Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Sera na mipango ya rais Mwinyi inavyoimaliza ACT- Wazalendo kuelekea 2025
Deogratias Mutungi
Utawala bora, Uchumi imara, Demokrasia safi, nidhamu na maadili ya viongozi, Ufanisi na mweleko wa mafanikio ya serikali yoyote ile ulimwenguni upimwa kwa sera na mipango yake kimamlaka na ndani ya mifumo yote ya kitaasisi, Serikali isiyo na sera na mipango mbadala ni dhaifu kwa utawala bora, na usimamizi wa misingi ya sheria na kanuni za uwajibikaji kwa wananchi wake.
Udhaifu wa serikali katika sera na mipango uzalisha ombwe la umaskini na ukosefu wa amani na haki kwa watu wake rejea yaliyotokea Sierra leone, Liberia, Haiti na Niger ni matokeo ya sera na mipango mibovu ya serikali na vyama tawala, Ukosefu wa sera na mipango endelevu kwa serikali ni madhira na hatari kwa taifa na wananchi wake.
Mapinduzi ya Januari 1964, ni ukombozi wa Mzanzibar ili aweze kujitegemea kisera na kuwa na mipango ya kujistawisha kiuchumi na kisiasa, kukosekana kwa sera na mipango madhubuti ni utumwa mambo leo na tishio kwa Wazanzibar wote, Je nini sera na mipango ya awamu ya nane hapa Zanzibar? Kwa muhtasari sera na mipango ya rais Mwinyi ni jumuishi kwa mantiki ya “sera ya umma” ambayo inalenga kutatua changamoto mahususi ndani ya jamii.
Serikali ya awamu ya nane visiwani Zanzibar chini ya rais Mwinyi inajitambulisha kwa sera na mipango mbadala ya utatuaji wa wimbi la matatizo yanayomkabili Mzanzibar wa kawaida, uwepo wa sera na mipango inayoeleweka katika usimamizi wa maendeleo ya watu, ni matokeo ya ubora wa ilani ya Chama. Ilani ya chama na serikali ni sawa na pande mbili za sarafu ambazo kamwe uwezi kuzitenganisha. Ilani mbovu ya chama uzalisha serikali legelege na hatima yake ni mkwamo wa maendeleo ya watu na vitu kisiasa.
Sera na mipango madhubuti ya awamu ya nane ni daraja kuu la mabadiliko ya kiuchumi kwa Wazanzibar, kwa mantiki ilivyo sasa serikali inatimiza kwa kasi kubwa kile ilichokihaidi mwaka 2020 wakati ikiomba kupewa usukani wa dola.
Ifahamike kuwa ACT-Wazalendo ni Chama Kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, ni wazi kuwa ACT-Wazalendo wana nguvu kisiasa hapa Zanzibar, swali ni Je kwa sera na mipango madhubuti ya rais Mwinyi ACT-Wazalendo wataweza kumdhibiti Mwinyi hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025? Au ni agenda zipi ACT, wanazo sasa kuweza kujinadi kwa mwananchi wa kawaida aweze kuelewa na kuwapa ridhaa ya kushika dola? Je ACT-Wazalendo wapo na dhamira ya kweli kushika dola au wanatania kisiasa na ni wasaka tonge na fursa?
Mantiki ya kisiasa hapa ni moja tu, ACT-Wazalendo hawana agenda madhubuti ya kushika dola hapa Zanzibar, wanatania kisiasa na dhamira yao si kushika dola bali kuwa wasindikizaji wa dola na wasaka tonge bin fursa , upo mstari mpana kati ya kushika dola na kuwa msindikizaji wa dola, Viongozi wa ACT, Wanafahamu hilo na wanachama wao wanatambua hilo.
Mwanazuoni nguli Aristotle katika wazo lake kuu la siasa aliwai kusema, “Dola ipo kwa sababu ya kukuza wema na kuleta maisha mazuri kwa raia wake, na si kila kikundi kinaweza kushika na kuongoza dola”
Si kila chama au kikundi cha kisiasa hapa Zanzibar kinaweza kushika dola la asha! Dola si sehemu ya majaribio ya uongozi wala kwenda ikulu kutalii, Ikulu si jumba la maonyesho, bali ipo miiko na miongozo ya kushika dola na kuingia ikulu, inapokiukwa uzalisha tundu la kuzimu kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hoja inayojengwa hapa tukirejea kwa Aristotle ni Je ACT- Wazalendo awaoni mazuri ya serikali ya awamu ya nane bila shaka wanaona, lakini kwa sababu ACT, ni chama cha kisiasa chenye nia ya kushika dola wanaweza kusema hawaoni maendeleo ya kisera na mipango ya awamu ya nane kama ndio hivyo Je wanao uwezo wa kushika dola? au ni kwa asilimia ngapi Wazanzibar wana imani na chama cha ACT- Wazalendo dhidi ya chama cha Mapinduzi CCM?
Mvuto na uwezo wa ACT-Wazalendo hapa Zanzibar unapungua na kuelekea kufifia kabisa, mantiki ya kisiasa inatambulisha asilimia isiyopungua 25% ya ACT, kushika dola dhidi ya asilimia 75% za CCM kurejea kwenye dola tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani 2025, kwa sasa ni vigumu mgombea wa chama chochote hapa visiwani Zanzibar anaweza kushindana na rais Mwinyi na akashinda kupitia sanduku la kura, sababu ni moja tu ametimiza kile alichowahaidi Wazanzibar kupitia ilani ya chama chake CCM.
Uwepo wa kikokotoo hiki cha asilimia za ushindi wa ACT, na CCM visiwani Zanzibar ni matokeo ya ubora na ufanisi unaofanywa na serikali ya rais Mwinyi kwa Wazanzibar, kwa sasa awamu ya nane, imeweza kuwafikia Wazanzibar wote katika kila huduma ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi na pato la mtu mmoja mmoja.
Kinachofanywa na rais Mwinyi ni matokeo ya uzalendo wake kwa nchi na watu wake, dhamira ya kweli ya rais ndio silaha muhimu ya mafanikio ya sasa kwa Wazanzibar, Uzalendo ni nguzo muhimu ya maendeleo na ndicho tunachokiona kwa serikali hii ya awamu ya nane.
Ieleweke kuwa ubora wa Zanzibar ya sasa ni tofauti na Zanzibar ya miaka ishirini iliyopita, asilimia 90% ya Wazanzibar wanaielewa serikali ya rais Mwinyi, kubwa zaidi ikiwa ni namna ilivyoweza kuleta mabadiliko chanya ndani ya maisha yao ya kila siku na namna inavyoendelea kusimamia vipaumbele vya maendeleo vinavyogusa maisha yao kwa namna moja au nyingine.
Ipo wazi kuwa ACT-Wazalendo wanao mtihani mgumu kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025, dhidi ya serikali ya CCM inayoongozwa na rais Mwinyi hapa visiwani Zanzibar, Sera na mipango ya awamu ya nane ndio siri ya ushindi wa kishindo hapa Zanzibar, Aidha uzalendo na falsafa za Zanzibar kwanza ni ishara nyingine ya ushindi wa kishindo kwa rais Mwinyi.