waliocheza jana Dar es Salaam wana mechi nyingine Jumapili”.
 
Mechi 5 za nyumbani zitawafanya muongee sana.... Mtakapo enda mikoani..... na soka lenu la pasi pasi......

Mkuu Kipindi tugawa dozi nzito nzito mkoani Morogoro, mlikuja na hili
 
Mechi 5 za nyumbani zitawafanya muongee sana.... Mtakapo enda mikoani..... na soka lenu la pasi pasi......

Mkuu Kipindi tugawa dozi nzito nzito mkoani Morogoro, mlikuja na hili.. "mnavionea vitimu vidogo vidogo mnaongeeea, ngoja ligi ianze mtakimbia jukwaa."

Sasa ligi imeanza, Mnyama anagawa dozi kwa mmoja baada ya mwingine, mmekuja na haya.. "Mechi 5 za nyumbani zitawafanya muongee sana.... Mtakapo enda mikoani..... na soka lenu la pasi pasi'..

Mkuu, tulieni tuli.. dawa iwaingie.
 
Mechi 5 za nyumbani zitawafanya muongee sana.... Mtakapo enda mikoani..... na soka lenu la pasi pasi......
Siku zote uwanja wa nyumbani ndiyo umekuwa ukituhalubia sana labda kama huna kumbukumbu mfano mwaka Jana tulifungwa na Cost tukatolea FA, Toto tukapoteza matumaini ya VPL hivyo viwanja wa nje kwatu siyo tatizo sana kama vyura fc..
Msimamo wa VPL mpaka sasa nao uko hivi, [emoji116]

View attachment 396577

Mtaa wa pili siwaoni kabisa.. Sijui wako namba ngapi?
 
Eeti mechi 5 nyumbani mfululizo afu wanalalamika Yanga anabebwa .....
kumbuka JkT ruvu, ruvu shooting, hutumia uwanja wa taiga kama uwanja wao wa nyumvani wanapokutana na timu kubwa hivyo mpaka sasa Simba tumecheza mechi 2 tu za nyumbani...
 
kumbuka JkT ruvu, ruvu shooting, hutumia uwanja wa taiga kama uwanja wao wa nyumvani wanapokutana na timu kubwa hivyo mpaka sasa Simba tumecheza mechi 2 tu za nyumbani...
Uongo mtakatifu..... Mpwa..... Mwenyeji zote ni simba....
 
Msimamo wa VPL mpaka sasa nao uko hivi, [emoji116]

View attachment 396577

Mtaa wa pili siwaoni kabisa.. Sijui wako namba ngapi?
Ndugu yangu una unazi kama sio ushabiki maandazi...

Yaani unasahau kabisa kwamba Yanga bado ana mechi moja mkononi?...

Halafu, wanaoongoza ligi si Mbeya City?....Ama?
 
Ndugu yangu una unazi kama sio ushabiki maandazi...

Yaani unasahau kabisa kwamba Yanga bado ana mechi moja mkononi?...

Halafu, wanaoongoza ligi si Mbeya City?....Ama?
Mkuu Mbeya City alikua akiongoza ligi hadi jumatano saa 10.. Baada ya hapo "Wazee wa Kazi" tulikua dimbani, ndipo tukamshusha.

Kua na mechi moja siyo sababu ya nyinyi kuonekana, maana hivi viporo hua vinachacha.. Na kwa jinsi kitakavyowachachia hamtaamini.

Kuhusu ushabiki wangu, Mimi ni Shabiki na Mwanachama kindakindaki wa Simba SC[mtaa wa pili hua mnatuita Taifa Kubwa]
 
Mzunguko wa pili haujaanza majeruhi hawapo watu wanapiga kelele na position mwaka Jana umesahau kiliwakuta nini mtani hii ligi bado sana tuuuuu.
 
Na suruhu nayo pia mligawa dozi? Kumbe mnapoint tisa hadi sasa? Leo Yanga anaongoza ligi sijui manaotafuta round ya nne mwenzenu ya tatu
 
Mzunguko wa pili haujaanza majeruhi hawapo watu wanapiga kelele na position mwaka Jana umesahau kiliwakuta nini mtani hii ligi bado sana tuuuuu.
Mtani haya ni maongezi tu, Kelele bado hazijaanza.
Alafu kuhusu majeruhi msimu huu tuna kikosi kikubwa sana, yaani tunaweza kutengeneza timu 2 za nguvu.. huku kila timu ikiwa na sub zake za hatari.
Na katika kuridhihirisha hili, tumempeleka danny lyanga kwa mkopo nchini Oman. Source [emoji116]
STRAIKA WA SIMBA AKIMBILIA UARABUNI, APATA TIMU, AANZA KAZI - SALEH JEMBE
Ila japo bado ni mapema, sijaona mpaka sasa cha kumzuia Mnyama kutwaa makombe 3 msimu huu.
 
Na suruhu nayo pia mligawa dozi? Kumbe mnapoint tisa hadi sasa? Leo Yanga anaongoza ligi sijui manaotafuta round ya nne mwenzenu ya tatu
Sasa ile ilikua Ni zaidi ya dozi.. Maana wale wajeda walilala na viatu siku hiyo.

Si mbaya mkikaa kwa mda, ila kesho tutawashusha kama tulivyomshusha Mbeya City.
 
Sasa ile ilikua Ni zaidi ya dozi.. Maana wale wajeda walilala na viatu siku hiyo.

Si mbaya mkikaa kwa mda, ila kesho tutawashusha kama tulivyomshusha Mbeya City.
Yanga hawezi ongoza ligi leo, msimamo wa ligi hapo juu namba 2 umekosewa, ukweli ni kwamba Mbeya City nao wana pointi 7 kama Simba na Azam, walitoa sare mechi ya kwanza na Kagera, na baadaye ikazifunga Toto na Mbao. Leo Mbeya City wanacheza na Azam, matokeo ya aina yoyote yale katika mechi hii hayataweza kuwafanya Yanga kuongoza ligi labda nafasi ya pili inawahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…