Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZANGINA S. ZANGINA, KATIBU UENEZI CCM MKOA WA MOROGORO ALIPOKUWA IFAKARA AKIHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Ndugu Zangina S. Zangina alipokuwa akitimiza majukumu yake ya kuhamasisha wananchi wa Ifakara na maeneo mengine ya Mkoa wa Morogoro ili wajitokeze kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa.
Ndugu Zangina alitumia fursa hiyo kuzungumza na viongozi wa Dini mbalimbali ndani ya Kilombero Mkoani Morogoro huku akinukuu Maandiko ya Kitabu cha Warumi. 13:1-2 "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu"
Aidha, Komredi Zangina aliambatana na Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kibaoni na kumuona Baba Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kibaoni Padre Daudi Ndelacho Msaki ili kumsihi awape elimu Waumini wakajiandikishe ambaye alilipokea
Katibu Uenezi Zangina pia, alienda na kutembelea Kituo cha Kujiandikisha cha Saiti kujua maendeleo ya Uandikishaji ambapo alikuta hali ni shwari ambapo aliendelea kuweka hamasa ya kutosha wa wananchi ambao waliendelea kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa.
Vilevile, Katibu Uenezi CCM Mkoa wa Morogoro, Ndugu Zangina pamoja na viongozi alioambatana nao walifika kumuona Imamu Ahmadi Msusa Mgwali wa Msikiti wa Msikiti W Quba uliopo Kibaoni Stesheni ili kumuomba atangaze na kuhimiza Uandikishaji, akalipokea kwa furaha na kusema amefarijika kuona Chama tumemheshimu na kumthamini hata kumfuata kwa Ombi hilo muhimu, ambaye aliingia Msikitini kushika kipaza sauti na kutoa tangazo la Uandikishaji pamoja na elimu kwa Waislamu na Wananchi wa Imani zote waliokuwa wakiyasikia matangazo ya Msikiti kabla ya Sala.
Mwisho, Komredi Zangina alitoa shukurani kwa viongozi wote wa Dini Mkoa wa Morogoro kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.